Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Enaseketeshaaaaaaaa, hii ni nondo tupuuuuuuuu,

Unatoka dar unaenda kusaka maisha lindi
Wakati watu wanatoka Lindi kuja Dar, ni uzezeta wa Kiwango cha juu sana, ni mkurupukaji asiyefikiria ndio maana ata story kazira kwa jambo dogo tu

Dar umeshidwa hata kwenda kutembeza maji na soda kule Kariakoo, unaondoka na buku 5 kwa siku, au ukaenda kumenya viazi bar huko wakakupa msosi huku ukitafuta kazi nyingine za maana
 
Tarehe 4 mwezi wa pili 2020 nikiwa katika msongo wa mzito wa mawazo yaliyotokana na ugumu wa maisha nilijikuta nafanya maamuzi magumu bila kutarajia. Nilikuwa nakaa gheto maeneo ya buguruni sheli japo gheto lilikuwa na mshikaji wangu ambae tulisoma nae primary mawenzi shule ya msingi iliyopo moshi mjini mwaka 2006 ndotulimaliza darasa la saba hapo.

Nikiwa nimelala saa sita usiku naona napigwa mgongoni kwa nguvu kuamka namuona rafiki angu tunaelala chumba kimoja pia ndommiliki wa gheto mm kaniweka tu kishkaji, nikasema kulikoni jamaa akajibu kiunyenyekevu akisema "oya demu wangu kafukuzwa na Dada ake alipokuwa anakaa kwahiyo hana pakwenda nasaizi ni saa saba usiku amekuja yupo hapo kibarazani anataka tulale humu kwahiyo please wewe ni mwanaume ebu tafuta ustaraabu wa kuondoka saizi ukija asubuhi tutaweka mambo Sawa ".

Nikamwambia sasa mda huu mm niende wapi ndugu na Sina hata sehemu yakujiegesha!? Akajibu nitajua mwenyewe, ikabidi nivae niende kimboka night club kupoteza mda nikawa naangalia movie kwenye mabanda ya pale kimboka maana majamaa huwa hawalali. Ilipofika asubuhi nikatia timu bahati nzuri nikakuta wote wameamka ila wapo kitandani nikamsalimia shemeji pamoja na jamaa angu japo hawakuonesha uso wa tabasamu walikuwa serious kiasi ambacho nilishindwa kuwaongelesha.

Nilipotazama juu kwenye enga zakuwekea nguo zangu ghafla sikuona nguo yoyote, nilipouliza jamaa akasema nimekuwekea kwenye begi ili ukija usisumbuke kuzipanga maana shemeji ako kasema yeye hatoki atakaa hapahapa sasa hatuwezi kulala watatu. Ilikuwa ni kipindi kigumu sana Kwangu zaidi ya Alpha konde alipotolewa madarakani. Nikatazama juu chini nikawaza nikasema haina shida.

Nikabeba begi langu nikawaaga wakasema kila raheli. Nilikuwa na simu Aina ya tecno F1 na mfukoni nikawa na 20000 nikasema Poteleapote nitaenda popote pale kutafuta rudhiki.

Kwa pesa niliyokuwa nayo kukaa Dar Es Salaam hapakunifaa tena, hiki ndokipindi ambacho mikoani unapaona nafuu kuliko jiji la Dar Es Salaam. Nikiwa na begi langu Zito la nguo mpaka mida ya saa kumi jioni nilikuwa sijajua niende wapi na nitalala wapi. Nilipoona mda unakwenda ilibidi nimfate jamaa mmoja ivi yeye anauza nguo za jinsi buguruni sokoni kama unaenda shell nilipofika alinichangamkia akijua ni mteja kumbe ni mtu mwenye dhiki aliehitaji msaada. Sikupoteza mda ilibidi nimwambie ukweli yote yaliyotokea ila msaada wangu mkubwa ilikuwa anitafutie mteja wa kununua simu yangu.

Akasema nauzaje nikamwambia simu nauza 90000 tu jamaa akasema ngumu kupata mteja leoleo Sema ngoja nimpigie simu Dada mmoja anauza chakula Ana shida sana na simu kubwa. Yule dada akaja alivyoiona na alivyokuwa na pupa ya kumiliki smart phone nikajua tu huyu ni mteja. Jamaa akasema niongee nae ilibidi nimwambie nauza laki moja maana ngozi nyeusi ukitaja bei harisi ushahalibu. Yule Dada akasema ana 80000 nikajifanya nakataa akaongeza 5000 nikamwambia toa pesa akanipa nikampa simu akaagana na jamaa akaondoka. Sasa kimbembe kikaanza Kati ya mm na huyu Dalali.

Jamaa nikampa 5000 akasema niache utani inabidi nimpe 20000 nikacheka kidogo huku mdomo ukiwa umekauka maana mpaka jua lilizama sijapata chochote cha kuchezesha kinywa changu.

Nikamwambia 20000 hapana kutokana na shida niliyonayo jamaa akasema vinginevyo anamwambia yule dada hii simu ya uwizi arudishe. Nikaona isiwe tabu nikampa 10000 nikasema hutaki naondoka na pesa sirudishi maana ilibidi nikunje sura vinginevyo nitakwama. Jamaa akapokea.

Alipopokea Ile pesa nikapotea mda huohuo. Sasa kimbembe nipakulala maana ikawa ni usiku huku nikiwa nimechoka sana. Nikaingia bar moja ivi inaitwa sewa. Nikaongea na muhudumu akasema Vyumba kwanzia saa saba usiku mdaa huu ni short time. Kwa kuwa nilikuwa na shida nikavumilia Ilipofika saa saba nikawa hoi kweli kweli nikiwa nimekaa kwenye kiti huku bar ikiwa imefungwa yule muhudumu akaja akasema kaka pole nenda kalale chumba hicho apo. Akasema nimpe 4000 tu maana naonekana sipo sawa. Nikampa pesa yake Nikaingia kulala japo madadapoa walikuwa wanagonga sana mlango niwafungulie lakini sikujali.

Asubuhi kukapambazuka nikasema leo inyeshe mvua liwake jua sikai Dar. Mm nimemaliza kidato cha sita ila sikubahatika kuingia chuo kikuu lakini najua sana kufundisha. Nikasema hapa ngoja nikatafute kibarua cha kufundisha mikoani ila tu isiwe dodoma. Nikawaza sana nikasema hapa safari ni kwenda lindi. Nikachukua daladala mpaka mbagala, ilikuwa saa sita mchana, kufika pale wakasema mda huu Gari za lindi mpaka temeke hapa mbagala ipo gari ya kwenda kilwa mda huu inaitwa MASHALAH.

Kwasababu kichwa changu mda huo hakikuwa sawa nikasema nikate tiketi tu hata ya kwenda kilwa nitajua mbele ya safari. Wakasema nauli Dar mpaka kivinje ni 11000 halafu Dar mpaka kilwa ni 13000.
Saa sita na nusu tukawa tumeondoka Dar Es Salaam kuelekea kilwa nikiwa Sina ndugu wala yoyote anaenijua lakini nikiwa na Amani ya moyo kwakuwa kilwa sio sudani wala Uganda ni Tanzania pia.

Inaendelea...

Safari ya kuelekea Kilwa ikaanza. Nililipa nauli ya Dar Es Salaam to Kilwa shilling 13000 mfukoni mpaka na panda bus nikawa nimebakiwa na 70000 tu kutokana na pesa nyingine Jana usiku Nililipa gest 4000 asubuhi kabla ya kwenda kukata ticket nilienda saloon kunyoa kwa 2000 baadhi ya pesa nilikula mihogo na maji ya kunywa njiani. Ubovu nikuwa kwenye siti nilikuwa nimekaa na mtoto mdogo wa kike ambae alipakiwa na mzazi wake ila yeye huyo mzazi hakuwa anasafiri sasa akaniambia kuwa nimsaidie kumwangalia lakini pia konda alikuwa amepewa taarifa kimsingi ni mtoto ambae huenda ni miaka 11 au 12 huyu dogo yeye alikuwa anashukia somanga. Kwahiyo nikakosa hata msaada wa kuanzia nikifika kilwa itakuwaje maana nilikuwa nategemea labda mtu nitakae kaa nae atanipa mawazo namna ya mji ulivyo na jinsi ya kuhendo swala langu. Tukiwa safarini ilibidi nimuulize huyu dogo endapo anaijua kilwa ili tu nipate pakuanzia dogo akasema yeye hajawahi fika anaishiaga tu somanga maana ndo kwao. Nikapiga moyo konde nikajisemea moyoni kuwa liwalo na liwe itajulikana.

Tukiwa safarini niliona kibao kimeandikwa IKWIRIRI gari likasimama kwa dakika chache nikajiuliza kulikoni tena kumbe Kuna wa mama walisimamisha wakapanda lakini cha ajabu walikuwa wananuka shombo ya samaki na mabeseni yao. Kuna mmoja alikuja kusimama karibu yangu nikamuuliza kama Ana samaki akasema Sina mwanangu samaki zimeisha. Nikakausha huku mawazo ya kwenda nisipopajua yanakuja nakunikosesha raha kabisa. Mungu yumwema baada ya dakika chache nilipata usingizi mzito sana hii nikutokana na siku ya jana kutokupata usingizi wa kutosha namm kulala Kwangu nikupumzisha mawazo. Nilikuja kushtuka kutokana na makerere mengi yawafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanaouza biskuti, korosho, mahindi ya kuchoma na kadharika, kuangalia pembeni dogo simuoni niliyeambiwa nimwangalie nikasema kulikoni tena nikaamka chapu kwenye siti nikaenda kumuuliza konda dogo niliekaa nae yuko wapi??. Konda akasema nina mambo mengi kaka huyo dogo ni yupi? Nikamwambia nilikuwa nimekaa nae siti moja mm nikalala lakini cha ajabu simuoni konda akasema keshashuka. Nikamuuliza kwani somanga tumepita maana mm ni mgeni konda akasema nipande kwenye bus hapo tulipo ndosomanga yenyewe na dogo kashapokelewa na wazazi wake tayari.

Nikapanda kwenye gari. Bus likaiacha somanga na safari ya kwenda kilwa ikawa imewaka moto, niliona bus limejaza wa mama ambao walikuwa wanauza samaki kwenye bus. Kwa kuwa nilikuwa na njaa sana nikasema hapa samaki ni bei sana nilifanya mistake kutokununua muhindi wa jero somanga anyway nitauliza kama ana samaki hata wa buku mbili hata kambale nitatafuna usabato nauweka pembeni.

Nikiwa nasubiri afike Kwangu yule mama muuza samaki nikawaza wale wa mama wa mwanzo waliopandia IKWIRIRI kwani ni tofauti na hawa? Mbona siwaoni? Pembeni Kuna mzee mmoja alipandia somanga kwahiyo tukawa siti moja nikamuuliza akasema wale kwao ni somanga IKWIRIRI huwa wanaenda kuuza samaki wakiisha wanarudi somanga, nikasema hapo Sawa
Mama muuza samaki akawa amefika Kwangu nikamwambia sogeza beseni nichague mwenyewe mama akasogeza beseni la samaki nijichagulie.

Kucheki kwenye beseni niliona samaki wakubwa tupu Aina ya kibua na Changu. Nikajisemea moyoni hapa nimetoka patupu hawa samaki bei yake siiwezi lakini acha tu nimuulize ni bei gani akitaja nimrushe aendelee kuwauzia wengine. Yule Dada akasema samaki ni buku buku. Nikasema ebu rudia tena? Akasema kaka bei haipungui samaki mmoja ni elfu moja. Jamani sikuweza kuamini samaki mkubwa ambae Dar Es Salaam ni 7000 somanga anauzwa buku. Nikasema hapa ndo penyewe nikamwambia anifungie samaki wa buku mbili.

Nikachagua samaki wangu huku nikiwa na tabasamu la kusahau shida kwa dakika chache nitakazotumia kumnyanvua samaki na minofu yake. Mama akachukua samaki akawafunga kwenye gazeti na kumimina chumvi kiasi. Kwa kuwa biashara ni cash to cash basi ikabidi nitoe wallet nimpe pesa yake. Ningaingiza mkono mfuko wa nyuma sikuona wallet nikasema hivi kumbe nimeweka mfuko wa mbele kuangalia mfuko wa mbele wallet hakuna, nikasema nini tena nikaangalia mifuko yote Hola jasho jembamba likianzaga tu kunitoka ujue kweli. Yule mama akasema napitia nikamwambia Sawa aendelee tu kuwauzia abiria wa nyuma akianza kurudi atapitia...

Ikabidi niangalie chini ya seat huenda imedondoka yani Sasa mpaka mwili ukawa unatetema kichwa hakipo sawa na wale samaki nikawadondosha chini kwenye abiria huwa wanapita tukiwa tumekaa.

Nikasema hapana sio kweli wallet imeenda wapi?? Ilibidi nipaniki nikamnyanyua yule mzee tukiokuwa tumepanda nae mzee alivyoniona tu kuwa sipo Sawa nikaona akasimama nikawa naangalia kila Engle ya seat lakini sikupata wallet yangu yenye pesa zangu.

Abiria wa pembeni yangu wakaniuliza kulikoni nikawaambia kilichotokea wakaishia tu kunipa pole. Nikajisemea labda nikiweka kwenye begi? Lakini sio kweli maana mpaka begi linawekwa kwenye boot la bus nilichomoa pesa yangu nikiwa ndani ya bus nikanunua maji tukiwa Mbagala rangi tatu. Nikiwa nimechanganyikiwa nikasikia konda anatangaza kijiji flani jina nimesahau Kuna jamaa yupo nyuma akasema kwa sauti "shusha" konda akamwambia asogee mbele maana washafika ikumbukwe kuwa Ile misamaki kipindi nasechi wallet yangu nilidondosha chini ya tule tunjia twakupita abiria, jamaa aliekuwa anashuka akapiga akazikandamiza na American buti zake samaki zote zikawa chapati tena zikagandamana na kapeti la bus.

Ile nasema we jamaa umekanyaga samaki zangu akajibu kwa hasira hapo ndo bakuli ilipo samaki unazibwaga njiani, ikabidi ninyamaze Sasa nikawa sipo Sawa kabisa maana wallet siioni samaki sijalipia na mama ndo huyo anakuja kutoka nyuma kudai pesa ya samaki shilling 2000 na samaki zimekanyagwa hazitamaniki kiasi ambacho hata paka hawezi kula.

SEHEMU YA TATU

SEHEMU YA NNE

SEHEMU YA TANO

SEHEMU YA SITA

SEHEMU YA SABA

SEHEMU YA NANE

SEHEMU YA TISA
Kuna wallet ya kahawia niliokota stendi ya Rangitatu ikiwa na pesa isiyozidi 70,000/= nadhani itakuwa ni yako, nitumie namba yaki ya simu nikurushie.
 
Wakati watu wanatoka Lindi kuja Dar, ni uzezeta wa Kiwango cha juu sana, ni mkurupukaji asiyefikiria ndio maana ata story kazira kwa jambo dogo tu

Dar umeshidwa hata kwenda kutembeza maji na soda kule Kariakoo, unaondoka na buku 5 kwa siku, au ukaenda kumenya viazi bar huko wakakupa msosi huku ukitafuta kazi nyingine za maana
huyu jamaa muongo
 
Chai imestukiwa,eti akampiga kichwa kibaka akaona. Nyota nyota ahaaaa
Kwa nini nasema nichai...huwezi kwenda sehemu mara moja ukakariri majina ya shule zote,vijiji jina la walimu,kirahisi kama hujakaa huko jaoo mwezi unless uwe unaaandika sehemu,w ewe umeishi huko kusini na umefundisha huko acha chai bloo
 
Sana asee Yani majina yte anayataja tena kuwa usahih adi sehem ambazo amefk mar moja hyu itakuwa Lindi kaishi mda mrefu san
 
Mwanaumee km mwanaumee ktkt utafutaji tunapitiaa mengi sanaaa ,hapaa ninaposomaa uzii huu napitiaa magumu mpk naonaa ninachokisomaa kwa jamaa bado naonaa alipitiaa madogo maana yy bora hata alikuwa anakutanaa na binadamu Wanamsaidiaa mia mia mbiliii ,kuliko mm nilikutana na wanyamaa badala ya binadamu walitakaa kuniuaa nakunila kbs ,ila MUNGU acha aitwe MUNGU
Itabidi utupe hiyo stori siku moja na unitag
 
Back
Top Bottom