Sitaki kufa nifanyeje?

Sitaki kufa nifanyeje?

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
686
Reaction score
589
Remmy aliimba "kifo hakina huruma". Hichi kifo ni nini?

Dini na imani mbalimbali zina mambo mengi kuhusu kifo. Zingine zinasema kufa ni kupumzika tu kipindi unasubiri ufufuo, ukishakufa umemaliza kila kitu duniani na ndo milele hiyo haitakuja kutokea umefufuka, ukifa roho yaenda mbinguni!

Hivi baada ya kifo kuna maisha kweli! Nahitaji mtu aliyekufa akaendelea na maisha mengine huko asimulie hapa ili nijue ng'ambo ya kaburi kuna nini! Mawasiliano ya roho ni magumu sana kuelewa kwamba mtu akifa mwili ndo unaoza ila roho/nafsi inaendelea kuishi sasa sijui inaishi wapi..

Wakristo wanaamini kuwa wapo watu watakuwa hai kipindi cha ujio wa yesu wa mara ya pili. Waislam kwa upande wao wanasema kila nafsi itaonja umauti kwamba kila mwanadamu atakufa, sasa hapa haizingatii watoto wanavyozaliwa kila siku au hawaamini katika ujio wa pili wa mwana wa Adam.

Swali la msingi nifanyeje ili nisife kwa sababu sitaki kuona naiacha dunia ni tamu kweli kweli japo ina raha na maudhi ya kila aina.. Nahitaji immortal body. Naona kifo hakichagui wafanya mema, mabaya na hata ufanye chochote unakufa tu.. Dawa ya kutibu kifo ni nini? Ukifikiria kifo mwili unapata ubaridi na kujiuliza ng'ambo ya kaburi kuna maisha mengine!!

Sintofahamu hii!!! [emoji58] [emoji58] [emoji42] [emoji42]
 
Kamuombe mwanafuz akuasist papuch yake
Kifo utakua unakiskia tu
 
Pole sana, imeamriwa kwa watu kuishi mara moja na baada ya kufa hukumu. Utumie muda na zamu yako vizuri katika dunia hii. Ishi na watu vizuri, watendee wema, acha alama nzuri katika maisha na hata zamu yako ikiisha utaendelea kuishi katika kumbukumbu za watu. Kwa kadiri watu wanakukumbuka utaendelea kuwa hai... na ukiwa na imani basi ya upande wa pili wala yasikuogofye sana. Ni sawasawa na mtoto kutoka tumboni kwa mama yake. Akiwa tumboni maisha yake yote yanategemea tumbo, wazo la kuwa kuna maisha nje ya tumbo la uzazi alipo.. na akitoka huko analia lakini hakuna namna ni lazima atoke. Na hupokewa kwa mikono ya wanaompenda.. kilio chake wakati wa kujifungua na hofu zote za wakati wa kuzaliwa hutulizwa anapokumbatiwa na kupendwa. Cha kuhofia wakati mwingine ni namna tu ya tutakavyoondoka lakini ukimuamini Mungu, unajiachia katika wema wake. Kwa waliomuamini Yesu hawana hofu kwani imeahidiwa "waniaminio mimi hawatokufa!" Yoh. 11:25
 
Of all the wonders I yet ever seen, it seems to me most strange that man should fear death while knowing that it is a necessary end that it will come when it will..
William shakespear
 
Pole sana, imeamriwa kwa watu kuishi mara moja na baada ya kufa hukumu. Utumie muda na zamu yako vizuri katika dunia hii. Ishi na watu vizuri, watendee wema, acha alama nzuri katika maisha na hata zamu yako ikiisha utaendelea kuishi katika kumbukumbu za watu. Kwa kadiri watu wanakukumbuka utaendelea kuwa hai... na ukiwa na imani basi ya upande wa pili wala yasikuogofye sana. Ni sawasawa na mtoto kutoka tumboni kwa mama yake. Akiwa tumboni maisha yake yote yanategemea tumbo, wazo la kuwa kuna maisha nje ya tumbo la uzazi alipo.. na akitoka huko analia lakini hakuna namna ni lazima atoke. Na hupokewa kwa mikono ya wanaompenda.. kilio chake wakati wa kujifungua na hofu zote za wakati wa kuzaliwa hutulizwa anapokumbatiwa na kupendwa. Cha kuhofia wakati mwingine ni namna tu ya tutakavyoondoka lakini ukimuamini Mungu, unajiachia katika wema wake. Kwa waliomuamini Yesu hawana hofu kwani imeahidiwa "waniaminio mimi hawatokufa!" Yoh. 11:25
Lakini wajuaje mawazo ya mtoto awapo tumboni.. Siri nzito sana ukomo wa mawazo ya mwanadamu ni sekunde anayoishi hana uhakika katika sekunde inayofuata atakuwa wapi..
 
Sali sana usiku na mchana Mungu anaweza kukuonea huruma, jiepushe na papuchi, bia na starehe zote ili upate maisha ya milele na milele
 
Yesu akija hatufi tena?
Hakuna kufa tena, makaburi yatawaachia wafu watapewa miili mipya na sisi tulio hai kufumba na kufumbua tutabadirishwa na kuvaa miili ya kutokufa tayari kwa hukumu.
 
Kama hutaki kufa Goma kula!
mungu ataona uko serious na atakubatilishia kifo.

Mgomo uwe endelevu bila kikomo.
 
Ukifa unazaliwa tena ila ni sayari nyingine, unakuwa kiumbe mwingine ila Roho yako hyohyo.
 
Remmy aliimba "kifo hakina huruma". Hichi kifo ni nini?

Dini na imani mbalimbali zina mambo mengi kuhusu kifo. Zingine zinasema kufa ni kupumzika tu kipindi unasubiri ufufuo, ukishakufa umemaliza kila kitu duniani na ndo milele hiyo haitakuja kutokea umefufuka, ukifa roho yaenda mbinguni!

Hivi baada ya kifo kuna maisha kweli! Nahitaji mtu aliyekufa akaendelea na maisha mengine huko asimulie hapa ili nijue ng'ambo ya kaburi kuna nini! Mawasiliano ya roho ni magumu sana kuelewa kwamba mtu akifa mwili ndo unaoza ila roho/nafsi inaendelea kuishi sasa sijui inaishi wapi..

Wakristo wanaamini kuwa wapo watu watakuwa hai kipindi cha ujio wa yesu wa mara ya pili. Waislam kwa upande wao wanasema kila nafsi itaonja umauti kwamba kila mwanadamu atakufa, sasa hapa haizingatii watoto wanavyozaliwa kila siku au hawaamini katika ujio wa pili wa mwana wa Adam.

Swali la msingi nifanyeje ili nisife kwa sababu sitaki kuona naiacha dunia ni tamu kweli kweli japo ina raha na maudhi ya kila aina.. Nahitaji immortal body. Naona kifo hakichagui wafanya mema, mabaya na hata ufanye chochote unakufa tu.. Dawa ya kutibu kifo ni nini? Ukifikiria kifo mwili unapata ubaridi na kujiuliza ng'ambo ya kaburi kuna maisha mengine!!

Sintofahamu hii!!! [emoji58] [emoji58] [emoji42] [emoji42]
Kwani kifo ni nini?Yani ni kitendo gani hufanyika ambacho ndiyo huitwa kufa?

Kwani ni nini ambacho unafanya sasa ili uishi,uwezo uliyonao sasa ambao unautumia ili kuishi na hadi sasa hujafa basi ndiyo huohuo unatazui kufa.

Kwahiyo njia ya kufanya ili usife ni kuendelea kufanya hichohicho unachofanya sasa chenye kukufanya uwe hai.

KWAHIYO KUZUI KIFO NI JAMBO RAHISI SANA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom