machomanne
JF-Expert Member
- Feb 22, 2017
- 822
- 926
Ohh brother, mbona swali lako hujalifafanua?. Umesema hutaki kufa. Nani kakwambia utakufa?. Wewe uliumbwa kuishi milele, na ndio ulikuwa mpango wa Mungu kabla ya kumuumba Adamu. Kosa walilolifanya Adamu na Hawa, ni kula lile tunda walipodanganywa na nyoka. Kama Adamu na mkewe wasingekula tunda lile, wangeendelea kula matunda, hata kufikia kula matunda ya mti wa uzima uliokuwa pembezoni mwa bustani ya Eden. aliupuliziaKwa kula matunda ya mti wa uzima, wangekamilisha mpango wa Mungu, yaani kuishi milele wakiwa katika mwili wa nyama( udongo.). Hebu sasa tuangalie wazo lako la kutotaka kufa. Kifo alichoambiwa Adamu na Hawa, ni kuzitenganisha Roho(pumzi ya Mungu), Nafsi(maamuzi kuhusu mema na mabaya), na Mwili( Udongo,au mwili wa nyama). Hiki ndio kifo alichoambiwa mwanaadamu kuwa lazima atakipitia. Mtu akifa, una chini una kimekufa ni mwili wake, ambao ndani yake Roho, na nafsi vimetoka. Kumbuka Mungu alipoumba udongo aliupulizia pumzi yake ambayo ni ya kuishi milele . na pumzi ilipoungana na mwili, kulitengenzwa kitu kingine kilichoitwa Nafsi. Hivi viwili(roho+Nafsi), havifi vinaendelea kuwa pamoja Mtu akifa, kama alikuwa amempokea Yesu , na kuishi maisha mema, roho yake itaenda paradiso,au ahera. Kama akifa akiwa hajampokea Yesu, na maisha yake aliishi katika maovu, roho yake itaenda kuzimu au Sheol, mahali wanapoishi mizimu . Mzimu ni roho+ Nafsi ya aliyekuwa na mwili akafa katika dhambi... Angalia sasa gone mpaka hapo bado aliyekuwa na mwili akafa, bado anajitambua kuwa yeye ni nani, na alikuwa na elimu au cheo gani duniani, ikiwa ni pamoja na kuwa kumbuka watu alioishi nao duniani kama vile ndugu, wazazi, watoto, mke., NK. Angalia mfano wa Tajiri na maskini Lazaro katika Luka 16:19--31(mfano aliusema Bw. Yesu mwenyewe.. Kaka, baada ya kufa, maisha yanaendelea katika paradiso, au kuzimu, Mtu akingojea Siku ya hukumu ambapo kila Mtu atasimama kupokea hukumu ya jinsi alivyoishi hapa duniani. Kumbuka kuwa kuzimu, na ahera, ni sehemu za kusubiri Siku ya hukumu. Hakuna kula, hakuna,kulala, wala hakuna SAA pale kwa sababu usiku na mchana viko duniani tu. Ukienda nje ya dunia hakuna usiku kwa sababu roho, haihitaji mwanga wa jua wala mwezi ili kuangalia mzingira. Kifo cha kutenga mwili na roho, ni kama kulala ,maana Mtu atafufuliwa ili apokee hukumu. Kifo unachotakiwa kukiogopa ni ile mauti ya pili,( kutengwa na upendo wa Mungu) yaani kutupwa katika ziwa la moto. ambamo roho+Nafsi zitateseka milele bila kufa. Wewe usiyetaka kufa, Mpokee Yesu tu. Siku ya hukumu , ambayo atakayehukumu walio hai na wafu, ni yeye Yesu; hivyo atakukaribisha katika uzima wa milele. Usiogope kifo cha kwanza kila Mtu atakionja. Hata parapanda itakepolia, wore watakaokutwa wakiwa bado hai katika mwili, watabadilishwa kwa sekunde, maana yake wataonja mauti na kufufuliwa ndani ya muda mfupi. Mpokee Yesu , kisha kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, hutakufa mauti ya pili, ambayo, ni kuishi milele mbali na upendo wa Mungu ndio ziwa la moto..Good day, brother.