Sitta awasha moto mpya DOWANS

Sitta awasha moto mpya DOWANS

Samwel Sitta huyu alikuwa Spika wa Bunge alikuwa na nguvu kubwa ya kupambana na Richmond na Dowans/Syimbyon zisingezaliwa.Nimesema na ninarudia tena na nitarudia nitakapokuwa naomba kura 2015 jimboni huyu ni mmoja wa Watanzania waliolifikisha Taifa hapa lilipo kwa Unafiki wao. Sitta ni Mnafiki sana.
 
6 anachuki tu na hao DOWANS yeye hana hata chembe ya usafi,ilikuwaje akatumia mamilioni ya walipa kodi kujenga ofisi ya spika urambo? so aache unafiki wake
 
Naomba tuelewane, mkirejea kwenye post yangu nimesema, sita ni mwadamu kama wewe, anayo mazuri na mabaya yake aliyoyafanya, lakini katika kazi aliyoifanya akiwa kama speaker, lazima tukiri amefanya mambo mengi ambayo mimi na wewe kwa namna yoyote lazima tukiri.

Yupi bora, anaekaa kwenye vikao akatoa hoja ikakataliwa na akanyamaza au anayejitokeza na kusema hadharan KUTORIDHISHWA KWAKE JUU YA MWENENDO FULANI! NANI AIYEJUA TANZANIA ILIVYOHARIBIKA?

NANI ASIYEJUA UMAFIA UNAOENDELEA?NANI ASIYEJUA SYNDICATE INANYOZUNGUMZWA? NA WANGAPI WAMESHIKA MADARAKA MAKUBWA KAMA SITA HAPA NCHINI? NA WANGAPI WALIKUWA NA MATEGEMEO MAKUBWA JUU YA UONGOZI ILA HAYAKUTIMIA LAKINI SOR FAR WAMEFANYA NINI?

UNAWASIKIA? KWA NINI SITA ANASIKIKA NA HARAKATI ZAKE SI ZA LEO WALA JANA WALA JUZI?HUYU MTU TUMUHUMU KWA HAKI!WATU WENGI WAPO NYUMA YAKE TENA WENGI NDANI YA CCM NADHANI NI MTU ANYEWEZA KUONEKANA LABDA NA MAGUFULI! WATU HUWA WANATELEZA!

NAKUMBUKA JUZI ALIWESEMA WAPINZANI KUWA NI VYAMA VYA MSIMU, WENYEWE NI KUBEZA TU HATA MIMI SIKUFURAHI KWANI MIMI NI MPINZANII LAKINI YULE NI MTU KAMA WEWE! NI SAWA NA MAGUFULI ALIPOKUWA ANAMPIGIA DEBE KAFUMU KUWA WAKIMCHAGUA ATAJENGA BARABARA!

HUO NI UTELEZI!AJALI ZA MANENO KAMA HIZI HUWA ZIPO! SITTA NA MSIFU SANA NI MJASIRI NA ANAWEZA KUDHUBUTU!KAWAFUNGUA MACHO WATANZANIA WALIO WENGI ALIPOKUWA SPEAKER, KARUHUSU MIJADALA MINGI SANA AMBAYO ILIFUNIKWA SIKU ZA NYUMA NA SASA TUNAONA INAFUNIKWA!YEYE ALIFANYA KAZI YAKE!

KAZI ILIYOBAKI YA UTEKELEZAJI HAIKUWA YA SITTA LAZIMA TUELEWE!KILA KITU KINA SEHEMU YAKE KWA SETUP YA HII NCHI!ULITAKA AWAFUNGE YEYE KAMA SPEAKER?SIDHANI KAMA ANA MAMLAKA HAYO!HUYU NI MTU MWENYE UDHUBUTU, ALISHAWAHI KUMWAMBIA RAIS '' UWE MKALI''JAMANI NANI ALISHAWAHI SEMA MANENO KAMA HAYA NDANI YA SYSTEM YAO????

TUKUBALI 6 NI MTU AMBAYE AIBA YAKE NA USHAWISHI VINARIDHISHA!
 
Tatizo la nchi za kiafrica ni kukumbatia wazee hata kama umri wao wa kufanya kazi umeshapitiliza mfano hai ni huyu babu Sitta
 
Huyu Sitta ANACHEZA NA AKILI ZETU, yeye nae pia ni wale wale!
 
Anaongea maneno mazuri lakini ni kama debe tupu ambalo haliachi kuvuma, hawezi kata mkono wake kwa kisu alichokishika na mkono huo huo
 
Sasa baada ya kusema hayo what next?Sitta tuambie utafanya nini?kupinga mahakama au kutujaza chuki pasipo kutueleza solution ni nini?mzee wangu acha kutafuta cheap popularity
 
Huyu mzee ni mzalendo sana, ila huwa wakati fulani anajisahau. Alipowaita wapinzani kuwa wanafiki wakati yeye mwenyewe ana msimamo wa upinzania, nilimuonea huruma sana. CV ilisheki kidogo. asikate tamaa
 
Uchaguzi wa urais 2015 magamba wanasafari ndefu maana kila mwenye mic anapayuka kadri anavyoweza, yeye yuko kwenye cabinet kwanini asilisemee huko na kufanya maamuzi huko wakimkatalia ajiuzulu tujue kweli anapingana na vitendo hivyo vya "kipumbavu" na "Ushenzi" vinginevyo nae ni sehemu ya huo upumbavu na ushenzi
 
Tatizo la nchi za kiafrica ni kukumbatia wazee hata kama umri wao wa kufanya kazi umeshapitiliza mfano hai ni huyu babu Sitta

Makupa,

Issue hapa si umri.Kinachotakiwa ni HEKIMA.BUSARA na UTASHI wa kuwatumikia Watanzania/Wananchi.

Juzi kule Zambia wenzetu wamempa Bwana Michael Sata mwenye umri wa MIAKA 74 kuwa Rais wa Nchi(The highest office in the country) Watu wanaamini kuwa mtu anapokuwa mzee na busara zinaongezeka. Unaweza kuweka vijana kwenye uongozi na bado wakapwaya kama tunavyoona akina Ngeleja,Malima(Nishati/Madini),Januari Makamba(MB/M-kiti Kamati Nishati na Madini),Nape Nnauye K/Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Magamba-CCM.

Sitta ni mojawapo ya Wana-magamba ambaye anajitofautisha na mfumo mzima wa CCM. Tuliona vitu vyake wakti akiwa Spika wa Bunge lililopita. Hizi habari anazoongea ni UKWELI MTUPU.
Pengine mimi ningelipenda kumpa ushauri wa bure Mhe.Sitta kwamba anatakiwa KUJITOA CCM na kujiunga na upinzani hasa CHADEMA!
 
Mzee 6 aoneshe uzalendo wake kwa Kuhama nyumba ya Spika na Kuokoa hela zetu watanzania Shs 12,000,000/- za serikali zanazolipiwa pango hilo la nyumba ya spika wakati yeye siyo spika!
Fisadi ni fisadi hata akiiba au kutumia ndivo sivyo senti moja ya Umma!
Kama alishindwa kukataa Posho(Ujira wa Mwiha) nani atamwani!
Hizi 94M alipe yeye na Kikosi chake wala asijikoshe!
 
Sikatai kwamba labda Sita na wenzake wana personal interest katika hili, lakini akikaa kimya halafu hizo hela zikalipwa tutakuwa tumemkomoa nani, wala siyo Sita, bali kila mtanzania atasugua meno maana katika kuzilipa. Mimi nawahakikishia wenye DOWANS wanafurahi sana wakiona argument zenu, maana wanajua kumbe sasa tuna support.

Cha muhimu deni lisilipwe kwa sababu ni wazi hizo pesa tunatapeliwa, hata kichaa analijua hilo, na tusitegemee judicial system yetu itatusaidia katika hilo, tunachotakiwa ni kukomaa tu katika kukataa deni lisilipwe.
Tunachomtaka sita afanye ni kumtaja mtu/watu aliyesitiriwa na ile kamati. Sita hawezi kututaka tulaani tu, baada ya kulaani iweje??? Sita anakerwa na na wizi wa dowans wakati huohuo hataki kuweka siri za hili sakata wazi. Kama dowans wanafurahia sisi kumtaka sita awaumbue kwetu, basi kazi ipo.
 
SAMMOSSES:
Watanzania wenzangu,tufike mahali tuseme basi inatosha kufanyakichwa cha mwendawazimu!ah! leo hii Sitta anang'aka kama kweli ni mzalendo.Yeye alikuwa kiongozi wa mhimili mmojawapo wa dola katika ya mihimili mitatu.Kinachonishangaza ujasiri huu ameupata wapi hivi sasa ilihali yeye ndiye aliyezima hoja ya Richmond bungeni.Akili zetu si mgando kama anavyofikiri,hatuna ubongo wa panzi wa kusahau mapema na wazito wa kuelewa.Tunaamini ulikuwa kinara mzuri katika kufanikisha hoja nzito kuwasiolishwa bungeni lakini ulikuwa bingwa mkubwa wa kuzuia hoja zenye tija na maslahi kwa wananchi na taifa hili,ndo maana tunajiuliza ujasiri huu umeupata wapi katika kipindi hiki?

