GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,542
- 108,877
Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuwa na taarifa nyingi na za ndani ( Nyeti ) kabisa kuhusu mambo mbalimbali ya nchi na pia nawapongeza mno TISS kwa Utendaji wao wa Kutukuka kwa sasa ila nasikitika na sishauri sana Mheshimiwa Rais awe anapenda mno kuzizungumzia hadharani katika hadhira.
Taarifa za Ugomvi wa Waziri wa Afya na Katibu Mkuu mpya wa sasa ( wote wanatoka Mkoani Tanga ), Ugomvi wa DC wa Gairo na Mbunge wa Gairo hadi wanatukanana Matusi ya Nguoni ya Viungo vya waliotuzaa ( Mama zetu Wapendwa ) pamoja na Mtifuano wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na DC wa Dodoma na hadi Siri za ndani kabisa juu ya Sakata zima la Dhahabu ambalo pia lipo katika Uchunguzi zaidi kwa sasa sidhani kama zilipashwa kuwa ' disclosed publicly ' katika hadhira kwani ' technically ' kabisa linawaharibia mno Watendaji wake Kiusalama TISS.
Sitaki kuamini kwamba Mheshimiwa Rais huwa hawezi Kutunza Siri labda ndiyo udhaifu wake mkubwa ila nimwombe tu sasa TISS DG Dkt. Kipilimba ajitahidi kadri awezavyo aweze ' Kumfunda ' Bosi wake hasa juu ya suala zima la Kunyamaza na kutopenda ' Kuropoka ' mambo mengine ya ndani ( Nyeti ) mbele ya Umma kwani yanaharibu misingi ya Uchunguzi na Kuudhoofisha ' Utendaji ' wa Kisiri. Nina uhakika japo ' Poti ' wangu IGP Sirro amesifiwa sana na Mheshimiwa Rais kwa ' Utendaji ' wake ila nina uhakika hata Yeye pia Kimoyomoyo hajapendezwa na jinsi Rais alivyokuwa anatiririka na anaserereka kulihadithia ' Sakata ' zima la Dhahabu.
Nawasilisha.