BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
- Thread starter
- #81
Hatu msemi kwa sababu ya kupinga malipo yasi lipwe tunamsema kutokana na unafiki wake, Alipokuwa Spika alikuwa nauwezo wa kulimaliza ili tatizo lakini baada ya walichokihitaji kutimia yaani EL kuutema U waziri mkuu, vita ikawaimeishia hapo. Hawakutaka kuangalia kisheria mkataba unaweza kuvunjwa au la! wao waliamua kusonga mbele wakati wanajua wazi kuwa mikataba yenyewe imeingiwa kifisadi hivyo hata conditions zilizomo kwenye mikataba hiyo ni ya kutuumiza sisi waTZ, kumbuka mwakyembe na sitta ni wanasheria lakini hilo wakalipuuza. Tuseme walipitiwa lakini BUNGE lilisha azimia waliotuingiza ktk dhahama hii waazibiwe serikali ikaanz kupiga danadana Badala ya Sitta kukomaa ili maazimio ya Bunge yatekelezwe akakubaliana na chama chake wakalimaliza suala hilo kisanii tulipo lalama yeye akadai maazimio yametekelezwa na yaliobaki yatatekelezwa mjadala umefungwa, sasa kiko wapi? Waliotuingiza mkenge wapo serikalini wanapeta, waliokuwa wanawalinda mf Mkurugenzi PCCB hadi leo anakula bata. Umeme hatuna hadi leo giza totoro, mitambo ileile ya dowans sasa imebadili jina ni symbion na tunalipishwa hela ndefu si tuna shida ! Kesi tumeshindwa tukiendelea kukata rufaa riba ndio inaongezeka kwa kwenda mbelle yeye anasema tusilipe. Je tusipo lipa nini kitafuata? inamaana Sitta hajui kuwa wenyewe tumeridhia sheria za kimataifa kwa kusaini makubaliano ya kuziheshimu, kuzitii na kuzitekeleza sheria za kimataifa pindi tutakapoingia ktk kuzitumia! Aoni kutuambia tusilipe anaongeza tatizo badala ya kulipunguza au kuliondoa? Soma maelezo yake yote hatoi suluhisho yeye anasema tusilipe tu basi, je tusipolipa nini kitatupata hazungumzii.
Mwisho RA anakusanya malipo yote tutakayolipa kama fidia lakini Sitta anajifanya haoni au hajui kuwa RA bado ni mwanaccm na yeye ndie kawafadhili helkopta ktk uchaguzi igunga, hivyo ni mwenzao na swahiba wao na ni mfadhili wao pia. Sasa kama yeye ni mkweli na anauchungu na taifa hili kwanini asitoke uko alipo ccm na kujiunga na CHAUSTA,SAU au NLD kama anaogopa kwenda CUF au CDM maana CCJ imejifia kifo cha mende, tunaitaji afanye maamuzi mazito kuonyesha kweli anapinga hayo malipo na si longolongo tu anazozitoa ktk media
Weka pembeni unafiki wa Sitta au hata ufisadi lakini kwa kauli hii aliyoitoa hastahili kulaumiwa hata kidogo. Wako wapi hao ambao si wanafiki na mafisadi ndani ya CCM watoe kauli kama ya Sitta kupinga malipo haya? Huyo Magufuli ambaye baadhi wameshaanza kumpigia debe la 2015 umemsikia katamka lolote kupinga malipo haya ya kifisadi? Hao akina Asha Migiro na Hussein Mwinyi ambao nao wanadhaniwa wanaweza kuingia Ikulu 2015 umeshawasikia kupinga kuhusu malipo hayo ya kifisadi yanayotaka kufanywa kwa Dowans. Pinda naye yuko kimya na huyo aliyekuwemo Ikulu sasa hivi wala hatii neno kama vile haoni uchungu dhidi ya wizi huu unaoataka kufanywa na kundi la mafisadi wachache. Unafiki wa Sitta na hata ufisadi wake ujadiliwe lakini hii kauli yake ya kutetea maslahi ya Tanzania haistahili kabisa kulaumiwa na Watanzania ila ni kuunga mkono na kuhakikisha malipo hayo ya kifisadi hayafanyiki.