Tatizo la hawa watu wanaimba kijamaa huku wanacheza kibepari.Dhihirisha uzalendo wako leo hii kwa step down kama kweli wewe ni mzalendo,mwambie bwana mkubwa unachoamini kinapingana na dhamira yako.sisi kukaa underground nakuloloma huku ukiendelea kujilimbikizi mijiposho isiyo na tija kwa nchi na wananchi wake
 
Samwel Sitta na John Magufuli ndio turufu pekee CCM ilizobaki nazo, kama CCM itataka kuendelea kushika the highest office katika nchi hii.

Wana mapungufu yao, so is every body else, lakini wana misimamo isiyotetereka katika kutetea maslahi ya umma. Na hapa im not talking about
the petty issues wengi wenu mlioreffer kama ni ishara ya ufisadi wake, naongelea mambo mazito yenye kuweza kuipeleka nchi hii mbele ndani ya miaka 10 tu. Mfano mikataba ya kinyonyaji, ufisadi mkubwa wa kalamu, na ufujaji wa kitaasisi.

Tatizo wamekanyagana na magamba wenzao wengi katika kujitofautisha kimsimamo na matokeo yake, kuna watu wanareact kwa jina tu bila hata
kusikia amesema nini.

Igunga imetoa mwelekeo wa chaguzi zijazo, na Igunga imeonesha, kwa CCM kuwa na any chance ya kuendelea kutawala, karata ya kupeana zamu sijui uzanzibari, jinsia, ukanda, sijui nini havitafua dafu kwa mchakamchaka wa CHADEMA. Na kama wakitia pamba masikioni wakaamua kupata mtu wa uvuguvugu basi kuna hatari ya umwagaji damu, au maafa ya Kenya, maana tume ya taifa ya uchaguzi itakua na kazi ya ziada kutangaza mshindi.

CCM inaweza kuwa na chance kama kitamsimamisha mmoja kati ya hawa wawili, provided hawatatumbukia kwenye any major scandal between now and 2015.

Adios.
 
Sita sio mnafiki nchi hii tuu bali ni africa mashariki na kati na kusini mwa jangwa la sahara na vitongoji vyake,,sita hana dhamira ya kweli bali tatizo ni uwaziri mkuu kama alivyosema lowasa wakati akijiuzulu,, wala hana dhamira ya kweli ya kupigania ufisadi yeye pamoja na kundi lao wanaojipambanua bali ni siasa za chuki binafsi zimewajaa
 
Nakuunga mkono. Pamoja na usanii na unafiki wa Sitta hastahili kushambuliwa katika kutetea Tanzania katika malipo haya (Shilingi bilioni 113) yaliyojaa ufisadi wa hali ya juu yanayotaka kufanywa dhidi ya kampuni hewa ya Dowans. Wako wapi hao Watanzania ndani ya chama ambao si wanafiki au wasanii wasimame hadharani kama alivyofanya Sitta kutoa kauli za kupinga malipo haya ya wizi wa mchana kweupe.

Watu hawajui kwamba kwa kumshambulia Sitta basi wananyamazisha sauti moja ya Mtanzania mwenzetu katika kutetea maslahi ya nchi. Inawezekana kabisa Sitta ni mwizi, msanii, mnafiki n.k. lakini katika hili la kupinga malipo yanayotaka kufanywa dhidi ya Dowans, Sitta hajakosea lolote na anastahili kuungwa mkono na Watanzania wote ambao ni wapenda haki na wako mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya nchi.

Sioni sababu yoyote ili ya kumnyamazisha Sitta na kuwarahisishia mafisadi kulipana shilingi 113 bilioni pesa ambayo hawakuitolea jasho kabisa, ikumbukwe mitambo ile inadaiwa imeshauzwa kwa Symbion kwa shilingi bilioni 120.

Kuikosoa CCM/Serikali si lazima uwe nje ya CCM, wako wanachama chungu nzima ndani ya CCM ambao wanaikosoa CCM/serikali na wengineo kati ya hao waliwahi kushika nyadhifa za juu ndani ya CCM na Serikali.

