nashy
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 679
- 141
Umetumwa na nani wewe
tatizo lake amechukua habari kama ilivyoandikwa Jambo leo na kuileta kama ilivyo
Umetumwa na nani wewe
Taarifa ya mwakyembe kutoka kwenye vyombo vya habari ikinukuu taarifa toka hospitali ya appollo
"taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa"
Kwa kiswahili rahisi kabisa ni kwamba bado madaktari hawajagundua chanzo cha tatizo alilonalo mwanyembena wala mwakyembe hajathibitisha kulishwa sumu tofauti na SITTA anavyotaka wananchi waamini kwamba mwakyembe alilishwa sumu, huu ni ushahidi wa siasa za maji taka za mweshimiwa samweli sitta.
Mytake: Tujihadhari na taarifa za uzushi zisizo na uthibitishoi wa kutosha
Kwa nini kwenye taarifa ya mwakyembe alaumu polisi kutoa taarifa ya ugonjwa wake ktk media wakati uchunguzi unawendelea? Mbona asilalamike sitta ambavyo amekuwa akitoa ktk media?huwa sitta anatoa taarifa za ugonjwa wa mwakyembe kama nani? dr au mwanafamilia?
Yaani ukiwa na mawazo ya kishirikina kila saa unadhani unalogwa,abdonomalitisi ktk mwili wa binadamu ziko. kitaalamu ni gene mutation ambazo zinaishia kuleta kansa kwa hiyo yawezekana kuna sumu au hakuna sumu.
Sasa mtihani ni kuwa ni kwani sumu iwe kapewa na el na sio jk,ambaye katika ile riport aliyoficha alimsitiri jk na yeye ndio amekuwa na mawasiliano naye ya karibu kama wazir?
Unafiki wa mwakyembe umetunyima mengi wa tz
kuna watu makauzu Tz,mtu yupo tayari kuharibu utu wake hata familia yake kwa mlo wa masaa machache tu
yawezeka kapewa sumu tusubirie majibu ya mwisho ya india, halafu pia mwakyembe amuombe sitta naye afute subira maanake sitta asingeropoka mapema polisi wasingekurupuka kujibu
Kaumbuka kivipi sasa?
Mkuu wangu hii ni vita ya makundi hasimu ndani ya CCM. Kuna kundi kwasababu ya uoga hata mtu akiugua malaria kwa kuumwa na mbu basi anakimbilia kusema ugonjwa umesababishwa na hasimu/mahasimu wake kisiasa. Mimi naamini tamko la juzi la serikali kupitia DCI,Robert Manumba ndiyo msimamo rasmi wa serikali.