UGONJWA WA MWAKYEMBE: Sitta amtwisha zigo Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UGONJWA WA MWAKYEMBE: Sitta amtwisha zigo Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lupaso, Feb 2, 2012.

 1. l

  lupaso Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amemtwisha mzigo wa lawama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa kushindwa kuueleza umma ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.

  Sitta alisema kuwa anashangazwa na ukimya huo wa Pinda kwakuwa Dk. Mwakyembe alishatoa idhini kwa serikali kuuzungumzia ugonjwa wake, hasa baada ya madaktari waliokuwa wakimtibu katika Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kuwasilisha ripoti serikalini.

  Waziri Sitta, alitoa kauli hiyo jana mjini hapa, alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima kuhusu ukimya wa serikali juu ya afya ya Dk. Mwakyembe ambaye alidai amelishwa sumu na watu aliowaita ni mahasimu wake kisiasa.

  Alisema kuwa ripoti ya ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ipo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hivyo hakuna sababu yoyote kwa serikali kuificha.
  Akizungumza kwa kujiamini, Sitta alisema hata kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba mwenye haki ya kueleza siri ya ugonjwa wake ni Dk. Mwakyembe si sahihi, kwani suala hilo linahusu jinai, hivyo serikali inawajibu wa kulizungumzia.

  Kauli ya Sitta inakinzana na ile aliyoitoa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hivi karibuni kuwa serikali haiwezi kuzungumzia ugonjwa unaomkabili mtu, bali mhusika ndiye mwenye wajibu wa kueleza umma nini kinamsumbua.

  Sitta, pia amesisitiza kuwa Dk. Mwakyembe amelishwa sumu na anazo sababu nne za kuamini jambo hilo.
  Sitta alisema anashangazwa na kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kumtaka apeleke ushahidi wakati suala la kuchunguza madai hayo liko chini ya polisi wake.

  Waziri huyo alizitaja hoja nne kuthibitisha kwamba naibu waziri huyo amelishwa sumu kuwa ni pamoja na aina ya ugonjwa na mwonekano wa mgonjwa mwenyewe kwamba si wa kawaida.

  "Mimi nina bahati ya kumtembelea nyumbani kwake mara kwa mara. Dk. Mwakyembe anapokaa, mfanyakazi wake kila baada ya muda anakuja kufagia unga unaoanguka kutoka miguuni mwake. Miguu yake imevimba na kuchanika mithili ya tembo. Je, huo ni ugonjwa gani?" alihoji Waziri Sitta.

  Kwa mujibu wa Sitta, sababu ya pili kuthibitisha Mwakyembe kalishwa sumu ni pale madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili waliposhindwa kubaini aina ya ugonjwa na kushauri aende India kwa uchunguzi zaidi.

  Aliitaja sababu ya tatu kuwa ni vitisho alivyokuwa akipata Dk. Mwakyembe kutoka kwa mahasimu wake wa kisiasa kwamba angeuawa kwa ajali ya gari ya kupangwa au sumu na mara zote alitoa taarifa polisi, lakini hazijafanyiwa kazi.

  "Kwanini tusiamini kama kalishwa sumu?" alihoji.
  Waziri Sitta alisema sababu ya nne ni ukimya wa serikali katika kuzungumzia suala hilo.
  Alisema taarifa ya ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kutoka kwa madaktari wa Hospitali ya Apollo nchini India iko Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na akashangaa kwa nini inaona ugumu wa kuitangaza wakati mwenyewe ameridhia.

  Sitta alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa uchunguzi aliofanyiwa Dk. Mwakyembe nchini India kwa kuchukua kucha, ngozi na uboho, umeonyesha kwamba Dk. Mwakyembe alilishwa sumu.

  Waziri huyo alisema Dk. Mwakyembe anatarajiwa kwenda tena India Februari 19 mwaka huu na atakaporejea nchini ameahidi kupasua jipu juu ya ugonjwa wake.

  Sitta alililaumu Jeshi la Polisi kupuuza madai ya vitisho vya kuuawa kwa baadhi ya viongozi, akiwamo yeye pamoja na watu binafsi.
  Akitolea mfano, alisema aliwahi kupeleka taarifa za kutishiwa kuuawa mjini Dodoma wakati huo akiwa Spika wa Bunge, lakini Jeshi la Polisi mkoani humo hadi leo halijazifanyia kazi taarifa hizo wala kumpa majibu ya kuridhisha.

