SITTA AUMBUKA, BAADA YA TAARIFA YA Dr. Mwakyembe

SITTA AUMBUKA, BAADA YA TAARIFA YA Dr. Mwakyembe

Eh mbona wewe ndio umeumbuka,mbona sitta aliyatamka hayo mbele ya mwakyembe?
Umetumwa na desi kayumba?
 
Taarifa ya mwakyembe kutoka kwenye vyombo vya habari ikinukuu taarifa toka hospitali ya appollo
"taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa"
Kwa kiswahili rahisi kabisa ni kwamba bado madaktari hawajagundua chanzo cha tatizo alilonalo mwanyembena wala mwakyembe hajathibitisha kulishwa sumu tofauti na SITTA anavyotaka wananchi waamini kwamba mwakyembe alilishwa sumu, huu ni ushahidi wa siasa za maji taka za mweshimiwa samweli sitta.

Mytake: Tujihadhari na taarifa za uzushi zisizo na uthibitishoi wa kutosha

Jamani hamna aibu yaani ukitumwa basi wee unaandika chochote... Kumbuka wakishamaliza kazi yao watakutupa kama piece of used toilet paper... Dont be cheap... Watakuhesabu kuwa ni mpu....vu.
 
siku zinakaribia,kila kitu kitakuwa wazi,poleni wafuasi wa mamvi
 
Nikweli katba inaruhusu uhuru wa mawazo bu wakati mwingne we should be serious on the matter.Bila kumung'unya maneno utaumbuka wewe coz sidhani kama huu ni utashi wa dhamira yako but unasukumwa na njaa ak.a mchumia tumbo. Punguza kufikri kwa kutumia masaburi.
 
Na mwenye Ushahid wa kulishwa sumu na auweke hapa! Mna hasira sana mlitaka mwakyembe aseme kalishwa sumu?
Soon you will realize that Mweshimiwa aliyekuwa spika wa bunge lililopita alikurupuka! and all those who are behind this false propaganda will fail.
Kwa hiyo anavyoumwa hadi kupelekwa India ni mchezo tuu wakuigiza, hakuna linalomsumbua na shuhuda zake Mheshimiwa hadi makanisani ni porojo tuu!!!! Ndugu yangu mwogope Mungu usilete utani na maisha ya watu, apandacho mtu ndicho atakachovuna, zamu yako inakuja bwana!!!!!!!!

 
[/QUOTE]
Kwa uongo aliouweka kwenye vyombo vya habari< tuleteeni ushahidi wa mwakyembe kupewa sumu!
hiyo habari uliyoisoma ukanukuu baadhi ya sentensi, nadhani inajitosheleza. dr. mwkymbe amelalamikia
kwa nini jeshi la polisi linatoa habari za uongo juu yake... wala hajalalamika kwa nini mheshimiwa six anatoa habari za uongo juu yake..
kkkuona40 wala huhitaji akili ya darasani kuuelewa ujumbe wake. tumia akili ya kawaida tu ambayo hata wanyama kama nyani na ngendele wanatumia.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa “sikunyweshwa sumu” ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini!

Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu;

na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa.

(Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu.

Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:

(i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya “wapelelezi” ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!

(ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo “kuanza kazi”, Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.

(iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari “wale wale” niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!

(iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya “siri” kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa magazetini ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.

Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi?

Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi na bila aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”!

Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung’unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.

Tuendelee kuombeana afya na uhai ili kutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania.

sasa hapo kwenye red.... nani ameumbuka? samweli sita au serikali ya magamba kupitia watumwa (wake jeshi lapolisi) lake?
 
Kakauona kweli nimeamini akili ni nywele na hilo para lako ndo maana waongea upu***
 
Taarifa ya mwakyembe kutoka kwenye vyombo vya habari ikinukuu taarifa toka hospitali ya appollo
"taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa"
Kwa kiswahili rahisi kabisa ni kwamba bado madaktari hawajagundua chanzo cha tatizo alilonalo mwanyembena wala mwakyembe hajathibitisha kulishwa sumu tofauti na SITTA anavyotaka wananchi waamini kwamba mwakyembe alilishwa sumu, huu ni ushahidi wa siasa za maji taka za mweshimiwa samweli sitta.

