stubborn wa Njombe
Member
- Dec 8, 2016
- 79
- 170
Wanajamvi habari za leo.
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika kwa kuwapa kwa ufupi tukio lililosababisha nilete huu uzi .
Kuna rafiki yangu ni Mchungaji wa kanisa moja hivi la kipentekoste huku tunapoishi. Kwa vile kanisa lake bado ni changa hivyo sadaka hazikidhi mahitaji ya familia yake. Nilimpa gari yangu ndogo ili afanye uber baada ya mida ya ibada. Lakini changamoto ikawa kwenye service ya gari anapitiliza mpaka 6000km bila kumwaga hata engine oil.
Kwa vile mimi ni mganga njaa kama yeye nikamwambia hiyo gari ukiharibu mimi na wewe wote tutakuwa masikini ila nakutafutia kazi ambayo itakuwa haikubani kwa hizi shughuri zako za ibada. Hivyo kuna jamaa yangu mmoja hivi mtu wa Asia huko alikuwa anahitaji dereva wa kupeleka watoto wake shule kwa gari ndogo hivyo ilikuwa kazi inayoisha saa tisa alasiri kisha anawahi kwenye kuchunga kondoo wake.
Tukakubaliana vizuri na mimi nikamjulisha yule muasia aliniomba akaanze kazi haraka iwezekanavyo nami nilimpa taarifa Mchungaji ili akaanze kazi. Lakini si ya tukio alikuja na habari mpya kuwa ana shemeji yake ni muhitaji zaidi wa hiyo kazi kuliko yeye. Nilimuuliza kwa hiyo wewe utaweza kusubiri tutafte sehemu nyingine kwa kipindi hiki alisema sawa ila shemeji yake anadhalilika. Kwa vile yule ndugu Muasia sikumtajia jina la huyu bwana Mchungaji basi tukampachika huyo bwana shemeji aende kuanza kazi .
Alifanya kazi siku nne akaenda kwa bosi wake na kuomba advance salary , bosi wake alishangaa then alinipigia kutaka kujua kama ampe au asimpe . Ki ufupi huyu bwana shemeji mimi hata sura yake siijui na wala sijawahi kumuona . Kwa kumuamini mchungaji nikamwambia mpatie tu huyo hana shida kwa vile ni mfanyakazi wako kwa sasa hivi. Ndugu muasia alimpatia laki mbili ili bwana shemeji wa mchungaji aka solve personal issue zake .
Hela alipewa ijumaa hivyo juma mosi hakuna kazi , ilipofika juma pili usiku alimtumia sms ndugu Muasia kuwa amefiwa kijijini kwao tena huko kijijini kwao kumbe ndio nilipozaliwa mimi kwa jinsi alivyomwambia yule Muasia. Muasia alistuka alihisi ameshapigwa laki mbili yake. Saa kumi na moja asubuhi Muasia alinitumia sms whatsApp kuwa anahisi yule jamaa ajafiwa ila atakuwa ameacha kazi. Nilimwambia asijali mimi nitaenda nyumbani kwake ili kujua kuhusu huo msiba ila kiukweli nyumbani kwake sipajui wala nini nilikuwa naimani amefiwa kweli kwa vile nilikuwa ninamuamini mchungaji.
Sasa kizungumkuti kilianza hapo mchungaji alipokea simu yangu siku ile tu baada ya kumtaarifu lile tukio , akanituia namba ya bwana shemeji ili niongee naye mimi mwenye . Kiukweli bwana shemeji alikiri kuwa hakuwa amefiwa bali amepata kazi sehemu nyingine inayomlipa zaidi ya pale kwa Muasia. Nilimwambia sasa kwa nini ulichukua hela za watu wakati unajua hauna nia ya kuendelea na kazi.
Ili kulinda urafiki wangu na yule muasia ilibidi nimrudishie ile hela yake. Pia niliomba radhi kwa yote ya yaliyokea na nilimshauri yule kijana kuwa kwenye maisha ajitahidi sana asiongozwe na njaa na ajitahidi sana kuongeza marafiki badala ya maadui . Nilimwambia kupitia yeye atasababisha nisije kumdhamini mtu yoyote yule nisiye mjua.
Laki mbili ya kula watoto wangu yeye amenilazimisha kumlipia deni tena ilikuwa Januari ya kulipa ada.
Mniwie radhi kwa kuandika maelezo marefu sana . Sisi wakulima TZS 200,000/- ni nyingi sana kwetu.
Nawasilisha