Sitta autamani Urais 2015

Sidhani kama Sitta atamshinda Tenga kwenye kinyang'anyiro cha urais wa TFF...

Kama unaongelea urais wa JMT hapo hesabia maumivu kwani hatuna tena mpango wa kuweka wanafiki kwenye nafasi hiyo halafu tujiingize kwenye miaka mitano mingine ya ombwe....
 
Sita hawezi kuwa raisi kwa unafiki na usaliti wa nchi yake, ataishia kwenye uwaziri tuu, walimtoa kwenye uspika kwa hila katulia tuu amebaki kuropoka mambo ya sumu ya mwakwenmbe utadhani yeye ndo msemaji wake mkuu!
 
CCM isifanye makosa kuleta siasa za makundi katika kumpitisha mgombea URAIS mwaka 2015,mtu mwenye uwezo kwa sasa ni Mh.SITTA ambaye ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mpambambanaji mbele ya mafisadi wenye vijisenti.Rai yangu kwake asifikirie kufanya VISASI katika uongozi wake bali asimamie utawala BORA kwa kuwawajibisha mafisadi wote na kujenga misingi bora ya UTAWALA ili kuinua UCHUMI wa NCHI yetu. Mafisadi watubu na kurejesha mali zao kwa hiari yao kabla ya kiama chao,kwa sasa hawana uwezo wakuwadanganya Watanzania ili wachaguliwe hata kama watagawa 100,000/= kwa kila mtu.....tumewagundua janja yao na sasa hawatuwezi tena ...PESA wakitoa tunapokea lakini hawatachaguliwa kamwe !

Mpaka apate chama cha kukiwakilisha.:rockon::rockon::rockon:
 
labda URAHISI , ila sio uraisi wa JMWT , sasa sisi kibabu hicho tukipigie kura cha nini jamani...akagombee uraisi wa mababu wenzie labda watamchagua..
 
Tatizo la Sitta ni kwamba ni wale viongozi wenye syndrome mbili mbaya sana;

1) anaona upinzani ni uadui au mtu yeyote aliye kwenye chama kingine zaidi ya cha kwake hana akili sawa sawa
2) anadhani watu wengine wote ni vichwa maji bali yeye peke yake ndio ana busara na anavyoona yeye ndivyo inavyotakiwa

Sasa raisi wa namna hii ni hatari sana kuwa naye katika nchi.
 
Back
Top Bottom