Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Date::2/11/2009 (mwananchi)
Waziri Mkuu, wabunge waalikwa tamasha la albino Dar
Na Clara Alphonce
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi (albino) lililoandaliwa na Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
Katibu Mwenezi wa UV- CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara alisema kuwa tamasha hilo lililobeba ujumbe wa ' kila kijana ni mlinzi wa albino' litafanyika kesho kwenye Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam
Alisema nia ya tamasha hilo ni kuunga mkono hatua ya serikali ya kukemea mauaji ya albino yanayoendelea nchini kote.
Manara alisema mbali na Waziri Mkuu Pinda, pia kutakuwa na wabunge mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova ambao watatoa ujumbe wao kuhusu mauaji hayo.
Manara aliwataja wasanii mbalimbali watakao tumbuiza katika tamasha hilo kuwa ni TID, Prof. Jay, Soggy Doggy, Wanaume Halisi na Wanaume TMK wakati bendi zitakazotumbuiza ni Msondo Ngoma, FM Academia, Vibration Sound na kwa muziki wa taarab, East African Melody.
My Take:
what is wrong with this picture? Clue: angalia kauli iliyotiliwa uzito. Yaani bendi zote na viongozi waalikwa watakuwa kwa ajili ya lengo hilo.

Last edited: