Sitta autamani Urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta autamani Urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Superman, Apr 1, 2012.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Please note: Huu si Mkenge wa April's Fools Day. Akili zako changanya na za Mbayuwayu!

  Source 1:
  Sitta atangaza nia kuwania urais ‘akiombwa' | FikraPevu.com

  Source 2:
  Sitta kugombea Urais 2015

  Source 3:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=28475 (Sitta: Ninafaa Urais)

  * ATAKA KUONGOZA MIAKA MITANO AWAACHIE VIJANA

  Na Sheilla Sezzy, Mwanza

  MWANASIASA machachari ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 na kutamba kuwa ana nafasi nzuri kutokana na sifa alizojijengea ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).

  Sitta alitaja sifa hizo kuwa ni pamoja ile ya kuwa mteule wa rais, kwa awamu zote nne za uongozi taifa, tangu Tanzania ilipotaka uhuru wake, Desemba 9 mwaka 1961.

  Spika huyo mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , alisema kwa sasa anawasikiliza wananchi kama wataona anafaa na haoni ubaya wowote wa kushika nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa taifa kwa miaka mitano tu na kuwaachia vijana waendelee.

  "Mimi nawasikiliza wananchi kama wataona nafanana na rais wanayemtaka, basi nitachukua maamuzi kwa wakati huo. Sioni ubaya wowote kama wakiniachia kuongoza nchi hii hata kwa miaka mitano halafu niwaachie vijana waendelee,"alisema Sitta.

  Alisema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2014, kila kitu kitakuwa wazi na haweza kukataa majukumu atayopewa na wananchi wake kwani anatambua wanamuamini kwamba ana uwezo wa kuchapa kazi.

  Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa( NEC) ya CCM, aliyasema hayo jana muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani kufunga kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Kirumba.

  Mwanasiasa huyo ambaye umaarufu wake umepanda kwa kasi katika miaka ya hivi karubuni kutokana na msimamo wake wa kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya CCM, alitamba kuwa amefanya mambo mengi ndani ya Serikali ya CCM, ambayo yamesaidia kuleta mageuzi makubwa nchini.

  Alisema kadri siku zinavyokwenda rais wa Tanzania atajulikana kwa matendo yake na kubainisha kuwa mtu mbaya hawezi kubadilika kuwa mzuri kwa kipindi kifupi.

  "Sioni sababu ya mtu kuutafuta urais wakati wananchi wanaona na wanajadili kila siku ni rais wa aina gani wanayemuhitaji kutokana na mahitaji yao,"alisema

  Alisema anachofanya kipindi hiki ni kutimiza wajibu wake na wananchi ni mashahidi kila nafasi anayopewa, anatimiza wajibu wake ipasavyo na kusisitiza kuwa amefanya mengi yanayoonekana machoni pa watu na kudhihirisha kwamba ni kiongozi bora.

  Akizungumzia umri wa urais, alisema mijadala kuwa vijana hawawezi kuongoza haina msingi. Alifafanua kuwa kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo.

  Alisema rais anachaguliwa na wananchi hivyo maamuzi yote ya nani anafaa kwa nafasi hiyo na umri upi, ipo mikononi mwa wananchi wenyewe.

  Katika hatua nyingine Sitta, aliwashangaa wanasiasa wanaopigana vijembe majukwaani na kueleza kwamba tabia ya kumtukana mtu mmoja mmoja, haina maana yoyote.

  Aliwashauri viongozi wa CCM kutojibu mapigo ya wapinzani na kuwataka kutumia busara kila wanapokutana na kauli chafu kwani nia ya kudumisha amani ya nchi.

  Alionya kuwa amani ya nchi ikitoweka, itakayobebeshwa lawama ni CCM na Serikali yake.

  "Kauli nyingi za majukwaani zinachochea chuki miongoni mwa wananchi, matokeo yake zinaweza kuibua machafuko na waathirika watakuwa wananchi wenyewe, tena wale wasio na uwezo wa kujiokoa,'' alisema Sitta.

  Alisema kuwa katika miaka 50 ya utawala wa CCM, kuna mambo mengi yamefanyika na kwamba wapinzani hawana haja kubeza kwani yanaonekana kwa macho.

  Alisema kuwa katika mafanikio hayo, kuna mengi yamefanywa na Rais Jakaya Kikwete, mfano mzuri ni kampuni tano za madini kulipa kodi na wananchi kuanza kufaidika na rasilimali za nchi yao.

  Hofu ya mahasimu wake

  Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Tamasha Vyombo vya Habari lililofanyika wiki iliyopita kwenye Ukumbi Msasanki Beach, Dar es Salaam, Sitta alieleza kuwa anashangazwa na watu wanaoweweseka wakisikia anataka kuwania urais mwaka 2015.

  "Nashangaa watu wanapata kiwewe kusikia nataka kuwania urais, kuwania urais ni haki ya kila Mtanzania na Watanzania ndiyo watakaoamua nani ni mzuri na atawafaa," alisema Sitta na kushangiliwa na waliohudhuria tamasha hilo.

  "2015 tunataka kuwa na mwelekeo mzuri, nikiwa na maana mambo ya hongo, ubadhirifu hatutaki yawe na nafasi, alisema Sitta na kuongeza:

  Alisema watu wanatumia fedha nyingi kusaka urais na hata wengine kutumia ndumba kwa kwenda Mlingotini, Bagamoyo, kwa nia ya kutaka uongozi na matokeo yake wanaposhinda lengo lao la kwanza linakuwa kurudisha fedha walizotumia.

  Source:
  Sitta kugombea Urais 2015

  MY TAKE:
  Kwa Changamoto za leo ambayo Nchi Yetu inazo, bado Mh. Samuel Sitta hana uwezo wa kuleta mageuzi ya Kimaendeleo katika Tanzania. Alipata mafasi kamili kama Kiongozi wa moja Mhimili kamili wa Kikatiba kama Spika wa Bunge kusimamia kuondoa uovu kikamilifu pamoja na Ufisadi Mwingine lakini akaamua kukumbatia uovu kuinusuru serikali yake ya CCM.

  Japo anaweza kuwa anakubalika na baadhi, Mzee Sitta hawezi kuwa udhubutu wa kutupa Tanzania tunayoiota, na hata huko Wizara ya Afrika ya Mashariki bado hatujaziona cheche zozote.
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwa upande wangu nasema hakuna ccm kama sita,afadhari yeye anaweza kuliko hao wengine,labda tumpe magufuri tatizo tu huwa hatupendi kuambiwa ukweli

  Lakini ccm ya leo sitta ama magufuri ndio wanaweza angarau kutusogeza
   
 3. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hana akili! angekuwa mjanja angepigania kuwepo kwa mgombea binafsi, sasa anafikiri atapitia wapi? Kwa hicho chama chake hawampitishi. Akisumbua sana ataondolewa kwa zengwe lile lile la zamu ya kina mama na Asha Migiro atasimamishwa. Labda arudi CCJ.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  na leo ni siku ya wajinga
   
 5. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Magufuli naye asingekuwepo hapo alipo kama sio nafasi yake kwa jinsi alivyojijenga kwa wananchi. Na ili agombee lazima apitishwe na chama, tatizo "wenye chama walioshika hatamu" hawamtaki. Na mbaya zaidi amejiingiza mno kutangaza chama badala ya wa utendaji wa serikali, hivyo basi amelipunguza kundi la kati lililokuwa likimuunga mkono.
   
 6. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,115
  Likes Received: 1,745
  Trophy Points: 280
  Sitta yuko sahihi kuweka wazi nia yake hiyo,tatizo ni mfumo uliopo ndani ya CCM,uongozi wa mtandao! angalau kidogo ana uthubutu wa kuzungumzia yale mabovu ya ndugu zake!
   
 7. m

  mbwagison Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana ubavu! Akiwa Spika wa bunge hakututendea haki hata kidogo! aliuzima mjadala wa Richmond kidikteta, je alihongwa ahadi ya kugombea Urahisi 2015? huyu mtu ni hatari sana!
   
