stigajemwa
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 449
- 430
La ! Nimekimbilia kutafuta rekodi za 2015 nikakuta kweli wapiga kura waliopiga kura walikuwa 60000.Habari za wakati huu wadau,
Katika uchaguzi wa marudio wa ubunge uliofanyika katika jimbo la Monduli hivi karibuni idadi ya waliopiga kura ilikuwa;
2015 kati ya 60,000
2018 kati ya 70,000
hapa inaonyesha idadi ya waliopiga kura kwenye uchaguzi wa marudio inazidi idadi ya wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu. Kwa mawazo yangu naona huu ni uwongo mtakatifu. Wa kunishawishi kuwa ni ukweli anisaidie. Asante.
Leo hii ni kweli wameongezeka hadi 69000. Kwa akili ya kawaida haiwezekani idadi ya wapiga kura kuongezeka kwani kuna suala LA watu kuhama kikazi au kimaisha ya utafutaji,kusafiri,kuzeeka na kufa.
Pili kuna suala LA hamasa ya kwenda kupiga kura kupungua kutokana na ukweli kuwa tume ya uchaguzi si huru na inasikiliza maelekezo kutoka juu. Mfano,wakurugenzi waliopewa nyumba nzuri na usafiri na posho wameshaonywa kuwa wasitangaze mpi nzani kuwa ndie ameshinda.
Hivyo naungana nawe kwa kutoa hitimisho kuwa kwa vyovyote vile matokeo haya yamepikwa kwani haiwezekani vituoni kuwe na mwitikio hafifu wa wapiga kura harafu takwimu za mwisho zioneshe wapiga kura wameongezeka na wamezidi hats idadi ya 2015.
Haya mambo yataendelea kutoka Tanzania tu kwa kuwa watu wake wengi ni wavivu wa kufikiri,kusoma na kufanya utafiti. Kwao unafiki na ubinafsi ndio mpango mzima: yaani unamkuta MTU kwakuwa yeye maisha take binafsi yanakwenda vizuri basi anakwambia hataki kufuatilia mambo ya siasa.