Foundation
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 1,420
- 613
Duh !! Kweli Arusha wameamua..
Mathayo 18:18
Amin,nawaambieni,yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Lile zimwi la kutokukubalika kwa diwani wa kata ya Olorien kama Meya wa jiji la Arusha limeendelea kumwandama Diwani huyo leo baada ya kupata mapokezi hafifu kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt. Teresia jijini Arusha inayoongozwa na Mh. Samwel Sitta. Tofauti na wageni wengine waliokuwa wakishangiliwa kwa vigelegele na makofi wakati wa utambulisho, Mh. Gaudence Lyimo hakupata mapokezi hayo kutoka kwa waumini hao kama wenzake. Waumini walionyesha kupoa hadi alipotangazwa mgeni mwingine ndipo hali iliporudi kama awali.
Mbunge wa Arusha ameendelea kutomtambua "Meya" huyo kwa kumtambulisha kama diwani huku akimwomba Mh. Sitta kuongea na wakubwa wake ili wakamilishe haraka kuumaliza mgogoro uliopo kupitia kamati iliyoundwa na Pinda na Mbowe.
Ninachojiuliza ni kwamba, ni lini atapata hekima ya kujiuzulu hiyo nafasi ili apate tena heshima kwa jamii ya Arusha. Licha ya kampuni yake ya ujenzi kufanya miradi mingi ya kanisa hilo kabla ya mgogoro huo, waumini hao hawamdhamini tena kama awali. Poor him!

"haki tutaitafuta by the ballot or the bullet" Lema (via Martin jr wa Jf)... Hii kauli haijakaa vyema, inaweza kuwapa CCM credit kwa dhana kwamba CHADEMA ni chama cha fujo, watch out guys..!
Mbele ya Askofu mkuu Josephat Leburu, Mbunge wa Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta .Mbunge Lema ashikana mikono na mkuu wa mkoa wa Arusha na Meya wa Arusha. Lema akihaidi hadharani hana chuki na mtu yeyote binafsi ila hata choka kupigania haki kama haki haita tendeka katika jamii. Amemwomba Mbunge huyo wa Afrika Mashariki kumaliza mgogoro huo mapema. Wadau toeni mchango wenu katika hili.
wamekufadhili wewe pia kumbuka shule zao, hospitali zao na wakufunzi kibao waliojaa nchi nzima wamesoma shule zao na hata waalim waliokufundisha chuoni kama uliwahi kukanyaga walifadhiliwa na wao kwahiyo kwa namna moja ama nyingine wamefadhili asimilia kubwa ya watanzania kama siyo kaka basi dada na kama siyo shangazi basi mjomba. kiumbe uliyekosa fadhila we, leo unajaribu kulipakazia kanisa baada ya miaka chungu mzima ya huduma zao kwa jamii.Hilo si jipya kwani CHADEMA wanawaogopa wafadhili wao 'kanisa' hivyo ni lazima wawasikilize.
CCM shule ipo, nao hawkuona jingine ispokuwa kutumia udhaifu huo. Mwalimu sijui alikiachia nini chama hiki, pengine kale kafimbo hakakuzikwa naye bali kapo ikulu kakifanya vitu vyake.
Sasa mchezo umekwisha!
Mh S.Sitta akiwa ktk harambee Mjini Arusha.Ameombwa na kutafuta amani ktk mji wa Arusha kwa kuwapatanisha Mbunge Mh Lema na Meya wa Mji wa Arusha,na akachukuwa jukumu hilo kama ambavyo picha inavyojieleza.
Nawasilisha
Kichwa cha uzi kinasomeka 'kanisa lawapatanisha...' lakini habari yenyewe inasema hawajapatana bado, bali walikwenda kushikana mikono tu. Kiukweli wanasiasa wetu watz hawaaminiki. Kazi yao ni kukaribishana juisi, kushikana mikono na kuuza sura kwa kuchekacheka tu. Hakuna cha maana hapo, ni kupotezeana muda tu. Mb. Umeitwa na askofu wako upatanishwe na RC na Meya, badala yake unamwomba mb. mwenzio aumalize 'mgogoro' mapema, ww umeshindwa nn! Siasa zingine ni uchwara kweli.Mbele ya Askofu mkuu Josephat Leburu, Mbunge wa Afrika mashariki Mh. Samweli Sitta .Mbunge Lema ashikana mikono na mkuu wa mkoa wa Arusha na Meya wa Arusha. Lema akihaidi hadharani hana chuki na mtu yeyote binafsi ila hata choka kupigania haki kama haki haita tendeka katika jamii. Amemwomba Mbunge huyo wa Afrika Mashariki kumaliza mgogoro huo mapema. Wadau toeni mchango wenu katika hili.
By Sangarara
Anakunywa Maji kidogo, kisha anaendelea
Pale Kenya pale, wakati wa mchakato wao damu imemwagika pale, sasa mimi siko tayari kuona hili linatokea hapa,na ndio maana hata kwenye swala la madiwani wa arusha, mimi niliwaelekeza Waziri Mkuu na Katibu wangu Mkama kuhakikisha Mnakaa, mnazungumza na kulimaliza hili, lakini kinachoendelea pale mi hata sikielewi nikiuliza naambiwa tatizo ni Lema, vyombo vya habari kwanza vilikuwa vinasema tatizo ni Chitanda, sasa Chitanda simsikii tena naambiwa tatizo ni Kamanda wa Polisi Zuberi na Mkuu wa Mkoa, mimi sielewi kabisa nini kinaendelea Pale, na hali hii inachafua kabisa picha ya nchi yetu uko nje.