Sitaki kuamini wala sitokaa niamini kuwa uchaguzi wa Marudio Monduli waliojitokeza kwenye kura ni wengi kuliko wale wa uchaguzi mkuu!

Habari za wakati huu wadau,
Katika uchaguzi wa marudio wa ubunge uliofanyika katika jimbo la Monduli hivi karibuni idadi ya waliopiga kura ilikuwa;

2015 kati ya 60,000
2018 kati ya 70,000

hapa inaonyesha idadi ya waliopiga kura kwenye uchaguzi wa marudio inazidi idadi ya wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu. Kwa mawazo yangu naona huu ni uwongo mtakatifu. Wa kunishawishi kuwa ni ukweli anisaidie. Asante.
Mh. Sugu huwa anasema bungeni kuwa
"men lie, women lie, but numbers dont lie"
 
Tutashinda wakati wasimamizi hawatakiwi kuwa neutral?
We hujui watu wanashinda vipi uchaguzi?
Kwa hiyo wabunge wote wa chadema kina Mbowe, sugu, lema etc woote walipendelewa sio?
Hizi hoja nyingine za visingizio sio za kutamka mbele ya watu wazima.
 
Kuna watu ambao wengi walisusia kupiga kura baada ya kuona chaguo lao limewatoroka.....
Kama ilivyo kwa CUF (kundi kubwa hasa lenye mlengo wa kidini) walisusa kupiga kura baada ya kuona wamemkaribisha mtu aliueshiriki kutia saini MEMORANDUM OF UNDERSTANDING (Wenye mlengo wa kidini wanajua nazungumza nini)

Kama ilivyokuwa kwa CCM kwa uchaguzi wa 2005 na 2010. WanaCCM wengi hasa waliopiga 2005 walisusa kupiga 2010 na wakapiga 2015. Sintashangaa 2020 kura za CCM Ku-dabo
 
MONDULI ilikuwa ngome ya CCM, kwa mambo ya kijamii yaliyotokea 2015 ikawafanya MORANI/MALAIGWANAN wengine kutokupiga kura......

Sasa wale CCM kindakindaki ambao hawakupiga kura 2015 wamerudi na kupiga kundi lao
Achilia mbali sisi tusio na vyama....ambao tunaenda kulingana na upepo
 
Hii ndiyo sababu ya shangilio lile la mapolisi?
Hatutegemei mtu mwenye akili za kutosha awe analazimisha watu wamuunge mkono kwa nguvu za dola.
Kwa kawaida watu huwa wanatumia nguvu ya hoja kujenga hoja.
Unaposema unatarajia huko Monduli kua za ccm kudabo 2020,wenye akili tunajua kwamba wewe sio sangoma,una mpango mwingine wa kuiba kura mwaka huo wa uchaguzi ukifika.
Ni sawa lkn tambua tu kwamba jiwe la barafu halijengi nyumba
 
Mromboo
Nadhani wewe ndio una mhemko wa kipuuzi.
Swali la msingi ni Je,hiyo idadi ya watu 70,000 inazidi idadi ya wapiga kura walioandikishwa kwenye daftari la 2015?
Jibu ni hapana.
Sasa kejeli za nini?
Okay! Niwaache tu. Uzuri wewe uliko ni tofauti na niliko na niliyoyaona.
 
Kitu ambacho najua ni kwamba pamoja na ccm "kushinda" wanaelewa kabisa hawakubaliki na wananchi.
Hilo wanalijua wazi kabisa..
Hawakubaliki na wale wanaoshinda JF, lakini kwa wale wanaojengewa meli ni lazima wawakubali. Mashujaa wa nyuma ya keyboard hawawezi kuwakubali, lakini wale wanaojengewa zahanati wanawakubali.
 
Hii ndiyo sababu ya shangilio lile la mapolisi?
Hatutegemei mtu mwenye akili za kutosha awe analazimisha watu wamuunge mkono kwa nguvu za dola.
Kwa kawaida watu huwa wanatumia nguvu ya hoja kujenga hoja.
Unaposema unatarajia huko Monduli kua za ccm kudabo 2020,wenye akili tunajua kwamba wewe sio sangoma,una mpango mwingine wa kuiba kura mwaka huo wa uchaguzi ukifika.
Ni sawa lkn tambua tu kwamba jiwe la barafu halijengi nyumba

Umechanganya madesa.... SABABU UA ASKARI KUSHANGILIA NI UCHAGUZI WA UKONGA KUISHA KWA SALAMA KABISA.....
NAWAPONGEZA KWA ASKARI KUJIPONGEZA.......
 
Mbowe ashiriki ili kuendelea kuipa uhalali cdm wa kuwa chama cha siasa. Ila asichowez na ambacho hataweza ni kutulazimisha tujitokeze kupiga kura. Hii idadi ndogo ya wapiga kura tutaendelea kuishusha kudhibitisha kwamba ccm haikubaliki. Huko mbeleni tutapata njia sahihi ya kuiondoa ccm madarakani nje ya box la kura waliloshindwa kuliheshimu.
Jaribu uone cha moto. Unadhani ni uarabuni hapa mliweza Libya na misri
 
Jaribu uone cha moto. Unadhani ni uarabuni hapa mliweza Libya na misri
Uvumilivu una mwisho. Hao wamisri unaowasema,ujinga huu ulidumu kwa miongo kadhaa,hata wasomali unaowaona wanateseka walikataa uonevu kama huu.
Mwisho wa siku wale wapumbavu waliojiona miungu watu kama wa kwetu na wale wahanga wote wameingia katika mateso,wanakufa au wanateseka wote na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Sisi wengine tunatoa tahadhari mapema kwamba:sisi sote ni watanzania,tufanye mambo ya kuijenga nchi,tuache kubaguana kwa misingi ya ukabila,vyama,dini nk
 
MONDULI ilikuwa ngome ya CCM, kwa mambo ya kijamii yaliyotokea 2015 ikawafanya MORANI/MALAIGWANAN wengine kutokupiga kura......

Sasa wale CCM kindakindaki ambao hawakupiga kura 2015 wamerudi na kupiga kundi lao
Achilia mbali sisi tusio na vyama....ambao tunaenda kulingana na upepo
Ni Sawa kwamba ni ngome ya ccm na hata wakati wa uchaguzi hao malaigwanani wasiojua kusoma wala kaandika, huenda kwenye kura na kadi za ccm na kusisitiza wamekuja kuchagua hicho chama. Swali lamsingi ni kwamba Waliojiandikisha 2014 ni 80,000 na waliopiga kura uchaguzi wa marudio 2018 ni 70,000. Kwa akili yako Kweli unaona hizi namba zipo Sawa ukizingatia kwa hiyo miaka minne hakuna mabadiliko yaliyofanyika kwenye daftari la wapiga kura kwa maana kwamba watu wangepungua zaidi? Kuna tetesi toka kwa wasimamizi wa uchaguzi huo kwamba waliojitokeza kupiga kura walikuwa wachache ila idadi ya matokeo iliyobandikwa ilikuwa kubwa kuliko uhalisia, je madai haya hayana uhusiano na hilo la namba nililokueleza hapo juu?
 
Kwa waliokuwa kule siku ya uchaguzi, wanasema waliojitokeza walikuwa wachache mno mno! ccm+nec-ccm+mapolisi-ccm ndio wanajua hizo kura zilitoka kwa wanadamu au kwa wafu.
 
MONDULI ilikuwa ngome ya CCM, kwa mambo ya kijamii yaliyotokea 2015 ikawafanya MORANI/MALAIGWANAN wengine kutokupiga kura......

Sasa wale CCM kindakindaki ambao hawakupiga kura 2015 wamerudi na kupiga kundi lao
Achilia mbali sisi tusio na vyama....ambao tunaenda kulingana na upepo
Hivi ndugu zako na marafiki zako uliofungua nao mwaka wa 2014 hadi leo wapo wote kwa maana kwamba hakuna waliofariki, waliopoteza namba zako, waliovunja uhusiano na wewe ama waliohama eneo lako? Achana na wapya hao hawawezi kureplace.
 
Kesho nitawasimulia mchezo ulifanywa na CCM kwa kushirikiana na Serikali na Polisi Jimbo la Ukonga, baada ya kupewa hiyo story nimejisikia kichefuchefu jinsi ambavyo watawala tuliowaamini wasivyojiamini na ujinga wanaowafanyia Watanzania.

Vv
Imefika tayari
 
Back
Top Bottom