Sitta awafungulia mashtaka Lowassa, Rostam CCM

Katika mazungumzo yake hayo na gazeti hili, Sitta alitamka kwamba ingawa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rostam Aziz, Mbunge wa zamani wa Igunga na mfanyabiashara tajiri, ndiyo aliowataja kwa tuhuma za ufisadi, anafahamu pia mafisadi wengine walio ndani ya CCM lakini ameamua tu kuwataja hao kwa sasa.
Hapa ana maana shida yake hasa ni kupambana na Lowassa, siyo mafisadi....Mafisadi wengine hata kama wapo na wanaathiri maendeleo ya nchi hiyo haigusi kwa sana kwa vile hawamnyimi usingizi kwenye ndoto yake ya urais... ukishamuelewa vizuri hapo, hupati tena shida kujua ubongo wa mtu huyo.
 
Sita sawa na Mugabe, yupo tayari kusema/kufanya lolote ii mradi aende magogoni. Sitta, Malecela, Mukama, Makamba X2, Membe, Zito, Nchimbi, Lyatonga, Lipumba na Slaa wote ni hasara

mimi naona bora uliowataja kuliko anayenajisi makanisa na misikiti kwa rushwa zake anazogawa kama njugu!
 
page 4.JPG sitta+lowassa.jpg images.jpg ​

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema amewashitaki wanasiasa wenzake, Edward Lowassa na Rostam Aziz, kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo vyao vya kifisadi.

Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu, Sitta alisema tayari amewasilisha vielelezo vya ushahidi wake ndani ya chama hicho na anachosubiri kwa sasa ni majibu ya tuhuma zake hizo. "Tayari nimepeleka maelezo yangu kwenye chama kwa ajili ya kuchukua hatua. Haya mambo ninayoyazungumza kila siku si porojo bali ni ukweli na nina vielelezo vya kuthibitisha hayo na tayari nimevipeleka kwenye chama," alisema Sitta, mwanasiasa mkongwe ambaye amewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Sitta hakutaka kuingia undani wa tuhuma alizozitoa kwa maelezo kwamba anasubiri kwanza chama kitoe majibu ya hoja zake.

Katika mazungumzo yake hayo na gazeti hili, Sitta alitamka kwamba ingawa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rostam Aziz, Mbunge wa zamani wa Igunga na mfanyabiashara tajiri, ndiyo aliowataja kwa tuhuma za ufisadi, anafahamu pia mafisadi wengine walio ndani ya CCM lakini ameamua tu kuwataja hao kwa sasa.
Sitta alikuwa akijibu tuhuma za Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba, aliyezungumza na gazeti hili juzi Jumatatu na kudai kwamba chama hicho hakina mafisadi na kwamba wanaosema hivyo wanakivuruga chama badala ya kukijenga.

Katika maelezo yake, Makamba alisema; "Kama akina Lowassa wangekuwa mafisadi, wangekuwa tayari wamechukuliwa hatua na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) au vyombo vingine vya dola.
"Kama hawajachukuliwa hatua na bado ni viongozi halali waliopitishwa na chama kwenye nyadhifa zao, basi watu hao si mafisadi. Sitta anatakiwa awataje kwa majina mafisadi anaowasema badala ya kulitumia neno hilo kuzungumza kijumlajumla," alisema.

Akizungumza kwa utulivu, Sitta alisema kisiasa, mtu haondokewi na tuhuma za ufisadi kwa vile tu hajakamatwa na vyombo vya dola au ushahidi dhidi ya tuhuma zake haujapatikana.
"Kwenye siasa, mtu kujulikana kama fisadi au si fisadi hakutokani na kutokamatwa na vyombo husika. Ni tabia ambayo mtu unaionyesha kwa jamii ndiyo inakuwa taswira yako. "Ndiyo maana, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba mke wa Kaisari hatakiwi kutuhumiwa kwa uchafu. Hata kama hakufanya makosa, kule kutuhumiwa tu ni kubaya.

"Kwa bahati nzuri, namfahamu vizuri Makamba. Nafahamu kwamba ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakipokea pesa kutoka kwa Lowassa na Rostam. Sasa anapokuja hadharani na kuwatetea mimi sioni cha ajabu.
"Watu kama akina Makamba ndiyo wamelea ufisadi katika nchi hii. Ninaposema Makamba ni mlezi wa mafisadi sisemi kwa bahati mbaya bali kwa sababu nafahamu misaada wanayompa," alisema Sitta.

Akizungumzia suala la kukamatwa kwa mafisadi, Sitta alisema lina ugumu kwa sababu, kwa tabia, mafisadi ni watu wajanja na wanaofanya mambo yao katika usiri mkubwa na wana mahusiano na watu walio katika mfumo.
Alisema kama Tanzania haitakuwa tayari kupambana na mfumo uliopo ambao unalea mafisadi na ufisadi, itakuwa ngumu kupambana na rushwa ambayo alisema ndiyo adui mkuu wa nchi kwa sasa.

Hii si mara ya kwanza kwa wanasiasa kuweka hadharani tuhuma kati yao, mara ya kwanza ilikuwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kudai Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewahi kupewa fedha na Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono ili pamoja na mambo mengine, kumhujumu aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Musoma Vijijini katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Kutokana na tuhuma hizo, Zitto naye alikuwa mkali akisema anatumaini Mkono pia amemwambia Lissu kwamba Mbowe naye aliwahi kuchota mabilioni kadhaa kutoka Mkono, licha ya Mkono kutambuliwa na chama hicho kuwa ni fisadi.
Katika majibu yake kuhusu tuhuma hizo, Mbowe ambaye ametishia kumshitaki Zitto, alisema kuchukua fedha kutoka kwa yeyote akiwamo Rais Jakaya Kikwete au CCM si tatizo bali tatizo ni nia iliyopo kuhusu fedha unazochukua.
 
Sitta hajapona majeraha ya kudodondoshwa uspika sasa unajitengenezea vidonda vya tumbo.

Sitta, naona utu uzee wako unakupeleka pabaya. Lowassa na Rostam ni ngoma nzito huiwezi.

Naona Sitta kishajijuwa kuwa hata uwaziri wa geresha aliopewa sasa hanao tena, ameamuwa kutapatapa.

Nakushauri Sitta, uwache siasa majitaka, kama una lolote kaa chini uzungumze na Lowassa mkubaliane yaishe, haikusaidii kitu kutapatapa vyombo vya habari.
 
Ushahidi unapelekwa mahakamani ndo ambako hatua kali za kisheria zinachukulia kwa mafisadi
 
Yeye kama kweli ni mpiganaji kwanini alikubali kupewa uwaziri chini ya JK? Ukishakuwa waziri kazi yako ni kuitetea serikali siyo wananchi tena, kwahiyo Sitta ulibugi mwenyewe step.
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema amewashitaki wanasiasa wenzake, Edward Lowassa na Rostam Aziz, kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo vyao vya kifisadi.
Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu, Sitta alisema tayari amewasilisha vielelezo vya ushahidi wake ndani ya chama hicho na anachosubiri kwa sasa ni majibu ya tuhuma zake hizo.

“Tayari nimepeleka maelezo yangu kwenye chama kwa ajili ya kuchukua hatua. Haya mambo ninayoyazungumza kila siku si porojo bali ni ukweli na nina vielelezo vya kuthibitisha hayo na tayari nimevipeleka kwenye chama,” alisema Sitta, mwanasiasa mkongwe ambaye amewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.
Sitta hakutaka kuingia undani wa tuhuma alizozitoa kwa maelezo kwamba anasubiri kwanza chama kitoe majibu ya hoja zake.

Katika mazungumzo yake hayo na gazeti hili, Sitta alitamka kwamba ingawa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Rostam Aziz, Mbunge wa zamani wa Igunga na mfanyabiashara tajiri, ndiyo aliowataja kwa tuhuma za ufisadi, anafahamu pia mafisadi wengine walio ndani ya CCM lakini ameamua tu kuwataja hao kwa sasa.
Sitta alikuwa akijibu tuhuma za Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba, aliyezungumza na gazeti hili juzi Jumatatu na kudai kwamba chama hicho hakina mafisadi na kwamba wanaosema hivyo wanakivuruga chama badala ya kukijenga.

Katika maelezo yake, Makamba alisema; “Kama akina Lowassa wangekuwa mafisadi, wangekuwa tayari wamechukuliwa hatua na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) au vyombo vingine vya dola.
“Kama hawajachukuliwa hatua na bado ni viongozi halali waliopitishwa na chama kwenye nyadhifa zao, basi watu hao si mafisadi. Sitta anatakiwa awataje kwa majina mafisadi anaowasema badala ya kulitumia neno hilo kuzungumza kijumlajumla,” alisema.

Akizungumza kwa utulivu, Sitta alisema kisiasa, mtu haondokewi na tuhuma za ufisadi kwa vile tu hajakamatwa na vyombo vya dola au ushahidi dhidi ya tuhuma zake haujapatikana.
“Kwenye siasa, mtu kujulikana kama fisadi au si fisadi hakutokani na kutokamatwa na vyombo husika. Ni tabia ambayo mtu unaionyesha kwa jamii ndiyo inakuwa taswira yako. “Ndiyo maana, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba mke wa Kaisari hatakiwi kutuhumiwa kwa uchafu. Hata kama hakufanya makosa, kule kutuhumiwa tu ni kubaya.

“Kwa bahati nzuri, namfahamu vizuri Makamba. Nafahamu kwamba ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakipokea pesa kutoka kwa Lowassa na Rostam. Sasa anapokuja hadharani na kuwatetea mimi sioni cha ajabu.
“Watu kama akina Makamba ndiyo wamelea ufisadi katika nchi hii. Ninaposema Makamba ni mlezi wa mafisadi sisemi kwa bahati mbaya bali kwa sababu nafahamu misaada wanayompa,” alisema Sitta.

Akizungumzia suala la kukamatwa kwa mafisadi, Sitta alisema lina ugumu kwa sababu, kwa tabia, mafisadi ni watu wajanja na wanaofanya mambo yao katika usiri mkubwa na wana mahusiano na watu walio katika mfumo.
Alisema kama Tanzania haitakuwa tayari kupambana na mfumo uliopo ambao unalea mafisadi na ufisadi, itakuwa ngumu kupambana na rushwa ambayo alisema ndiyo adui mkuu wa nchi kwa sasa.

Hii si mara ya kwanza kwa wanasiasa kuweka hadharani tuhuma kati yao, mara ya kwanza ilikuwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kudai Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewahi kupewa fedha na Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono ili pamoja na mambo mengine, kumhujumu aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Musoma Vijijini katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Kutokana na tuhuma hizo, Zitto naye alikuwa mkali akisema anatumaini Mkono pia amemwambia Lissu kwamba Mbowe naye aliwahi kuchota mabilioni kadhaa kutoka Mkono, licha ya Mkono kutambuliwa na chama hicho kuwa ni fisadi.
Katika majibu yake kuhusu tuhuma hizo, Mbowe ambaye ametishia kumshitaki Zitto, alisema kuchukua fedha kutoka kwa yeyote akiwamo Rais Jakaya Kikwete au CCM si tatizo bali tatizo ni nia iliyopo kuhusu fedha unazochukua.
 
Sitta hajapona majeraha ya kudodondoshwa uspika sasa unajitengenezea vidonda vya tumbo.

Sitta, naona utu uzee wako unakupeleka pabaya. Lowassa na Rostam ni ngoma nzito huiwezi.

Naona Sitta kishajijuwa kuwa hata uwaziri wa geresha aliopewa sasa hanao tena, ameamuwa kutapatapa.

Nakushauri Sitta, uwache siasa majitaka, kama una lolote kaa chini uzungumze na Lowassa mkubaliane yaishe, haikusaidii kitu kutapatapa vyombo vya habari.
Bimkubwa, kwanza nakuballiana na wewe kwamba mzee 6 hauwezi muziki wa RA na EL, huo ni muziki mnene mno kwake, naomba mwongozo wako, Je tuhuma zilizotolewa na 6 ni za kweli au sio kweli? Bila kujali kama muziki wao anauweza au hauwezi!
 
Mzee wangu Sitta, hata chadema kuna mafisadi, waliopewa hela za ccm. Wewe kuwa mpole achana na siasa tuka kae Sikonge. Si unakumbuka kuna ofisi ya Spika kule, usijali!
 
Bimkubwa, kwanza nakuballiana na wewe kwamba mzee 6 hauwezi muziki wa RA na EL, huo ni muziki mnene mno kwake, naomba mwongozo wako, Je tuhuma zilizotolewa na 6 ni za kweli au sio kweli? Bila kujali kama muziki wao anauweza au hauwezi!

Ngoja tusikie maneno kwenye chama, Mzee Sita kaonyesha njia, waliotuhumiwa ni binadamu, utajili wao ukae kando, Kama kweli ni mafisadi umma utawahukumu, pesa nikitisho, Lakini daima ukweli nikitisho zaidi.
 
Sitta hajapona majeraha ya kudodondoshwa uspika sasa unajitengenezea vidonda vya tumbo.

Sitta, naona utu uzee wako unakupeleka pabaya. Lowassa na Rostam ni ngoma nzito huiwezi.

Naona Sitta kishajijuwa kuwa hata uwaziri wa geresha aliopewa sasa hanao tena, ameamuwa kutapatapa.

Nakushauri Sitta, uwache siasa majitaka, kama una lolote kaa chini uzungumze na Lowassa mkubaliane yaishe, haikusaidii kitu kutapatapa vyombo vya habari.

cheerleaders.jpg

Kumbe huyu mama ni cheerleader wa mafisadi hivi!
 
Bimkubwa, kwanza nakuballiana na wewe kwamba mzee 6 hauwezi muziki wa RA na EL, huo ni muziki mnene mno kwake, naomba mwongozo wako, Je tuhuma zilizotolewa na 6 ni za kweli au sio kweli? Bila kujali kama muziki wao anauweza au hauwezi!

Hakuna cha muziki mnene wala mkubwa hawa ni watu wepesi sana tataizo ni Rais aliyepo maana walimuweka madarakani lakini hawana lolote tungekuwa na Kagame Lowassa na Rostam wangekuwa historia pia ujinga wa watanzania nchi za watu yangepigwa maandamano mpaka wakafunguliwa mashitaka
 
Sitta hajapona majeraha ya kudodondoshwa uspika sasa unajitengenezea vidonda vya tumbo.

Sitta, naona utu uzee wako unakupeleka pabaya. Lowassa na Rostam ni ngoma nzito huiwezi.

Naona Sitta kishajijuwa kuwa hata uwaziri wa geresha aliopewa sasa hanao tena, ameamuwa kutapatapa.

Nakushauri Sitta, uwache siasa majitaka, kama una lolote kaa chini uzungumze na Lowassa mkubaliane yaishe, haikusaidii kitu kutapatapa vyombo vya habari.
Iko wazi kuwa Rostam na Lowasa ni mafisadi wakuu afrika mashariki na kati, sasa kwa wewe kukiri kuwa mafisadi hao ni ngoma nzito hawawezekaniki ndani ya ccm ni dhahiri umekiri kuwa taswira kuu ya ccm itaendele kuwa ni ya kifisadi na kikanjanja kama hao ngoma zito ndo wako in charge.

Otherwise CCM vipande-vipande.
 
sitta kama kweli unachukia ufisadi na mafisadi wenyewe hama CCM maana ccm ni sikio la kufa hata upande pale mlima kilimanjaro na kupiga panda hawatakusikia sana sana wanakuona mwehu
 
Heri yako Sitta umethubutu hongera sana achana na wanafiki CCM na watanzania wengi wao walio wajinga. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hata kama unayepingana naye ana nguvu za kutisha ile kumwabia hutaki au acha ufanyacho inatosha maana kukaa kimya ni kubaya zaidi. Na Mwanafalsafa mmoja alisema "The greatest tragedy of out time today is not the actions of the wicked (Lowassa & Rostam) but the silence of good people (Tanzanians) toward them"
 
Iko wazi kuwa Rostam na Lowasa ni mafisadi wakuu afrika mashariki na kati, sasa kwa wewe kukiri kuwa mafisadi hao ni ngoma nzito hawawezekaniki ndani ya ccm ni dhahiri umekiri kuwa taswira kuu ya ccm itaendele kuwa ni ya kifisadi na kikanjanja kama hao ngoma zito ndo wako in charge.

Otherwise CCM vipande-vipande.

Huo ufisadi wa mdomo tu? weka ushahidi.

Hata wewe ni fisadi kwa kuandika habari za uongo. Rostam ni tajiri namba 1 katika Tanzania wamesema forbes, mlileta siasa majitaka akaachia ngazi, sasa Sitta anataka kugombea Urais ambao hauwezi, ikiwa kashindwa mbinu na kijimwanamke tena kihasibu tu kwenye uspika ataweza ngoma ya Urais? nakuhakikishia hawezi hata aje na treni la majitaka wacha hivi vishtaka uchwara.

Mahakama hazijui hata akashitaki CCM?

Kama si ujinga huo ni nini?

Narudia, Lowassa na Rostam ni ngoma nzito ambayo Sitta haiwezi, hata aseme nini.
 
Back
Top Bottom