 8. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  April fools
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Watanzania kama tunataka rais mzalendo basi ni huyu!NA KUWEKA WAZI MAPEMA NI KUJIAMINI KWA UADILIFU,WANAOJIFICHA SIO WAADILIFU NDIO MANA WANAOGOPA KUJITOKEZA MAPEMA,HONGERA MZEE SIX,JAPO SAFARI HII NI ZAMU YA ZANZIBAR SIJUI ITAKUWAJE TUTAJUA MBELE!
   
 10. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Dah!Leo nakuwa mzito sana kukubaliana na habari yeyote ile maana nyingi ni za kusherehekea sikukuu ya wajinga!Kama ni kweli haya basi yetu macho tu!!
   
 11. b

  busar JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  We unadhan nani anafaa? Lowasa?
   
 12. I

  Ilongailunga JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 1,132
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Samuel Sitta ni mtu ambaye ameitumikia serikali ya CCM zaidi ya nusu ya Umri wake wote, na yeye alikuwa mwanamtandao.Inasikitisha sana watu kuhadaiwa eti Sitta anapinga ufisadi, Sitta anatumia neno ufisadi kwa maslahi ya kisisiasa na pia kuwachafua wapinzani wake kisiasa. Si ndo huyu Sitta alipopata nafasi ya kuwa kiongozi wa serikali bungeni povu lilimtoka kuwashambulia na kuwadharilisha wapinzani,na kuitetea serikali na chama kwa kuviita "waadilifu" na wasikivu? mnaomshabia huyu gamba opportunist ni vema muangalie na mtathmini misimamo yenu ya kisisiasa.
   
 13. I

  Ilongailunga JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 1,132
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Samuel Sitta ni mtu ambaye ameitumikia serikali ya CCM zaidi ya nusu ya Umri wake wote, na yeye alikuwa mwanamtandao.Inasikitisha sana watu kuhadaiwa eti Sitta anapinga ufisadi, Sitta anatumia neno ufisadi kwa maslahi ya kisiasa na pia kuwachafua wapinzani wake kisiasa. Si ndo huyu Sitta alipopata nafasi ya kuwa kiongozi wa serikali bungeni povu lilimtoka kuwashambulia na kuwadharilisha wapinzani,na kuitetea serikali na chama kwa kuviita "waadilifu" na wasikivu? mnaomshabia huyu gamba opportunist ni vema muangalie na mtathmini misimamo yenu ya kisiasa.
   
 14. I

  Ilongailunga JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 1,132
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Samuel Sitta ni mtu ambaye ameitumikia serikali ya CCM zaidi ya nusu ya Umri wake wote, na yeye alikuwa mwanamtandao.Inasikitisha sana watu kuhadaiwa eti Sitta anapinga ufisadi, Sitta anatumia neno ufisadi kwa maslahi ya kisiasa na pia kuwachafua wapinzani wake kisiasa. Si ndo huyu Sitta alipopata nafasi ya kuwa kiongozi wa serikali bungeni povu lilimtoka kuwashambulia na kuwadharilisha wapinzani,na kuitetea serikali na chama kwa kuviita "waadilifu" na wasikivu? mnaomshabia huyu gamba opportunist ni vema muangalie na mtathmini misimamo yenu ya kisiasa. Even if it is a fools day We cannot be fooled by cheap politics of Sitta and co.
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hizi thread za tarehe 1/4/2012 bora nichangie za jana
   
 16. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=28475

  Sitta: Ninafaa urais

  Imeandikwa na Grace Chilongola, Mwanza; Tarehe: 31st March 2012

  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ana vigezo vya kuwa Rais wa Tanzania kutokana na kutimiza wajibu wake vizuri kwa miongo minne iliyopita, kwa kuteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali.

  Alisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini hapa, muda mfupi kabla ya kwenda kufunga kampeni za udiwani katika kata ya Kirumba ambapo alisema amefanya mambo mengi katika Serikali ya CCM yaliyoleta mageuzi makubwa.