Hatu msemi kwa sababu ya kupinga malipo yasi lipwe tunamsema kutokana na unafiki wake, Alipokuwa Spika alikuwa nauwezo wa kulimaliza ili tatizo lakini baada ya walichokihitaji kutimia yaani EL kuutema U waziri mkuu, vita ikawaimeishia hapo. Hawakutaka kuangalia kisheria mkataba unaweza kuvunjwa au la! wao waliamua kusonga mbele wakati wanajua wazi kuwa mikataba yenyewe imeingiwa kifisadi hivyo hata conditions zilizomo kwenye mikataba hiyo ni ya kutuumiza sisi waTZ, kumbuka mwakyembe na sitta ni wanasheria lakini hilo wakalipuuza. Tuseme walipitiwa lakini BUNGE lilisha azimia waliotuingiza ktk dhahama hii waazibiwe serikali ikaanz kupiga danadana Badala ya Sitta kukomaa ili maazimio ya Bunge yatekelezwe akakubaliana na chama chake wakalimaliza suala hilo kisanii tulipo lalama yeye akadai maazimio yametekelezwa na yaliobaki yatatekelezwa mjadala umefungwa, sasa kiko wapi? Waliotuingiza mkenge wapo serikalini wanapeta, waliokuwa wanawalinda mf Mkurugenzi PCCB hadi leo anakula bata. Umeme hatuna hadi leo giza totoro, mitambo ileile ya dowans sasa imebadili jina ni symbion na tunalipishwa hela ndefu si tuna shida ! Kesi tumeshindwa tukiendelea kukata rufaa riba ndio inaongezeka kwa kwenda mbelle yeye anasema tusilipe. Je tusipo lipa nini kitafuata? inamaana Sitta hajui kuwa wenyewe tumeridhia sheria za kimataifa kwa kusaini makubaliano ya kuziheshimu, kuzitii na kuzitekeleza sheria za kimataifa pindi tutakapoingia ktk kuzitumia! Aoni kutuambia tusilipe anaongeza tatizo badala ya kulipunguza au kuliondoa? Soma maelezo yake yote hatoi suluhisho yeye anasema tusilipe tu basi, je tusipolipa nini kitatupata hazungumzii.
Mwisho RA anakusanya malipo yote tutakayolipa kama fidia lakini Sitta anajifanya haoni au hajui kuwa RA bado ni mwanaccm na yeye ndie kawafadhili helkopta ktk uchaguzi igunga, hivyo ni mwenzao na swahiba wao na ni mfadhili wao pia. Sasa kama yeye ni mkweli na anauchungu na taifa hili kwanini asitoke uko alipo ccm na kujiunga na CHAUSTA,SAU au NLD kama anaogopa kwenda CUF au CDM maana CCJ imejifia kifo cha mende, tunaitaji afanye maamuzi mazito kuonyesha kweli anapinga hayo malipo na si longolongo tu anazozitoa ktk media
 
Makupa,

Issue hapa si umri.Kinachotakiwa ni HEKIMA.BUSARA na UTASHI wa kuwatumikia Watanzania/Wananchi.

Juzi kule Zambia wenzetu wamempa Bwana Michael Sata mwenye umri wa MIAKA 74 kuwa Rais wa Nchi(The highest office in the country) Watu wanaamini kuwa mtu anapokuwa mzee na busara zinaongezeka. Unaweza kuweka vijana kwenye uongozi na bado wakapwaya kama tunavyoona akina Ngeleja,Malima(Nishati/Madini),Januari Makamba(MB/M-kiti Kamati Nishati na Madini),Nape Nnauye K/Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Magamba-CCM.

Sitta ni mojawapo ya Wana-magamba ambaye anajitofautisha na mfumo mzima wa CCM. Tuliona vitu vyake wakti akiwa Spika wa Bunge lililopita. Hizi habari anazoongea ni UKWELI MTUPU.
Pengine mimi ningelipenda kumpa ushauri wa bure Mhe.Sitta kwamba anatakiwa KUJITOA CCM na kujiunga na upinzani hasa CHADEMA!

Makoye,
Huyu mzee wakati akiwa spika alikuwa na nia ya kujipatia umaarufu tu na si vinginevyo, sio siri haya malipo ya dowans ambayo serikali inatakiwa kulipa chanzo ni sitta na kundi lake uchwara la wapapanaji w ufisadi
 
Back
Top Bottom