Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 8, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  KUtoka mwananchi:

  NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.

  Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Labda alikuwa ana maanisha kupimwa afya ya ubongo wake na siyo akili!
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Rais apimwe akili kwani anaonyesha dalili za ugonjwa wa akili? Labda kuna vitu anafanya kama vile kachanganyikiwa ndio maana wakaamua kumpima ugonjwa wa akili.
   
 4. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kama anaweza kuwa na waziri wa wizara nyeti kabisa mgonjwa wa akili[kwa mujibu wa malecela]kwanini asicheki ili kujiridhisha kuwa ni mzima?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  au hawakumwelewa Malecela aliposema anayetakiwa kupimwa akili ni Sofia Simba? Mi hata sijui bwana! I need to have my akili checked too maana ...
   
 6. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  walimwelewa kwamba kuna tatizo na wameamua kuaza kuliondoa kwenye shina, hawataki kukata matawi wakaacha shina, kwasababu kukata matawi hakutasaidia kuondoa matunda si mti utachanua tena na kuzaa matunda yaleyale?kwahiyo dawa ni kuondoa tatizo kuazia kwenye source.
   
 7. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sio lazima uwe na dalili za uwendawazimu ndio ukapime akili bana.
  Wakati mwingine,pressure na mihangaiko ya kimaisha husababisha matatizo akilini bila muhusika kujitambua.
  Checking just lets you know how far you can go without cracking.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Dec 8, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  Matokeo yakoje MKJJ? Isije ikawa miaka yote hii minne tuna mental case magogoni, we can easily confirm through his ministers and so called Makamba.
   
 9. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ina wezekana ni lile tatizo lake la kuzimia kwenye shughuli mbalimbali limefanya madaktari wake waone ni muhimu afanyiwe uchunguzi wa kichwa aka ubongo aka akili
   
 10. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Inaonekana Rais JK ameathirika kisaikoloji, ni hofu ya kuanguka tena mwakani wakati wa kampeni ndio maana kaamua kupima akili.
   
 11. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maadili ya udaktari yanatuambia kwamba ugonjwa wa mtu ni siri kati yake yeye mgonjwa na daktari wake. Inakuwaje Rais anaanza kutangazia umma ugonjwa wake?

  Labda anataka sympathy kutoka kwa wananchi lakini wananchi walio wengi wenye hali duni ni wagonjwa wa kudumu na hakuna hatua yoyote ya maana inayoonekana kwa macho inayochukuliwa kuwahurumia wananchi wa aina hii wasioweza hata kumudu kununua asprin! Tuhurumiane sote!!
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Dec 8, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Rais wetu anapenda sana sifa na ujiko wa hovyo hovyo ....hiyo ndo shida, bado anadhani anaweza kushika vichwa vya habari kwa vineno vineno kama hivyo.
   
 13. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kukosoa matamshi haya ya mkuu wa nchi tena aliepimwa na kukutwa hana matatizo ya akili ni sawa na kuendelea kuhoji majibu ya madaktari. Tena madaktari sijui wa Trinidad na tobago, cuba au Jamaica kwamba hana matatizo ya akili.

  Kwakua raisi hana matatizo ya akili, alimaanisha alichokisema na si vinginevyo.
   
 14. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi wetu tulishahisi rais wetu ana matatizo kutokana na yanayofanyika, tunashukuru kama amedhihirishia umma kuwa analo tatizo. Matokeo ya vipimo ni siri yake na daktari - anaweza kutangaza chochote (hasa kama analo hilo tatizo). Cha msingi ni wananchi kuchukua hatua - kama akili zetu pia ziko hivyohivyo basi tutaendelea naye tu.
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  NIFAFANUE::::: KULINGANA NA TAARIFA ZA WATAALAM!!!!!

  Unapopata jambo la kushtusha nk au kusononesha hata baada ya tukio hilo kupita... bado taswira au pacha ya lile tatizo huwa linabaki ndani ya fikra na taswira ya muadhirika ...kama uliona mtu akigongwa na gari...juzi .... hata leo picha inakuruduia na kukutatiza...picha sio halisi ...Lakini inalandana kabisa na lile tukio halisi... ni pacha wa lile tukio halisi .... lakini ... madhara yake ...huwa ni makubwa na yanaweza kuleta tatizo kuu hata mpaka mwilini.

  Kama kuna watu wanakutisha na kukutia woga... nk wanaweza kubakia kama pacha ndani ya fikra na mawazo...

  Kama kuna watu wanAkudai ... na mnavutana na mihadi unashindwa kuitekeleza .... pacha anayetokea ndani ya muadhirika anaweza kuwa mkubwa na akeleta matatizo mwilini nk

  Raisi wetu ametishwa au anatishwa na nini?

  Kundi la watu? Wakina nani? Kwa malengo na mihadi gani?

  Malengo ya kazi yake...? Ni Nini hakijatimiaa?

  Ana mapacha wangapi ndani yake wanao mtatiza..?

  Mapacha hao LAZIMA WAKAPIMWE NCHI ZA NJE? Kweli??????

  Na utatuzi wa mambo kama haya ni nini?

  SI KUCHUKUA UAMUZI MGUMU?

  DO THE IMPOSIBLE !!

  DO WHAT SOULD BE DONE...!!!

  !!!!!!!!!!!!!!KUACHANA NA UBIA NDANI YA IKULU!!!!!!!!!!!!!
   
 16. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lazima yeye au madaktari wake wameshaliona tatizo hili. Naamini zaidi ya uchunguzi wa kawaida ambao mgonjwa hufanyiwa kwa kupimwa vipimo mbalimbali kuchunguza afya yake " general medical check up" ( ambao nasisitiza hauhusisi kupima akili), madaktari huamua vipimo vya kumpima mgonjwa kutokana na maelezo yake au historia ya maradhi yake.

  Hivyo huenda kabisa maelezo ya mh au madaktari wake na historia ya maradhi yake yamefanya madaktari waone kuna uwezekano wa yeye kutokua na akili timamu hivyo kuona ni vyema kumfanyia uchunguzi ili kubaini hali yake na ikiwezekana aanzepata matibabu.

  Hii nadhani ilifanyika punde tu baada ya kutoka kubembea na mkewe huku nchi na chama chake kikifuma moto hivyo madaktari wakawa na kila sababu ya kuwa na wasiwasi na akili yake.

  Nilazima idhihirike pia vipimo vyote hufanyika baada ya maridhiano baina ya mgonjwa na daktari, hivyo ni ukweli usio na shaka kwamba, "mgonjwa" aliridhia akili yake ipimwe na hii ama ilipendekezwa na yeye au madaktari baada ya kumwelezea sababu na umuhimu wa yeye kupimwa akili.

  Ombi
  Kwakua mkuu amekua muwazi juu ya afya yake, na kwakua amesha amua kuujulisha uma juu ya vipimo alivyofanya na kwakua siku zote tumekuwa tukipewa taarifa juu ya maradhi na sababu za kuugua kwake " rejea report ya madaktari wake baada ya kuanguka Mwaza".

  Tunaomba, au yeye mwenyewe, madaktari wake au msemaji wa ikulu watueleze yafuatayo:
  1. Ni vipimo gani alivyofanyiwa alipokua nje ya nchi
  2. Nini sababu na kwanini ilionekana ni muhimu kufanyiwa vipimo hivyo hasa akili
  3. Kwanini akili yake imepimwa wakati huu ambapo utawala wake unalaaniwa kila kona ndani na nje ya chama kwa kuboronga na kuvurunda
  4. Kwanini watanzania waendelee kua na imani na raisi na serikali yake hasa ukizingatia raisi haamini juu ya uwezo wake wa kiakili
  5. Kwanini vipimo vya akili yake vifanyike nje ya nchi na wala si Mirembe ambapo wagonjwa wengine wote wa akili nchini wamekua wakipimwa na kwanini hili listafsiriwe kama kudharau wataalamu wetu wa akili na matumizi mabaya ya fedha za umma.

  Tunaomba majibu kabla ya kuwataka watanzania ambao wanaakili na wanaamini akili zao kutoendelea kumuweka kitini mtu asie amini akili zake mwenyewe.
   
 17. A

  African Member

  #17
  Dec 8, 2009
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Raisi kubembea ilhali asilimia 38 ya wananchi wake wanaishi chini ya mlo mmoja ni mzima kweli???????? huko ku-vascodagama kulikopitiiza kwaweza kuwa ndo dalili za matatizo ya akili.
   
 18. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Tanzaniaaaahhhhhhhhh
   
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,497
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Hivi wakati anbembea Jamaica alishapimwa akili au bado. Maana anything could have happened since hawakuwa na uhakika wakati anabemeba kama alikuwa ni mzima au mgonjwa!!!! Maana nafikiri alikuwa hajapimwa. Kwa nini Dr. wake alimuachia mtu anayehisiwa kuwa mgonjwa kubembea???
   
 20. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Basi waliompigia kura nao wakapimwe !
   
Loading...