  Alisema kuwa mbunge mmoja aliwahi kunasa mazungumzo ya watu fulani hapa Dodoma wakipanga kuligonga gari lake (Sitta), na kwamba alipeleka taarifa hizo polisi lakini hawakuzifanyia kazi.

  Kwa muda mrefu Dk. Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao hadi sasa haujaelezewa hadharani huku taarifa zisizo rasmi zikidai amelishwa sumu.

  Ugonjwa huo umemfanya anyonyoke nyusi, ndevu na vinyweleo, huku ngozi yake ikielezwa kutoa unga na miguu yake kupasuka mithili ya mtu mwenye magaga. Hali hiyo inadaiwa kumbadilisha kabisa muonekano wake wa asili.


  Hivi hilo neno nililopigia mstari hapo juu ndilo maana yake ile ninayohisi au kuna maana nyingine kama ndio ninayoifahamu mimi naona jamaa hana staha
  kama kuna maana nyingine nisahihisheni na hisia zangu potofu nilisikia siku nyingi hili neno labda kiswahili kimenyumbulika sana
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh hatari kubwa katika hili niko upande wa Mheshimiwa Sitta.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..mara ya kwanza kusikia mambo ya kulishwa sumu ilikuwa ni miaka ya 90 wakati wa kifo cha kutatanisha cha Dr.Fupi, aliyekuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

  ..ushauri wangu ni kwamba Dr.Mwakyembe ajitokeze hadharani kwenye mkutano wa vyombo vyote vya habari, viongozi wa madhehebu yote ya dini, na taasisi za haki za binadamu nchini, atuambie Watanzania on the camera kile kinachomsibu pamoja na kuiweka wazi ripoti ya madaktari.
   
 4. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,655
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Yeyote anayedai kuwa 6 ni mwongo. Alete ukweli hapa vinginevyo atakuwa mpuuzi
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,446
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  Hao waliompa sumu wanatulisha hasara,maana isingekuwa wao Dr asingeenda India kutumia mamilioni ya walipa kodi
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hivi hiyo report inapewa serikali au mgonjwa mwenyewe? Naona kama 6 ama Mwakyembe hawana hiyo report kwa kuwa 6 anatoa sababu nne amabazo kwazo anafikiri Mwakyembe alipewa sumu. Kama wana report nafhani angesema report inaonyesha kwamba Mwakyembe amepewa sumu badala ya kutoa sababu anazofikiri kuwa ndio ushahidi wa kulishwa sumu. Mwakyembe apewe hiyo report aomwage hapa tuone ukweli wake.

  Mkuu mtoa uzi Uboho ni bone marrow.
   
 7. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mwakyembe ni mtu wa ajabu asiyestahili kuonewa huruma hata kidogo!! Anapaswa kulaumiwa kwa unafiki wake! Hilo ni pigo la pili wanamkosakosa! Alipopata pigo la kwanza la ajali, alisema kwamba anamwachia Mungu!! Safari hii amepata pigo la pili; wamemchua kwa mafuta ya kinyonga! Yote anamwachia Mungu! Anakaa kimya ili kukinusuru chama chake kinachotaka kumtoa roho!

  Huyu mtu asiyejihurumia mwenyewe, si wa kuonea huruma hata kidogo!! Ni mnafiki wa kutupwa!! Anatusumbua akili bure!! Hadi rafiki yake wa karibu, Waziri Sita ametamka wazi kuwa kalishwa sumu. Yeye anakaa kimya ili kulinda heshima ya chama!! Kwa mtindo huo wa kinafiki, asubiri tu pigo la tatu. Hapo ndipo atakapomwachia Mungu yote kikwelikweli!! Jamani tumuache huyu mtu ajifie kwa amani kama anavyotamani, ili alinde heshima ya chama chake!!
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Huwa simfagilii Pinda lakini katika hii issue ni kumuonea maana mgonjwa yupo,Mwakyembe atwambie anaugua ugonjwa gani? Waache siasa zao za majitaka na unafiki!
   
 9. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Jamani maneno makali yaliyokolezwa na rangi nyekundu hayana hata chembe ya huruma! kwani kimya cha muhusika kakwambia ni kwa kukilinda chama chake?
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena kweli. Hivi ni kweli kwamba mgonjwa hana report ya daktari? Nijuavyo suala la ugonjwa huwa ni la daktari na mgonjwa, third party anahusishwa kama naye anahusika na ugonjwa. Mfano ukiwa na STD inabidi umpeleke partner wako naye apate dozi lakini kama una malaria ni wewe na daktari. Kwa mantiki hiyo serikali inakujaje hapo?
   
