Sitelekezi mtoto niliyezaa nje ya ndoa

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,421
40,409
Watoto ni baraka ndani ya familia; wengi wanatafuta watoto na wengine hukosa kabisa kupata watoto, na hatimaye kukimbilia kulea watoto wa ndugu au wa jamii nyingine.

Watoto wakiwa wadogo huwa ni changamoto hasa kwa kuhitaji malezi bora, huduma muhimu, ambazo zitahitajika huduma za kifedha kufanikisha malezi yao.

Kutokana na changamoto za kifedha, upelekea baba au mama kutelekeza watoto, na hatimaye watoto kuishi katika mazingira magumu na kushindwa kutimiza ndoto zao.

Hasa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa, wengi wao hukutana na hii changamoto, ambapo baba hutelekeza mtoto kwa mwanamke aliyezaa naye nje, na hatimaye mtoto kuishi katika mazingira magumu.

Majuto huja kutokea, baada ya miaka ya kiutu uzima, pale baba atakapofikisha miaka 60+, ambapo atakuwa anahitaji faraja kutoka kwenye uzao wake.

NB: Kama juzi uliipanga vizuri kufika leo, hakutakuwa na shida; ila kama hukuipanga vizuri, lazima kuwe na shida.

Mfano halisi:-

Mzee wangu katika ujana wake aliweza kuzaa na mwanamke mmoja nje ya ndoa, alizaa naye watoto 2 (ke na me).

Mnavyojua tena maisha ya ujana, mzee hakugharamia malezi, ila mama yao alipambana nao mapaka wakakua.

Mbaya zaidi mzee hakuwahi kufuatilia maendeleo ya wale watoto au hata kutaka kujua wanafanya nini.

Baada ya miaka mingi kupita, zaidi ya 30; mwaka jana watoto wamekuja kumtafuta baba yao. Mbaya zaidi mama yao alishafariki, kwa hiyo watoto walitaka kumfahamu baba yao.

Mbaya zaidi, watoto wanaishi nje (Mmoja Botswana, mwingine USA); baada ya kuulizia ulizia, ndipo wakaelekezwa kwa mzee, huko machame Moshi, wakafunga safari mpaka kijijini.

Walipofika tu; sura zote zinafanana, wakapokelewa na wakafanya mila, na kuanza kueleza hisia zao, na pia kufurahi kumuona baba yao.

Baada ya kufahamiana; vijana waliondoka zao, kwenda kupambana na maisha yao huko ugenini; kwa sababu kwa sasa na wao wana miji yao huko waliko.

Lakini mzee hana sauti, hawezi kuwaambia chochote, na kwa sasa wale vijana wako bize na maisha yao tu.

Nilichojifunza: Sitelekezi mtoto niliyezaa nje ya ndoa, kesho yangu siijui.

Karibuni kwa mjadala.
 
Sasa mzee wako alitaka awes na sauti gani
 
Back
Top Bottom