Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Hapana kiongozi acha tu maana humu Kuna watu wanajiona ni mataita wakudadisi nakunya distinction ya kipi cha ukweli na kipi cha uongo basi mm nimewapa fursa hiyo wachunguze ikiwezekana wasafiri hata huko nilikopita. Huu uzi ulikuwa una sehemu mpaka ya 25 na hayo matukio niliyoeleza ni baadhi tu na nichamtoto maana nilitaka kueleza madhira niliyopitia mpaka ningekuja kueleza nimefikaje chuo lakini mtu anadandia treni kwa mbele. Na Leo sio kucheka na kufrahishana Bali nikukupa funzo kuwa Kuna watu wanapitia magumu mpaka shilingi ya kuchota ndogo moja kwa wiki haipati lakini tunapishana nao barabarani na huko mbeleni yaani sehemu ya kumi na tano na sehemu ya kumi na saba ambayo sijaweka humu kutokana na baadhi ya wapuuzi lilah Kuna mtu angetoa machozi kwa misukosuko iliyonipata. Namshukuru mungu ni mzima nawatakia jioni njema

Usisikilize hao wanaokukatisha tamaa, endelea kutuletea simulizi yako! Nakuhakikishia hii inaweza kutengenezwa movie na ikakulipa balaa! So ukiendelea na simulizi mpaka mwisho kuna faida kubwa sana utapata! Unaweza shangaa mzee baba unapata connection ya Hollywood!! Karibu uendelee na simulizi. Tunasubili
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI​

Basi baada ya kina Kidagaa na bosi zake kuondoka, nikaona isiwe tabu kwa vile njia naijua nikaanza kutembea kufuata uelekeo wa lile basi lilipopita huku nikiangalia alama za matariri ya basi la MACHINGA ili nisije kupotea. Niliendelea na safari kwa muda wa masaa matano bila kupumzika na begi langu la nguo likiwa kichwani. NIkapita sehemu nikakuta wanacheza prutable. Kiukweli walinishangaa sana wale wacheza prutable lakini mimi sikuwajali nikaendelea na safari yangu huku begi lipo kichwani.

Kufika mbele kidogo giza lilishaanza kuingia nikaona hapa sina jinsi itabidi tu nitafute mti nilale juu. Na wakati huo njaa inauma kweri kweri. Sasa wakati najadili jinsi gani nitapata chakula na mti wa kulala, nikaona kwa mbali taa za gari. Ikumbukwe giza lilikuwa tayari lishaingia na mimi lengo langu lilikua nifike Lindi Mjini ili kesho niende Mlandizi kwa rafiki ake baba. Nikaona ngoja nilipungie ili gari linaweza kunisaidia kufika Lindi Mjini. Gari ile ikakairbia na kweli ikasimama. Ilikua ni Nissan Hardbody. Aliekua kwenye gari akashusha vioo vya gari nikaweza kumuona vizuri, dah huwezi amini alikua ni Yule mwarabu wa basi la MACHINGA alienirudishia nauli na kunikataza nisipande ile costa yao. Pembeni ya mwarabu alikua Kidagaa. Yule mwarabu akanitukana na kuniambia nitafia porini kwa sabu ya ujuaji wangu kisha akapandisha vioo na nikamsikia Kidagaa anasema IMEISHA HIYO, gari likatimua vumbi.

Kiukweli nilichoka sana na kuanza kujilaumu huu ujuaji unaniponza kwa kweli sasa nitafia kweli kwenye miji ya watu.

Itaendelea ………………………….
Hahahahaaa
Daaaah!!!!!!!
 
Mpwayungu Village vp!! Hebu tuendelee na sehemu ya 14!!!! Na hii Blue monday tukipata muendelezo itakuwa swadakta!! Mambo ya kususa ni ya kina dada!! Wanamme hatususi!! Twende kazi Mwanangu!!!... bilashaka utaitikia wito na kuanza kuporomosha life story yako kali sana!! I think It’s the best story ever narrated in JF.? Endelea sasa baadae tukatengeneze Movie Hollywood!!@MpwayunguVillage
 
Imeishaa iyooh
IMG-20220521-WA0027.jpg
 
Back
Top Bottom