 11. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kila siku Mwakyembe, Sita, kwa nini Mwakyembe asiweke ripoti kamili hadharani tujue pumba na mchele sio kila siku wanaumiza akili za watu, au nao wanauza sura
   
 12. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Single yao ya richmond ishachuja sasa wanatafuta Remix ya kutoka nayo,huyo sitta analalamika polis haijafanyia kazi madai yake ya kuuawa je hafikirii polis kuna kaz wamefanya ndo mana hajauwawa au alitaka bodgurd auze nae sura mtaani!
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Wakati naanza kuisoma habari hii nilitaka kuanza kuiamini lakini baada ya kuendelea kuisoma zaidi najihis kuachwa njia panda na kujiuliza uhalali wa ukweli unaosemwa na Sitta!!

  Twende taratibu, Mheshimiwa Sitta anasema kwamba ripoti ya madaktari wa Hospitali ya Apollo inaonesha kwamba Dr. Mwakyembe alilishwa sumu!! Bila shaka hiyo ni ripoti ya kisayansi na sio ya kidhahania. So, kama ripoti inasema Dr. Mwakyembe amelishwa sumu, kuna haja gani tena ya Mh. Sitta kui-highlight mambo yanayothibitisha kwamba Dr. alilishwa sumu?! Hivi ripoti ya kitabibu /kisayansi ikishasema kwamba NasDaz ni mwanaume, kuna haja ya mtu mwingine ku-highlight vijisababu vya kuthibitisha uanaume wangu?! Kwa jinsi ilivyo, mtu mwingine anaweza ku-highlight hizo sababu endapo tu itaonekana nafanya matendo yasiyolingana na uanaume ulioelezwa na utafiti wa kisayansi! Tumchukulie Mwanariadha mdada yule wa South Africa ambae kama sikosei anaitwa Amenya (nisahihisheni). Ilitakiwa ipatikane ripoti ya kitabibu kuthibitisha jinsia yake kwa matendo yake yanatilia shaka jinsia yake!! Ripoti ya kisayansi ndio mwisho, lakini ukina mtu bado anakazia yake ndani ya hiyo ripoti maana yake ni kwamba ana mashaka na uhalali wa hiyo ripoti!

  Mheshimiwa Sitta ame-highlight mambo ambayo ana-conclude; kwa kuzingatia vigezo hivyo; "ni kwanini basi tusiamini kwamba Dr. Mwakyembe alilishwa sumu!!!" Haya ni mapungufu makubwa kwavile suala lililokuwa certified kisayansi hakuna cha kuamini hapo. Mambo ambayo mtu anatakiwa kuamini ni yale ambayo hayana uthibitisho wa kisayansi na badala yake itabidi kutumia nadharia na dhahania...kama vile kuamini uwapo wa mungu!!! Huwezi kumsimamisha (say) Dr. Slaa mbele halafu liwepo suala la kuamini au kutoamini kama ni mwanaume unless kama matendo yake yanatia shaka na uanaume wake!!

  Hivyo basi, ikiwa Mh. Sitta bado analeta sababu nne za kutghibitisha kwamba Dr. Mwakyembe alilishwa sumu wakati vile vile anatuambia ripoti ya kitabibu imesema alilishwa sumu; basi ni ama:
  1. Ripoti ya kitabibu haisemi hivyo (haisemi kwamba amelishwa sumu) na ndio maana anataka kuwajenga watu kisaikolojia ili ripoti hiyo itakapotolewa hadharani na kuonesha hakulishwa sumu; watu wageukie highlights alizozitoa kwamba alilishwa sumu na kutaka tuamini kwamba ripoti imechakachuliwa!!!

  2. Kama kweli ripoti inasema Dokta alilishwa sumu, basi inaelekea Sitta ana mashaka na sumu iliyosemwa na ripoti hiyo....mathalani unaweza ukakuta ni sumu iliyokuwa imejengeka mwilini labda kutokana na matumizi ya kitu fulani; iwe chakula, madawa au kinywaji fulani. Sasa kwavile anahisi ripoti inayoelezea sumu ya aina hiyo haiwezi kuleta taste mzuri masikioni mwa watu, ndio maana anaamua kutujenga kisaikolojia kutokana na maelezo niliyoyatoa kwenye namba 1 hapo juu.

  Kama kweli ripoti imesema amelishwa sumu, haina haja ya highlights za kufikirika unless kama anataka kucheza michezo ya kisiasa!

   
 14. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mh. Mwakyembe, weka mambo hadharani ukweli uwe wazi
   
 15. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitta Urais 2015 unamchanganya!!!!!!!!! Huyo Mwakyembe hana mdomo kwa nini kumsemea kama mtoto mdogo?
   
 16. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  UBOHO = BONE MARROW
  Kwa mtazamo wangu, ni kwamba ripoti ya mgonjwa huwa anapewa ndugu wa mgonjwa anayetambulika na hospitali, hasa pale ugonjwa huo unapokuwa complicated. Shabaha ni kuwa Ukimpa mgonjwa mwenyewe unaweza kumtisha na hata kumkatisha tamaa. Na pia ili ndugu huyo ajue ni jinsi gani ya amuhudumie mgonjwa wake. Na kama ni ugonjwa ambao utapelekea kifo cha mgonjwa, ni ili ndugu aamue mwenyewe kama aendelee kutumia gharama kubwa kwa mgonjwa ambaye hata hivyo hatapona au aamue kumrudisha nyumbani kupunguza gharama na kumhudumia kwa dawa baridi za kumpunguzia maumivu huku akisubiri siku ya Bwana pasi na mgonjwa mwenyewe kujua.
  Katika issue hii ya Mwakyembe, ndugu yake anayetambulika na hospitali, ni yule anayemhudumia na kumgharamia gharama zake zote za matibabu pale hospitalini, ambaye niserikali. Tofauti na Chami ambaye alikwenda mwenyewe India na kujitibu kwa gharama zake mwenyewe bila kuhusisha serikali. Ndio maana ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe wamepewa Serikali na si ndugu zake. Huenda ni kweli hata yeye hajui ni nini kilichomo kwenye ripoti, kwa sababu zile zile nilizotangulia kuzieleza hapo juu.
   
 17. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi nadhani kwa jinsi Mwakyembe anavyochelewa kusema ukweli wa kinachomsibu ndivyo atakapofunguka baadhi yetu nikiwemo mimi nitaona ni muongo tu.
   
 18. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini kubwa jinga Sitta anataka Serikali imsemee Mwakyembe? hata kama Mwakyembe anataka serikali ichukue hatua ni lazima awepo mlalamikaji. Je, taarifa ya mwakyembe ilikwenda kama ripoti ya daktari au ambatanisho la kulishwa sumu?
   
 19. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si kweli kwamba wakati wote binadamu akikutwa na sumu mwilini basi awe amelishwa wakati mwingine sumu tunakutana nazo kwenye vyakula, wangapi hawajawahi kusikia watu wamekufa baada ya kula mihogo yenye sumu au kasa mwenye sumu. Kinachohitaji hapa ni aina gani ya sumu na kama inaweza kupatikana kwenye chakula, vimiminika au nje ya chakula na vimiminika. Madaktari watakuwa wameweka maoni yao.
   
 20. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati ufike Sitta naye afyate mdomo ili airuhusu na Familia ya Mwakyembe kuzungumza sasa yeye ni nani au ndo kaacha nafasi yake ya Uwaziri akaamua kuwa msemaji mkuu wa Familia ya Harrison??? Yani kila kukicha Mwakyembe kalishwa sumu mambo ayafanyayo na umri wake ni tofauti kabisa hilo jasho linalomchuruzika naye pia kalishwa sumu ama?? Hii Sheria alosoma 6 ni ubatili mtupu

  Eti Harrison anaenda India tena na akirudi atapasua jipu jamani tumekuwa tukimsubiri Harrison manake alishatuahidi Watz kuwa tumwombee arudi salama nyumbani na akirudi atasema yote haya sasa amerudi bado ngonjera zinaendelea na anaenda India tena na kutuachia kauli ile ile ya nikirudi......... Halafu hao jamaa ni wanasheria wanafahamu fika principle of confidentiality kwamba hapo ni kati ya Madaktari na Mwakyembe sasa Serikali inatoka wapi tena??

  Kwa hiyo naye anatudanganya na vibakia.

  Hawa wazee watuache bana sasa Watz! Yani 6 kweli kazi unayo mzee.
   
Loading...