Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!?

Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!?

majibu aliyopewa sio ya kweli,wamekuta kasoro kubwa sana hasa upande wa kulia (right hemisphere) ya ubongo wake. uwezo wake wa kubuni mambo ni mdogo, anakurupuka sana kwenye maamuzi, na pia mafanikio yake huwa hayaji in a natural way mpaka awe na mtu amfanyie.

pia wamekuta ni mzuri sana kuona lakini kusikia kuna matatizo.
uchungzi hauishia hapo wamekuta pia na ugonjwa wa kusahau (alzemia) . Iinteeligent quotient (IQ) ya mzee iko chini.

kimsingi wameshangaa sana kuona mtu mwenye matatizo haya anaongoza nchi, ili kuwapa wananchi amani wakasema hivyo.
hta hivyo amepewa dawa za kupunguza tatizo la kusahau
 
..huo uchunguzi wa afya alifanyiwa ktk nchi gani? Jamaica,Cuba,au Trinidad and Tobago?

..je, alipatwa na matatizo ndiyo akalazimika kwenda hospitali na kufanyiwa uchunguzi, au walishapanga toka wanaondoka Tanzania?

..halafu kwanini wananchi wanataarifiwa baada ya Raisi kutoka hospitali, na siyo wakati anapelekwa hospitali?
 
..huo uchunguzi wa afya alifanyiwa ktk nchi gani? Jamaica,Cuba,au Trinidad and Tobago?

..je, alipatwa na matatizo ndiyo akalazimika kwenda hospitali na kufanyiwa uchunguzi, au walishapanga toka wanaondoka Tanzania?

..halafu kwanini wananchi wanataarifiwa baada ya Raisi kutoka hospitali, na siyo wakati anapelekwa hospitali?


Wasipotaarifiwa kabisa kutakuwa na shida gani?

location ya uchunguzi inakusaidia nini?

Si lazima upate matatizo ndio ufanye vipimo..ukipata fursa hiyo wakati wowote kwani wewe ni dakatari wa rais?

Maswali mengine hayana maana yeyote zaidi ya kupoteza wakati kuyajibu...ndio maana nasema rais anazungumza sanaaaaa mpaka vitu vya kijinga
 
KUtoka mwananchi:

NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.

Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?
mimi naomba kukupinga mkuu mwanakijiji.kusema kweli kwa maaumuzi yanaofanyika nchini humu ni vizuri hivi vipimo vya akili vifanyike mara kwa mara na sio kwa raisi tu bali na viongozi wengine wa nchi na matokeo yawekwe kwa uma.

kwa jinsi nchi inavyoendeshwa nina huakika kila mtu kashawahi kujiuliza kuhusu akili za viongozi wetu na naomba waendelee kabisa kumpima akili raisi na viongozi wengine.
 
Tumain said:
Wasipotaarifiwa kabisa kutakuwa na shida gani?

location ya uchunguzi inakusaidia nini?

Si lazima upate matatizo ndio ufanye vipimo..ukipata fursa hiyo wakati wowote kwani wewe ni dakatari wa rais?

Maswali mengine hayana maana yeyote zaidi ya kupoteza wakati kuyajibu...ndio maana nasema rais anazungumza sanaaaaa mpaka vitu vya kijinga

Tumain,

..Raisi siyo mtu wa kawaida kama mimi na wewe.

..ndiyo maana hata alipokuwa amepanda lile bembea kule Jamaica tuliletewa taarifa na tena ikawa headline kwenye magazeti hapa nyumbani.

..wakati Raisi anaondoka hapa tuliambiwa anakwenda kufanya shughuli tofauti kabisa na kupanda mabembea, na kwenda hospitali kwa uchunguzi. ndiyo maana nikauliza maswali niliyouliza.

..si jambo la kawaida kwa Raisi wa nchi kwenda hospitali anapokuwa ugenini. akifanya hivyo naamini wananchi wake wanapaswa kutaarifiwa mapema bila kuchelewa.
 
KUtoka mwananchi:

NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.

Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?
.Wewe ni nani mpaka uchukizwe na kukerwa wewe ni daktari wa rais?

.Si lazima kufanya vipimo baada ya dalili unaweza kufanya vipimo wakati wowote unapopata fursa hiyo?

.unajidhalilisha mwenyewe kwa kule kufikiri kwamba unadhalilika endelea kuwa na mawazo finyu na mgando endelea kudhalilika maana uanpenda kuwa hivyo by the way.. kufanya vipimo ni normal medical routine

.wangeweza kugundua ana matatizo ya akili! yes asingeweza kuwa rais kwasababu angekuwa mgonjwa...hoja yako umekaa kama vile hilo ndilo lililokusukuma kuandika huu upupu
 
He sasa na wananchi tuliomchagua inabidi tukapime akili kwa sababu yawezekana na sisi tukawa na matatizo kwani tulichagua tabasamu (mvuto) baada ya kiongozi wa kutuonyesha njia.
 
Angekuwa na akili timamu asingeachia haya yaendelee!

Jana nilikuwa na safari ya kwenda airport nikitokea nyumbani maeneo ya mikocheni. Nilitoka nyumbani saa 8 mchana, nikapitia Ali Hassan-Bibi titi-Nyerere road. Kuanzia mjini niliona askari wa traffic kila mahali kwa idadi isiyo ya kawaida. Nikahisi ni matatizo ya umeme kwenye taa za kuongozea magari hivyo wanakuja barabarani kutoa msaada. Cha kushangaza ni kwamba baada tu ya kufika maeneo ya kiwanda cha sigara karibu na TAZARA, foleni ikawa kubwa magari yote yamesimama.

Tumesimama kama masaa mawili hivi, kisha nikaona ving'ora na magari yakitoka mbio upande ninakoelekea. Kumbe ni mheshimiwa rais alikuwa anapita. Ndio akili ikanijia! Ala! Kumbe ndio sababu ya yote haya. Kutoka pale mpaka nijinasue na msongamano ule, nilifika airport saa 11 jioni. Safari ya nusu saa ikawa imenichukua masaa 3.

Nikaanza tena safari ya kurudi nyumbani, hali ikawa ni ile ile. Kutokana na ule msongamano uliosababishwa na rais, ule msongamano wa kawaida wa siku zote ukawa mara mbili zaidi. Nilifika nyumbani saa mbili usiku. Safari ya nusu saa ikawa tena imenichukua masaa 3.

Ninasikitishwa sana na hali hii. Dar es salaam ina msongamano wa magari kwa sababu ya ufinyu wa miundo mbinu yake. Halafu mtu maarufu kwa jina 'mheshimiwa' anadiriki kuuongeza bila aibu ili yeye awahi baada ya starehe yake ya kubembea. Hawa anaowanatisha barabarani ndio wale wanaomzalishia kodi ya kufanya asiyotakiwa kufanya ikiwemo kubembea (kama vile hakupitia utoto) na kwenda hospitali kupima akili wakati hili ni wazi linadhihirisha hali ya akili yake.

Kama tusipobadilisha jinsi ya kufanya shughuli zetu tutaendeleaje? Barabara tulizo nazo hivi sasa licha ya kuongezeka magari kwa maelfu, sio tofauti sana na tulizokuwa nazo miaka 20 iliyopita. Namaanisha hakuna uwiano wa ukuaji. Swali langu la kwanza ni kwanini tuendelee na tabia ileile ya kuzuia magari yote jiji zima wakati 'mheshimiwa' anapopita kama tulivyokuwa tunafanya miaka hiyo tukiwa na magari kumi?

Miaka ya sitini na sabini rais alikuwa anapita na kingo'ra ili jiji lote lijue(wakati huo watu na magari ni machache na mfumo ulikuwa wa kibabe). Je ni lazima hadi leo tuendelee kufanya hivyo hata kama tunajua shughuli za uzalishaji mali zinasimama?

Barabara zinaanzaga kufungwa pindi tu ndege inapokaribia kutua, au rais akiwa anajiandaa lisaa limoja kabla ya safari. Je kuna umuhimu wa kuendelea kufanya hivyo hata kama tunajua shughuli za maendeleo zimesimama kwa kuwa 'mheshimiwa' hajajenga barabara za kutosha?

Ni kwa nini askari polisi wanajaa barabarani kuzuia magari ya wananchi walipa kodi na wazalishaji mpaka 'mheshimiwa' apite halafu na wenyewe wanatokomea kusikojulikana na kuwaacha watu barabarani wanateseka kwa msongamano waliousababisha? Hii nchi inamtumikia mtu mmoja? Ni kwa nini basi tulipe kodi? Kuwalipa polisi kumtumikia 'mheshimiwa' tu?

Kama 'mheshimiwa' anatumia barabara ya uelekeo moja, ni kwa nini watumiaji wa uelekeo mwingine wasiruhusiwe kuendelea? Hata barabara kama ya Nyerere, lane za kushoto ziko mbali kabisa na lane za kulia. Ni kwa nini zote zizuiwe wakati mheshimiwa anahitaji kutumia moja tu at a time? Kuna siri gani ya ajabu hapa? Mnaohusika mmeliona hilo?

Mbona nchi nyingine zilizoendelea viongozi wao hawana misafara? Wanakaa kwenye foleni na wananchi wa kawaida hivyo wanapata changamoto ya kuleta mabadiliko? Kama hatuwaigi walioendelea tutaendeleaje?

Mimi nakerwa sana na muda unaopotea barabarani pasipo na sababu ya msingi. Mengi ya tunayoyafanya ni mapokeo ya tangu enzi za mkoloni, hakuna anayetaka kuumiza kichwa kufanya mabadiliko. Ni wakati sasa wa kuyatizama.
 
KUtoka mwananchi:

NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.

Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?
Ni majuzi tu daktari wake alisema alipimwa presha ya damu kwenye macho na kichwa. Kapimwa tena Lo! labda kuna kitu
 
KUtoka mwananchi:

NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.

Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?

I can now understand why it takes ages for him to decide mambo muhimu ya nchi.Pia kutokuwa na msimamo thabiti kuhusu mustakabali mzima wa nchi yetu!Ningekuwa mimi ningesema tu nilichekiwa afya BUT anything kuhusu akili ningeweka kibindoni!It will spark controversy!!!
 
Very nice JK nadhani sasa utakuwa na uwezo wa kutatua matatizo ya wadanganyika baada kucheck ubongo you can now surmone all of your leaders!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Rais Kikwete arejea nchini toka ughaibuni, ajibu mapigo kwa makada wa CCM
Na Sadick Mtulya
RAIS Jakaya Kikwete jana alirejea nchini akitokea Cuba na kujibu mapigo ya makada mbalimbali wa CCM wanaomtuhumu kushindwa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema anajipanga kujibu tuhuma dhidi yake kuwa anashindwa kufanya maamuzi magumu ambazo zilitolewa na makada mbalimbali wa CCM, wakiwemo mawaziri wa zamani.

Lakini Kikwete alidokeza majibu yake kwa kusema: ”Japokuwa ndio kwanza ninafika, sishangazwi na yote mabaya yaliyozungumzwa dhidi yangu katika kongamano hilo. Ningeshangazwa kama ningesemwa vizuri.”

Jakaya, ambaye alikuwa anarejea kutoka ziara ya takribani wiki mbili kwenye nchi za Jamaica, Cuba na Trinidad na Tabago ambako alihudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, alisema hatishwi na maneno yaliyozungumzwa kwa kuwa watu waliozungumza wanajulikana wanatoka upande gani.

Katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Rais Kikwete alishutumiwa kwa kutochukua hatua madhubuti dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na kukiacha chama kikipoteza mwelekeo na kutekwa na matajiri wachache.

”Japo bado sijapata taarifa vizuri kuhusu yote yaliyozungumzwa katika kongamano hilo; siwezi kushangazwa sana, lakini ninakwenda kupata taarifa kamili na kujadiliana na wenzangu kisha nitajibu mambo yote yaliyokuwa na maana na yale ambayo hayana maana na yaliyosemwa kwa chuki, tutayapuuza tu,” alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisema hashangazwi na hali iliyotekea kwa kuwa binadamu wanatofautiana kimtazamo, lakini akasisitiza kuwa anachojali zaidi ni dhamana aliyonayo kwa umma.

“Kama nilivyosema kuwa nimedokezwa kidogo tu, lakini naomba muelewe kuwa huwezi ukamridhisha kila mtu kwani binadamu wamegawanyika katika sehemu tatu," alisema.

"Asilimia 15 watakupenda, asilimia 15 nyingine watakuchukia na asilimia 70 iliyobaki watabaki wanaangalia upepo unaelekea wapi hivyo tusubiri kuna maamuzi tutafanya,” alisema Rais Kikwete.

Katika mkutano huo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, waziri wa zamani wa menejimenti ya utumishi wa umma, Matheo Qares alisema iwapo rais atashindwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi kabla ya 2010, CCM haina budi kumtosa na kumteua mgombea mwingine wa urais.

Naye waziri wa zamani kwenye serikali ya awamu ya pili, Mussa Nkangaa alisema CCM sasa imetekwa na wafanyabiashara matajiri na kuachana na sera zake za kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, ndio maana imekuwa vigumu kushughulikia mafisadi.

Katibu mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula, katika mahojiano na Mwananchi, alisema tatizo la kupeana uongozi kwa urafiki limefanya taifa liwe na viongozi wasio na sifa na kusababisha mambo yanayoendelea kutokea sasa ndani ya chama hicho kikongwe.

CCM inaonekana kuwa katika hatari ya kuparaganyika kutokana na kuwa na makundi ambayo yanarushiana tuhuma kila kukicha. Tuhuma hizo zimekuwa zikitolewa kwenye mikutano ya Bunge na hivi karibuni zilihamia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu na baadaye mkutano wa kamati iliyoundwa kuchunguza mfarakano huo, maarufu kama Kamati ya Mwinyi na wabunge kilichofanyika Dodoma.

Kikwete, ambaye pia amekuwa akishutumiwa kwa kufanya safari nyingi za nje zinazokula fedha za walipa kodi na huku akishindwa kutulia nyumbani kutatua matatizo mengi yanayoikabili nchi kwa sasa, alitetea safari hizo akisema ni vigumu kwake kuacha safari hizo kwa kuwa hazina mbadala.

Na kuonyesha kuwa hawezi kuziacha, Kikwete akaongeza:“Na wiki chache zijazo ninatarajia kwenda nchini Denmark kuhudhuria mkutano wa Capenhagen.”

Ikulu pia iliwahi kutoa taarifa ya kutetea ziara hizo ikisema kuwa zina manufaa kwa nchi kwa kuwa Rais Kikwete huenda nje kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo. Ikulu ilitoa kauli hiyo baada ya wananchi kulalamika kuwa fedha nyingi hutumika kwenye safari hizo.

Kikwete anatarajia kuongoza msafara wa watu takribani 60 atakapokwenda Copenhagen kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

Kuhusu hali ya afya yake, Kikwete, ambaye alizidiwa nguvu jukwaani mjini Mwanza kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kufanya safari ndefu bila ya kupumzika, alisema yuko salama lakini anatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya.

“Nilipokuwa huko nilipima afya yangu na hasa akili na mishipa ya damu na wataalamu wakaniambia nipo salama. Ninatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya,” alisema Kikwete.

Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa hali yake ni salama wataalamu wamemshauri kupunguza ratiba za kazi za kila siku.
 
Maneno ya rais yanaonyesha matatizo ya akili makubwa kuliko maneno ya daktari yanavyofariji kwamba hana matatizo ya akili.
 
Maneno ya rais yanaonyesha matatizo ya akili makubwa kuliko maneno ya daktari yanavyofariji kwamba hana matatizo ya akili.

Kuna watu hapa unawachokoza! Subiri majibu yao
 
Back
Top Bottom