Mytake: Tujihadhari na taarifa za uzushi zisizo na uthibitishoi wa kutosha

kwa hiyo naye manumba kazusha, au!
 
Taarifa ya mwakyembe kutoka kwenye vyombo vya habari ikinukuu taarifa toka hospitali ya appollo
"taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa"
Kwa kiswahili rahisi kabisa ni kwamba bado madaktari hawajagundua chanzo cha tatizo alilonalo mwanyembena wala mwakyembe hajathibitisha kulishwa sumu tofauti na SITTA anavyotaka wananchi waamini kwamba mwakyembe alilishwa sumu, huu ni ushahidi wa siasa za maji taka za mweshimiwa samweli sitta.

Mytake: Tujihadhari na taarifa za uzushi zisizo na uthibitishoi wa kutosha

ushaambiwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochea hali aliyokuwa nayo. we wadhani ni nini hicho? pili, mkyembe ni best mkubwa wa six kwa hiyo alichoongea six anakijua vzr.
 
Na mwenye Ushahid wa kulishwa sumu na auweke hapa! Mna hasira sana mlitaka mwakyembe aseme kalishwa sumu?
Soon you will realize that Mweshimiwa aliyekuwa spika wa bunge lililopita alikurupuka! and all those who are behind this false propaganda will fail.

mtaumbuka nyinyi na genge lenu
 
Kabla hata Dr Mwakyembe hajaenda India kuna jamaa mmoja hapa JF aliichambua hali iliyomfika Dr Mwakyembe na hali mbali mbali zinazoweza kusababisha hali ile..............ningependa kuamini kuwa yule jamaa wa hapa JF ni Daktari............

Nikiipata ile post nitaibandika hapa............
 
Kwa nini kwenye taarifa ya mwakyembe alaumu polisi kutoa taarifa ya ugonjwa wake ktk media wakati uchunguzi unawendelea? Mbona asilalamike sitta ambavyo amekuwa akitoa ktk media?huwa sitta anatoa taarifa za ugonjwa wa mwakyembe kama nani? dr au mwanafamilia?
Yaani ukiwa na mawazo ya kishirikina kila saa unadhani unalogwa,abdonomalitisi ktk mwili wa binadamu ziko. kitaalamu ni gene mutation ambazo zinaishia kuleta kansa kwa hiyo yawezekana kuna sumu au hakuna sumu.
Sasa mtihani ni kuwa ni kwani sumu iwe kapewa na el na sio jk,ambaye katika ile riport aliyoficha alimsitiri jk na yeye ndio amekuwa na mawasiliano naye ya karibu kama wazir?
Unafiki wa mwakyembe umetunyima mengi wa tz
 
njaa mbaya sana na ukiiendekeza waweza geuzwa kinyume na maumbile!pole kakakuona kwa kuendekeza dhiki!unakera sana unapokuwa dhaifu hivyo!
 
taarifa ya mwakyembe kutoka kwenye vyombo vya habari ikinukuu taarifa toka hospitali ya appollo
"taarifa halisi ya apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa"
kwa kiswahili rahisi kabisa ni kwamba bado madaktari hawajagundua chanzo cha tatizo alilonalo mwanyembena wala mwakyembe hajathibitisha kulishwa sumu tofauti na sitta anavyotaka wananchi waamini kwamba mwakyembe alilishwa sumu, huu ni ushahidi wa siasa za maji taka za mweshimiwa samweli sitta.

Mytake: Tujihadhari na taarifa za uzushi zisizo na uthibitishoi wa kutosha

total cr.ap!
 
mimi pia naungana aliyeleta mada kuwa sitta ataumbuka maana mwakyembe amesema bado uchunguzi unaendelea so polisi na sitta wote wanyamaze hadi mwisho tujue jibu la mwisho ktk uchunguzi wa mwakyembe
 
"..AFRICA...FOR AFRICANS".. mmhh!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom