Sitamani kuzaa mtoto wa kike

Sitamani kuzaa mtoto wa kike

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,849
Kuna matukio mabinti wa siku hizi wanafanya mpaka nakosa hamu ya kuja kuwa na mtoto wa kike maana yanatia aibu na kichefuchefu, fikiria mzazi unakutana na picha ya binti yako akiwa uchi wa mnyama kwenye mitandao hivi utajisikiaje,

Mzazi unatumia pesa nyingi kukupeleka binti kako shule mwisho wa siku anarudi akiwa na mimba mtaa mzima unakucheka, nawapenda sana watoto wa kike ila kuna visa nikiviona nachukia kuzaa mtoto wa kike maana wanaibisha sana.
 
Alafu maajabu ya Mungu uzao wako ukute ni watoto wa kike tu na watakuwa msaada na neema sana maishani mwenu,kwani watoto wa ngapi wa kiume wanafanya mambo ya ajabu.Omba Mungu akupe watoto kama kina isaka,daniel,esta,watoto wenye baraka na si machukizo mbele ya Mungu wazazi na jamii nzima.
 
Unaweza pia ukazaa mtoto wa kiume afu akawa shoga au waulize wenzako wenye watoto wao mateja, watakusimulia Shida wanazozipitia na hao watoto. Mshukuru tu Mungu kwa mtoto yoyote utakayepewa, mlee kwenye misingi iliyo bora na umuombee tu. mengine wanayopitia watoto Ni mipango tu ya Mungu
 
Mtoa mada ni kweli unaweza ukawa unachukizwa na hizo tabia za watoto wa kike, nakwambia hujakutana na mtoto wa kiume mwenye tabia chafu, sasa sijui utatamani usiwe na mtoto kabisa. Mtoto ni malezi mazuri na kumpa hofu ya Mungu tu
 
Yaani me mpaka nakuhurumia mkuu Molembe me nna watoto wa kiume acha kabisa mkuu! Hivi hebu niambie,vp ukiwa na toto la kiume halitaki shule,jizi na ni teja unapata furaha gani!? Mtoto wa kike hana athari sana kwa mzazi hata jamii. Ukimuona uchi Binti yako,yeye mwenyewe anakuwa amefanyiwa tukio hilo bila ridhaa yake. Mwenye mtoto wa kike mmoja tu ajitokeze me nimbadilishie nimpe wawili wa kiume!
 
Last edited by a moderator:
Shy land

Nakusikitia kwa sababu,bado una akili za kivulana bado.Fahamu kuwa mtoto yeyote ni malezi yenye maadili na kumwomba mungu awe na hofu ya mungu.Sijui utapozaa wa kiume halafu yote mashoga/bwabwa utaficha sura au utarudi kufuta haya maneno yako.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni kutokana na malezi yako kwa mwanao kuna watoto wakiume wanakuwa mashoga vp hyo haikupi shida?kuna page za picha za kiume za utupu vp hyo haikupi shida bila Huyo mwamamke mtampataje huyo mtoto wa jinsia isiyokukera.ni bora mtoto aniletee mimba au ukimwi kuliko mtoto awe shoga..jitahid katika malezi na kuwa karibu kiurafiki na kiuadui kwa mwanao utaona tofaut ya ukisemacho
 
Molembe
Hiyo mimba anakuwa kapewa na mtoto wa kike mwenzie? Nakuombea kwa Mungu upate matoto ya kiume. Moja liwe jambazi, likuibie mpaka wewe. Jingine liwe teja na jingine liwe kibaka wananchi walitie kibiriti. Labda ndo utajua watoto wa kike wana thamani kama mama yako mzazi alivyo na thamani kwako.
Shy land
Amina. Mungu akubariki upate toto la kiume liwe shoga. Wanaume wenzie walitafune mpaka kwenye masofa ya sebuleni kwako mchana kweupe.
Heaven on Earth
Umeona eh? Nadhani hawajazaliwa na mama hawa wana watoka pabaya.
sister
Hapana, waache wajaliwe watoto wa kiume ambao watawatoa machozi na kujutia makauli yao machafu kama vyoo vya stendi ya Sumbawanga.
 
Last edited by a moderator:
tian
Hapana Mungu atasikiliza dua lake. Atampatia watoto wa kiume aliowataka. Lakini atajuta kwa kufuru hii labda afute kauli vinginevyo atazaa mashoga na vibaka. We mwache tu.
 
Last edited by a moderator:
Wewe jitahidi kwenye malezi tu hakuna mtoto aliye bora kuliko mwingine, Kila siku huwa naambia watu hakuna mtoto mzuri kama wa kike na ni kweli iko hivyo, Ni muda wa mpito tu akiupita huwa hakuna tatzo lingne zaidi kulinganisha na hao wa kiume mnaowasema eti ni bora.
 
Hivi ulikaa ukatafakari kabla hujaandika haya?
Na hao watoto wa kiume mtazaa na wanaume wenzenu?
Na wewe unaesema mtoto wa kike ni laana hata sijisumbui kukuuliza kitu.
 
Yote ni malezi tu..kama wewe utavaa vimin na kukesha kwenye social networks mtoto wako atakuwa kama ulivyo wewe
 
kuharibika kwa mtoto iyo ni Matokeo ya jinsi gani umemlea na ni jinsi gani unashirikisha familia yako na uwepo wa mungu. walee wanako katika imani ya hofu ya mungu uone kama watafanya upumbavu. halafu jua kua mtoto ni mipango na ni zawadi kutoka kwa mungu sasa unavoilaani kazi ya mungu cjajua unamaana ip labda. of course nimekereka.
 
Back
Top Bottom