Sitta awasha moto mpya DOWANS

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,794
287,947
  • Asema ni biashara ya kipumbavu na wizi mtupu

na Mwandishi wetu

SIKU chache baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kusajili tuzo ya malipo ya fidia kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, ameibuka na kutoa madai mazito dhidi ya kampuni hiyo, akisema ni ya kikundi cha wezi wachache, wanaopaswa kulaaniwa na kila mzalendo mwenye mapenzi mema kwa taifa hili.

Septemba 28 mwaka huu, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Emilian Mushi, alitupilia mbali pingamizi la baadhi ya wanasiasa na wanaharakati waliotaka kulizuia Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), lisilipe dola za Marekani milioni 65 (sh bilioni 94) kwa Dowans Tanzania kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara (ICC).Tuzo hiyo ilitolewa Novemba 15, mwaka jana na Januari 25 mwaka huu, Dowans iliwasilisha ombi lake la kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania iisajili lakini baadhi ya wanasiasa na wanaharakati walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga tuzo hiyo isisajiliwe.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana kwa njia ya simu, Sitta ambaye ni miongoni mwa makada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa mstari wa mbele kutaka Dowans isilipwe mabilioni hayo, alisema kuwa msimamo wake upo pale pale na kwamba atapambana hadi mwisho."Sikiliza kijana, mbona mnakuwa kama hamna uzalendo, Dowans ni biashara ya kipumbavu…nawashangaa hata hao wanaotulaumu sisi kuwa ndio tumeifikisha nchi katika hatua hiyo ya kutakiwa kulipa deni hilo…Dowans ni wizi ambao kila Mtanzania anapaswa kuulaani ushenzi huo badala ya kushangilia," alisema Sitta ambaye ni Spika mstaafu wa Bunge la tisa.

Kada huyo ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, alifafanua kuwa Tanzania iliingia mkataba na Kampuni ya Richmond ili ifue na kuzalisha umeme lakini cha ajabu humo humo kukafanyika wizi na mkataba huo hewa wakarithishwa Dowans.

"Nakwambia wazi labda kama na wewe gazeti lako hilo ni la kifisadi…lakini sisi Dowans hatukuwapa mkataba bali walirithi wizi wa kampuni hewa, hivyo hatuwezi kubebesha wananchi matatizo ya majizi halafu tukashangilia kuibiwa," alisema Sitta kwa hasira.

Sitta, maarufu kama Spika wa Kasi na Viwango, katika Bunge lililopita alisimama imara pamoja na baadhi ya wabunge waliojipambanua kama wapambanaji wa ufisadi kupinga Kampuni hewa ya Richmond (sasa Dowans) na kuishinikiza serikali ivunje mkataba huo.

Akifafanua zaidi, alisema kuwa Watanzania wanapaswa kuwa na uzalendo wa kulipigania taifa lao badala ya kukatishwa tamaa kwa kutishwa kuwa Dowans lazima ilipwe. Hivyo, alidai kuwa mapambano ya kupinga malipo hayo yasifanyike bado yanaendelea.

"Kwanza nikuhakikishie huu si mwisho wa mapambano…Dowans kulipwa ni sawa na kuhalalisha ushenzi wa majizi hayo…hatuwezi kushangilia, nitapinga hadi mwisho…unanielewa, hatuwezi kulipa wezi," alisisitiza Sitta na kukata simu.ICC iliitia hatiani Tanesco kwa kosa la kuvunja mkataba na Dowans iliyokuwa ikitetewa na wakili wa kimataifa Kennedy Fungamtama na ikaiamuru iilipe tuzo hiyo na riba ya asilimia 7.5.

Hatua hiyo ya kuchelewesha malipo ya tuzo hiyo itaifanya Tanesco sasa kulipa kiasi kikubwa zaidi, kwani riba imekuwa inaongezeka. Hadi siku hukumu inatolewa na Jaji Mushi, Dowans ilikuwa inastahili kulipwa na Tanesco sh bilioni 113 badala ya sh bilioni 94.
 
Huwezi kupambana na wezi walioko ndani ya chama chako!!
Huu ni usanii waTZ wanataka kuonyeshwa ili imani yao na chama isipotee...

Pambana na adui ukiwa upande wake wa pili!!!
 
CCM imewapiga stop yeye na members wenzake wa CCJ kwenda igunga sasa anaona aongee ya Dowans ili tumkumbuke, ametoa kauli nzito sana ila jamaa ni mwoga, anapenda kufoka akiwa chini ya meza.
 
aaaah wale wale tu, hana jipya amechukua hatua gani? kama kweli anamapenzi ya kweli na taifa hili atutajie hao wajanja wachache.
 
Huwezi kupambana na wezi walioko ndani ya chama chako!!
Huu ni usanii waTZ wanataka kuonyeshwa ili imani yao na chama isipotee...

Pambana na adui ukiwa upande wake wa pili!!!

Huyu naye Sita ni msanii tuu, kwa hatua hii tuliyofikia jahazi la Tanzania yetu tuipewndayo linazidi kuzama!!!!!!!! Huo ni mgao wa watu fulani ndani ya uongozi wa nchi hii, wanafanya dhuruma lakini mwisho wa siku wataumbuka Mungu wetu hawezi kuvumilia wezi!!!!!!!!!!

Yeye Sita aliona mambo yote ya usanii wa RICHMOND akiwa spika wa bunge mbona hakuweza kuzuia hii taflani ya hasara kwa taifa letu, anangojea tumeingia mkenge anaimba usanii wake, yeye ni maghamba pia!!!!!!
 
Yupo ndani ya Meli iliyo kumba na dhoruba ajitose baharini au akomae hadi dhoruba itakapo tulia?
 
"Sikiliza kijana, mbona mnakuwa kama hamna uzalendo, Dowans ni biashara ya kipumbavu…nawashangaa hata hao wanaotulaumu sisi kuwa ndio tumeifikisha nchi katika hatua hiyo ya kutakiwa kulipa deni hilo…Dowans ni wizi ambao kila Mtanzania anapaswa kuulaani ushenzi huo badala ya kushangilia,"

Huyu Mzee anazunguka nini? Anachokijua kwenye red atwambie bayana banaaa.
 
Aaaaaa wale wale hana lolote,unaongelea kwenye vyombo vya habari,chukua hatua tujue una machungu na sie wananchi.
 
CCM imewapiga stop yeye na members wenzake wa CCJ kwenda igunga sasa anaona aongee ya Dowans ili tumkumbuke, ametoa kauli nzito sana ila jamaa ni mwoga, anapenda kufoka akiwa chini ya meza.
Sawa sawa FUSO kumbe jamaa umemuelewa, anatafuta popularity hanalolote huyo aonyeshe atachukua hatua gani sasa kuzuia hayo malipo!!!!! Jmaa wamechungulia mrahaba wa Buzwagi na Geita Gold Mine USD $ 65,000,000/= wanataka wachukue hizo, maskini Tanzania niipendayo!!!!!!!!!
 
CCM imewapiga stop yeye na members wenzake wa CCJ kwenda igunga sasa anaona aongee ya Dowans ili tumkumbuke, ametoa kauli nzito sana ila jamaa ni mwoga, anapenda kufoka akiwa chini ya meza.
Sawa sawa FUSO kumbe jamaa umemuelewa, anatafuta popularity hanalolote huyo aonyeshe atachukua hatua gani sasa kuzuia hayo malipo!!!!! Jmaa wamechungulia mrahaba wa Buzwagi na Geita Gold Mine USD $ 65,000,000/= wanataka wachukue hizo, maskini Tanzania niipendayo!!!!!!!!!
 
Huyu Sitta hata mie siumuelewi! haiwezekani Ngo'mbe akalala katikati ya Simba! hata kama simba hao wameshiba lazima watamlamba hata nywele! Hao wote wamoja tu! Hakuna mkweli yuko mpaka sasa CCM tena na Madaraka makubwa! Ajitoe huko then atueleze ukweli tutamuelewa Zaidi!
 
Hana lolote akiitwa na cc ya magamba ana uwezo wa kusema na kuthibitisha hayo anayoyasema??????alishaniboa toka yeye na wale waliojipambanua kuwa wapambanaji wa ufisadi waliponyamazishwa na kuikimbia hoja ya richmond.
 
Huyu Sitta hata mie siumuelewi! haiwezekani Ngo'mbe akalala katikati ya Simba! hata kama simba hao wameshiba lazima watamlamba hata nywele! Hao wote wamoja tu! Hakuna mkweli yuko mpaka sasa CCM tena na Madaraka makubwa! Ajitoe huko then atueleze ukweli tutamuelewa Zaidi!


Sipati picha haya maandalizi ya Uraisi hapo 2015 kazi ipo kila mtu anajarib kuonyesha njinsi gani anaweza kuogerea ndani ya kina kirefu cha maji. six kaza mwendo.
 
yeye naye mwizi tu, mbwa ya mtu ikiuma na kusababisha madhara anaye paswa kulipa ni mwenye mbwa.
 
Kama ilikuwa kijua ni wizi mtupu mbona lisitisha mjadala ndani ya bunge alipokuwa Spika baada ya kutishiwa kunyang'anywa kadi ya ccm? Mnafiki mkubwa sana huyu.
 
sita ni ***** san hili..yaani linapayuka hovyo hovyo tu ...lioga ka nini si alitaka kupokwa kadi ya ccm akalia na kuomba msamaha huyu
 
Sitta ni mwizi tu yeye! hana ubavu wowote au uwezo wa kufanya lolote! Kama kidume angejiunga na ccj...hahaha!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom