Sitaki kufa nifanyeje?

Sitaki kufa nifanyeje?

Remmy aliimba "kifo hakina huruma". Hichi kifo ni nini?

Dini na imani mbalimbali zina mambo mengi kuhusu kifo. Zingine zinasema kufa ni kupumzika tu kipindi unasubiri ufufuo, ukishakufa umemaliza kila kitu duniani na ndo milele hiyo haitakuja kutokea umefufuka, ukifa roho yaenda mbinguni!

Hivi baada ya kifo kuna maisha kweli! Nahitaji mtu aliyekufa akaendelea na maisha mengine huko asimulie hapa ili nijue ng'ambo ya kaburi kuna nini! Mawasiliano ya roho ni magumu sana kuelewa kwamba mtu akifa mwili ndo unaoza ila roho/nafsi inaendelea kuishi sasa sijui inaishi wapi..

Wakristo wanaamini kuwa wapo watu watakuwa hai kipindi cha ujio wa yesu wa mara ya pili. Waislam kwa upande wao wanasema kila nafsi itaonja umauti kwamba kila mwanadamu atakufa, sasa hapa haizingatii watoto wanavyozaliwa kila siku au hawaamini katika ujio wa pili wa mwana wa Adam.

Swali la msingi nifanyeje ili nisife kwa sababu sitaki kuona naiacha dunia ni tamu kweli kweli japo ina raha na maudhi ya kila aina.. Nahitaji immortal body. Naona kifo hakichagui wafanya mema, mabaya na hata ufanye chochote unakufa tu.. Dawa ya kutibu kifo ni nini? Ukifikiria kifo mwili unapata ubaridi na kujiuliza ng'ambo ya kaburi kuna maisha mengine!!

Sintofahamu hii!!! [emoji58] [emoji58] [emoji42] [emoji42]
Wewe huzitaki zile bikra kadhaa huko peponi?
 
Kuna mambo ukikaa na kuanza kuyawaza ni kujiumiza tu, kikubwa ni kukubali kuwa yapo.

Ni ujinga kuogopa jambo ambalo unajua wazi kabisa litakutokea ni sawa na kuogopa kula eti utenda kunya.

Tenda wema kwa manufaa ya roho yako na sio mwili wako.
 
Hakuna kufa tena, makaburi yatawaachia wafu watapewa miili mipya na sisi tulio hai kufumba na kufumbua tutabadirishwa na kuvaa miili ya kutokufa tayari kwa hukumu.
Soma ufunuo vizuri, hata Yesu akija tutakufa halafu dunia itasambaratishwa, shetani ataletwa duniani na kupata mateso yake i think ni kwa miaka 40 halafu atatupwa kwenye ziwa la moto then ufufuo ndio utafuata na wateule wa Mungu wataelekea mbinguni na wale wa shetani watamfuata kule alipo
 
Kwani kifo ni nini?Yani ni kitendo gani hufanyika ambacho ndiyo huitwa kufa?


Kwani ni nini ambacho unafanya sasa ili uishi,uwezo uliyonao sasa ambao unautumia ili kuishi na hadi sasa hujafa basi ndiyo huohuo unatazui kufa.

Kwahiyo njia ya kufanya ili usife ni kuendelea kufanya hichohicho unachofanya sasa chenye kukufanya uwe hai.


KWAHIYO KUZUI KIFO NI JAMBO RAHISI SANA.
Duh
 
Lakini sikulaumu hilo jina lako tu linaonesha unaipenda sana hii dunia!
 
Una nongwa wewe...

Swali la msingi nifanyeje ili nisife kwa sababu sitaki kuona naiacha dunia ni tamu kweli kweli japo ina raha na maudhi ya kila aina.. Nahitaji immortal body. Naona kifo hakichagui wafanya mema, mabaya na hata ufanye chochote unakufa tu.. Dawa ya kutibu kifo ni nini?
 
Itakuwa ndo unakaribia karibia kufa maana aliwazalo mjinga ndilo litalomtokea soon
 
Tafuta farasi na gari lake, lichomoe speed 120 , uenda yatakukuta yaliyomkuta nabii Elia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom