Sitaisahau hii!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Hii ilitokea wakati nipo primary school pale mpakani Tunduma.Kwa sababu tuko mpakani,ilikuwa si ajabu mtoto wa TZ kwenda kusoma pale Nakonde,zambia na pia wao kuja kusoma kwetu.Basi one day mwanafunzi mmoja wa kizambia hakuonekana shule na wala hakuomba ruhusa.Siku alipofika shule alipoulizwa sababu ya yeye kutokuja shule akajibu;"samawani mwalimu,'kuku' yetu alikufa,tulimuzika jana".Baada ya maelezo hayo,mwalimu alimbandika vibao viwili vya kutisha huku akisema,"pumbaf,hujafika shule kisa kuku kafa!".Mwanafunzi mmoja wa kizambia akatoa ufafanuzi kwamba kuku kwa kabila moja huko zambia ni Babu,kwa hiyo mwanafunzi yule alifiwa na babu yake na siyo kuku mnaemjua ninyi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom