Sitaki kufa nifanyeje?

Sitaki kufa nifanyeje?

hapo unatakiwa kwenda kwenye ghorofa reeefu kisha unapanda halafu ukiwa juu unasema nataka kuwa immortal mara 3 kisha unajiachia ukija tua chini baada ya dakika kama 10 hivi utajihisi mwepesi na uko free hapo ndipo umekuwa immortal ilambinu hii ni kwa mara moja tu ikifanikiwa ipasavyo nakutakia maisha ya u immortal bro.(angalizo dhara lolote litokanalo na njia hii mm sitahusika kwa lolote uzi huu ni kwa elimu tu jaribu on your own risk) mimi nina kama miaka isiyopungua 25 kwa njia hii
Mimi nna miaka 290 sasa hivi kwa style hiyo. Naikubali. Ila jihadhari na kuotangaza kijana
 
Post iwafikie ma Ethiest wote..@Al - Watan @Charmilton
Ohh brother, mbona swali lako hujalifafanua?. Umesema hutaki kufa. Nani kakwambia utakufa?. Wewe uliumbwa kuishi milele, na ndio ulikuwa mpango wa Mungu kabla ya kumuumba Adamu. Kosa walilolifanya Adamu na Hawa, ni kula lile tunda walipodanganywa na nyoka. Kama Adamu na mkewe wasingekula tunda lile, wangeendelea kula matunda, hata kufikia kula matunda ya mti wa uzima uliokuwa pembezoni mwa bustani ya Eden. aliupuliziaKwa kula matunda ya mti wa uzima, wangekamilisha mpango wa Mungu, yaani kuishi milele wakiwa katika mwili wa nyama( udongo.). Hebu sasa tuangalie wazo lako la kutotaka kufa. Kifo alichoambiwa Adamu na Hawa, ni kuzitenganisha Roho(pumzi ya Mungu), Nafsi(maamuzi kuhusu mema na mabaya), na Mwili( Udongo,au mwili wa nyama). Hiki ndio kifo alichoambiwa mwanaadamu kuwa lazima atakipitia. Mtu akifa, una chini una kimekufa ni mwili wake, ambao ndani yake Roho, na nafsi vimetoka. Kumbuka Mungu alipoumba udongo aliupulizia pumzi yake ambayo ni ya kuishi milele . na pumzi ilipoungana na mwili, kulitengenzwa kitu kingine kilichoitwa Nafsi. Hivi viwili(roho+Nafsi), havifi vinaendelea kuwa pamoja Mtu akifa, kama alikuwa amempokea Yesu , na kuishi maisha mema, roho yake itaenda paradiso,au ahera. Kama akifa akiwa hajampokea Yesu, na maisha yake aliishi katika maovu, roho yake itaenda kuzimu au Sheol, mahali wanapoishi mizimu . Mzimu ni roho+ Nafsi ya aliyekuwa na mwili akafa katika dhambi... Angalia sasa gone mpaka hapo bado aliyekuwa na mwili akafa, bado anajitambua kuwa yeye ni nani, na alikuwa na elimu au cheo gani duniani, ikiwa ni pamoja na kuwa kumbuka watu alioishi nao duniani kama vile ndugu, wazazi, watoto, mke., NK. Angalia mfano wa Tajiri na maskini Lazaro katika Luka 16:19--31(mfano aliusema Bw. Yesu mwenyewe.. Kaka, baada ya kufa, maisha yanaendelea katika paradiso, au kuzimu, Mtu akingojea Siku ya hukumu ambapo kila Mtu atasimama kupokea hukumu ya jinsi alivyoishi hapa duniani. Kumbuka kuwa kuzimu, na ahera, ni sehemu za kusubiri Siku ya hukumu. Hakuna kula, hakuna,kulala, wala hakuna SAA pale kwa sababu usiku na mchana viko duniani tu. Ukienda nje ya dunia hakuna usiku kwa sababu roho, haihitaji mwanga wa jua wala mwezi ili kuangalia mzingira. Kifo cha kutenga mwili na roho, ni kama kulala ,maana Mtu atafufuliwa ili apokee hukumu. Kifo unachotakiwa kukiogopa ni ile mauti ya pili,( kutengwa na upendo wa Mungu) yaani kutupwa katika ziwa la moto. ambamo roho+Nafsi zitateseka milele bila kufa. Wewe usiyetaka kufa, Mpokee Yesu tu. Siku ya hukumu , ambayo atakayehukumu walio hai na wafu, ni yeye Yesu; hivyo atakukaribisha katika uzima wa milele. Usiogope kifo cha kwanza kila Mtu atakionja. Hata parapanda itakepolia, wore watakaokutwa wakiwa bado hai katika mwili, watabadilishwa kwa sekunde, maana yake wataonja mauti na kufufuliwa ndani ya muda mfupi. Mpokee Yesu , kisha kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, hutakufa mauti ya pili, ambayo, ni kuishi milele mbali na upendo wa Mungu ndio ziwa la moto..Good day, brother.
 
Pole sana, imeamriwa kwa watu kuishi mara moja na baada ya kufa hukumu. Utumie muda na zamu yako vizuri katika dunia hii. Ishi na watu vizuri, watendee wema, acha alama nzuri katika maisha na hata zamu yako ikiisha utaendelea kuishi katika kumbukumbu za watu. Kwa kadiri watu wanakukumbuka utaendelea kuwa hai... na ukiwa na imani basi ya upande wa pili wala yasikuogofye sana. Ni sawasawa na mtoto kutoka tumboni kwa mama yake. Akiwa tumboni maisha yake yote yanategemea tumbo, wazo la kuwa kuna maisha nje ya tumbo la uzazi alipo.. na akitoka huko analia lakini hakuna namna ni lazima atoke. Na hupokewa kwa mikono ya wanaompenda.. kilio chake wakati wa kujifungua na hofu zote za wakati wa kuzaliwa hutulizwa anapokumbatiwa na kupendwa. Cha kuhofia wakati mwingine ni namna tu ya tutakavyoondoka lakini ukimuamini Mungu, unajiachia katika wema wake. Kwa waliomuamini Yesu hawana hofu kwani imeahidiwa "waniaminio mimi hawatokufa!" Yoh. 11:25
Well said
 
Remmy aliimba "kifo hakina huruma". Hichi kifo ni nini?

Dini na imani mbalimbali zina mambo mengi kuhusu kifo. Zingine zinasema kufa ni kupumzika tu kipindi unasubiri ufufuo, ukishakufa umemaliza kila kitu duniani na ndo milele hiyo haitakuja kutokea umefufuka, ukifa roho yaenda mbinguni!

Hivi baada ya kifo kuna maisha kweli! Nahitaji mtu aliyekufa akaendelea na maisha mengine huko asimulie hapa ili nijue ng'ambo ya kaburi kuna nini! Mawasiliano ya roho ni magumu sana kuelewa kwamba mtu akifa mwili ndo unaoza ila roho/nafsi inaendelea kuishi sasa sijui inaishi wapi..

Wakristo wanaamini kuwa wapo watu watakuwa hai kipindi cha ujio wa yesu wa mara ya pili. Waislam kwa upande wao wanasema kila nafsi itaonja umauti kwamba kila mwanadamu atakufa, sasa hapa haizingatii watoto wanavyozaliwa kila siku au hawaamini katika ujio wa pili wa mwana wa Adam.

Swali la msingi nifanyeje ili nisife kwa sababu sitaki kuona naiacha dunia ni tamu kweli kweli japo ina raha na maudhi ya kila aina.. Nahitaji immortal body. Naona kifo hakichagui wafanya mema, mabaya na hata ufanye chochote unakufa tu.. Dawa ya kutibu kifo ni nini? Ukifikiria kifo mwili unapata ubaridi na kujiuliza ng'ambo ya kaburi kuna maisha mengine!!

Sintofahamu hii!!! [emoji58] [emoji58] [emoji42] [emoji42]
Mpokee Yesu, awe Bwana na Mokozi wa maisha.Kifo cha mwili ni lazima kwa kila binadamu, labda kwa wale tutakaokuwa hai mpaka Yesu atakaporudi 1 Thessalonians 4:17. Ukifa,wakati umempokea Yesu Kristo utaishi milele pamoja na Yesu katika mbingu mpya na nchi mpya Ufunuo 21:1. Roho ya binadamu huwa haifi, ni mwili tu. Roho inaishi milele either jehanamu ya moto penye kilio na kusaga meno,mathayo 13:42, au mbinguni penye raha ya milele ufunuo 21: 4. Don't to choose to go to hell, choose Jesus. He is the only one who can save you from hell.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom