Chato yaandaa Tamasha la utalii

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
MKUU wa Wilaya ya Chato, Deusdedith Katwale amesema wanatarajia kufanya tamasha la utalii kwa lengo la kutangaza vivutio na fursa mbalimbali za utalii zilizoko katika ukanda huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Dar es Salaam, Katwale, amesema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 26 hadi Desemba 03 mwaka huu.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara katika kutangaza utalii nchini, akieleza kuwa Chato wamejipanga kuona ni namna gani wanaweza kuchangia sehemu ya watalii milioni tano wanaoingia nchini, na kwamba mkakati huo wa Chato Utalii Festival ni sehemu ya mipango ambayo wako nayo ili kuhakikisha wanafikia idadi hiyo ya watalii.

“Malengo mengine ya tamasha hili ni kutoa nafasi kwa umma kutambua fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya utalii, biashara katika Wilaya na Mkoa wa Geita kwa ujumla, na kutoa fursa ya kutangaza na kuhamasisha wadau wa sekata ya utalii kwenda kuwekeza Chato," amesema Katwale.
 
Labda tamasha la kuloga na kutuma fisi
 
Back
Top Bottom