  Sitta, ambaye kati ya mwaka 1967 na 1969 alikuwa Meneja wa Caltex Oil, na baadaye kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo Katibu wa CCM mikoa ya Iringa na Kilimanjaro, Mbunge, Mkuu wa Mkoa na Waziri, alisema Rais ajaye wa Tanzania atajulikana kwa matendo yake na kusema mtu mbaya hawezi kubadilika kuwa mzuri kwa muda mfupi.

  "Sioni sababu ya mtu kuutafuta urais wakati wananchi wanaona na wanajadili kila siku ni Rais wa aina gani ambaye wanamhitaji kutokana na mahitaji yao," alisema Waziri Sitta ambaye pia alipata kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

  Alisema yuko tayari kwa majukumu ambayo atapewa na wananchi kwa kuwa wanamwamini kuwa na uwezo wa kufanya kazi na kwamba yeye atawasikiliza kama wataona anafaa na kuchukua uamuzi.

  Alisema katika kipindi hiki anachokifanya ni kutekeleza wajibu wake na wananchi wenyewe wanaona kuwa kila nafasi anayopewa anafanya kazi ipasavyo na kudai kuwa vipo vitu vingi ambavyo amefanya na vinaonekana machoni mwa watu ambavyo vinamfanya kuwa kiongozi bora.

  Akizungumzia umri wa urais, alisema mijadala kuwa vijana au wazee hawawezi kuongoza haina msingi wowote na kusema kiongozi mzuri ni mwenye uwezo wa kuongoza wananchi na kuwaletea maendeleo.

  Aliendelea kusema kuwa, Rais anachaguliwa na wananchi kwa hiyo uamuzi wote wa nani awe rais na kwa umri gani yako mikononi mwa wananchi wenyewe. Desemba atafikisha umri wa miaka 70.

  Katika hatua nyingine, Sitta alishangaa viongozi wa siasa ambao wanapigana vijembe katika majukwaa ya mikutano ya hadhara na kusema tabia hiyo si nzuri.

  Alisema kauli za majukwaani zinawatia wananchi hasira.
   
 17. bht

  bht JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  superman mambo? (i come in peace today...lol?)

  Leo mi nimegundua habari nyingi kwenye magazi ni urongo mtupu
   
 18. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  MWANASIASA machachari ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 na kutamba kuwa ana nafasi nzuri kutokana na sifa alizojijengea ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).

  Sitta alitaja sifa hizo kuwa ni pamoja ile ya kuwa mteule wa rais, kwa awamu zote nne za uongozi taifa, tangu Tanzania ilipotaka uhuru wake, Desemba 9 mwaka 1961.

  Spika huyo mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , alisema kwa sasa anawasikiliza wananchi kama wataona anafaa na haoni ubaya wowote wa kushika nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa taifa kwa miaka mitano tu na kuwaachia vijana waendelee.

  “Mimi nawasikiliza wananchi kama wataona nafanana na rais wanayemtaka, basi nitachukua maamuzi kwa wakati huo. Sioni ubaya wowote kama wakiniachia kuongoza nchi hii hata kwa miaka mitano halafu niwaachie vijana waendelee,”alisema Sitta.

  Alisema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2014, kila kitu kitakuwa wazi na haweza kukataa majukumu atayopewa na wananchi wake kwani anatambua wanamuamini kwamba ana uwezo wa kuchapa kazi.

  Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa( NEC) ya CCM, aliyasema hayo jana muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani kufunga kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Kirumba.

  Mwanasiasa huyo ambaye umaarufu wake umepanda kwa kasi katika miaka ya hivi karubuni kutokana na msimamo wake wa kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya CCM, alitamba kuwa amefanya mambo mengi ndani ya Serikali ya CCM, ambayo yamesaidia kuleta mageuzi makubwa nchini.

  Alisema kadri siku zinavyokwenda rais wa Tanzania atajulikana kwa matendo yake na kubainisha kuwa mtu mbaya hawezi kubadilika kuwa mzuri kwa kipindi kifupi.

  “Sioni sababu ya mtu kuutafuta urais wakati wananchi wanaona na wanajadili kila siku ni rais wa aina gani wanayemuhitaji kutokana na mahitaji yao,”alisema

  Alisema anachofanya kipindi hiki ni kutimiza wajibu wake na wananchi ni mashahidi kila nafasi anayopewa, anatimiza wajibu wake ipasavyo na kusisitiza kuwa amefanya mengi yanayoonekana machoni pa watu na kudhihirisha kwamba ni kiongozi bora.

  Akizungumzia umri wa urais, alisema mijadala kuwa vijana hawawezi kuongoza haina msingi. Alifafanua kuwa kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo.

  Alisema rais anachaguliwa na wananchi hivyo maamuzi yote ya nani anafaa kwa nafasi hiyo na umri upi, ipo mikononi mwa wananchi wenyewe.

  Katika hatua nyingine Sitta, aliwashangaa wanasiasa wanaopigana vijembe majukwaani na kueleza kwamba tabia ya kumtukana mtu mmoja mmoja, haina maana yoyote.

  Aliwashauri viongozi wa CCM kutojibu mapigo ya wapinzani na kuwataka kutumia busara kila wanapokutana na kauli chafu kwani nia ya kudumisha amani ya nchi.

  Alionya kuwa amani ya nchi ikitoweka, itakayobebeshwa lawama ni CCM na Serikali yake.

  “Kauli nyingi za majukwaani zinachochea chuki miongoni mwa wananchi, matokeo yake zinaweza kuibua machafuko na waathirika watakuwa wananchi wenyewe, tena wale wasio na uwezo wa kujiokoa,’’ alisema Sitta.

  Alisema kuwa katika miaka 50 ya utawala wa CCM, kuna mambo mengi yamefanyika na kwamba wapinzani hawana haja kubeza kwani yanaonekana kwa macho.

  Alisema kuwa katika mafanikio hayo, kuna mengi yamefanywa na Rais Jakaya Kikwete, mfano mzuri ni kampuni tano za madini kulipa kodi na wananchi kuanza kufaidika na rasilimali za nchi yao.

  Hofu ya mahasimu wake

  Sitta alieleza kuwa anashangazwa na watu wanaoweweseka wakisikia anataka kuwania urais mwaka 2015.

  "Nashangaa watu wanapata kiwewe kusikia nataka kuwania urais, kuwania urais ni haki ya kila Mtanzania na Watanzania ndiyo watakaoamua nani ni mzuri na atawafaa," alisema Sitta

  "2015 tunataka kuwa na mwelekeo mzuri, nikiwa na maana mambo ya hongo, ubadhirifu hatutaki yawe na nafasi, alisema Sitta na kuongeza:

  Alisema watu wanatumia fedha nyingi kusaka urais na hata wengine kutumia ndumba kwa kwenda Mlingotini, Bagamoyo, kwa nia ya kutaka uongozi na matokeo yake wanaposhinda lengo lao la kwanza linakuwa kurudisha fedha walizotumia

  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 19. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Haaaa haaa Mkuu wangu mimi niko poa kabisa ndo kwanza nimetia timu DSM.

  Mkuu mbona mimi nakufahamu miaka sana na wala sina issue na wewe kabisa. Napenda tu unavyosimamia hoja unazoziamini.

  Kama uko Bongo, let us meet in one of the days. Naona AshaDii kule kishawafunga kamba wengi.

  Niaje habari ya Sitta kuweka hadharani nia yake ya kuwa kuishi makazi ya sasa ya Baba Mwana-Asha?
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Mkuu Superman, tafuta thread ya Mzee Mwanakijiji aliyouliza, "Wapiganaji Walioko CCM, Wanapigania Nini?". https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38155-wapiganaji-walioko-ccm-wanapigania-nini-hasa-2.html

  Nilisema hivi kuhusu hawa wanaojiita wapiganaji.

Loading...