Sishauri mtu kusoma PhD OUT

Sishauri mtu kusoma PhD OUT

Mara kadhaa huku kwenye makundi sogozi ya OUT nimekuwa nikiwapa za uso kwa watumishi wake kukosa weledi, hawana customer care kabisa.

Halafu wanakera sana tabia yao ya kutoa matokeo nusu nusu, kwa mfano ikiwa hawaja kuwekea matokeo ya somo moja utasota sana hadi kuja kuwekewa, ukiwajulisha wahusika hawatatui kwa wakati mara wasipokee simu, na hata ukiwacheki WhatsApp utaishia kuchezea blue tick tu.

Kinachochekesha zaidi kwamba wewe ambaye hujawekewa matokeo ndio uwape taarifa ya 'missing results' wao wenyewe sijui hawana mifumo ya kutambua au vipi...!! Wanachofanya hakiakisi maana ya CHUO HURIA, matarajio yangu ilikuwa kuona chuo hiki kinakuwa mstari wa mbele kiteknolojia lakini bado wapo analoji.

OUT mnachosha.!!

Wanachosa Sana mkuu. Wanakera Sana.
 
Mh. Mwendazake ndiyo yaliyomkuta.

Taasisi kama hiyo ya "Chuo Kikuu Huria Tz" na nyingine za serikali ni majanga yani.

Watu wanajikuta sana utadhani walilazimishwa kuomba hizo nafasi za kazi.

Unampigia simu secretary anakata na ukimpigia Tena hapokei. Anakuona kero unamsumbua. Najiuliza wapo pale kwajili ya nani kama mwanafunzi ni kero kwao?
 
Nilitaka nimshauri hivi hivi mkono mtupu haulambwi. Sikuhizi hadi kwenye misiba kuna rushwa. Mc anapewa rushwa ilimradi aseme natambua uwepo wa Adverse effect. Hasa hasa wanasiasa.

Kumbe na rushwa wanachukua. Shida Mimi nilitaka supervisor anisimamie bila influence ya pesa. Kama anataka aseme Sasa.
 
Pole sana mdau! Machungu uliyo nayo NDIYO yaliyonipata! Mimi nilimaliza miaka mitano bila kufanya presentation ya proposal. Yaani unatuma proposal kwenye email jamaa hajibu chochote! Unapiga simu weee lakini wapi! Mwisho nikaamua kuapply chuo kingine, Ada niliyolipa pale kama M3.5 ikaenda bure kabisa! Kwa Sasa nasoma chuo kingine vizuri kabisa hapa hapa TZ! Kile chuo hakina mfumo wa kumonitor masupervisor! Wanapuyanga tu kama wanavyojisikia! NI AIBU SANA KWA CHUO KIKUBWA KAMA KILE KUSHINDWA KUWASIMAMIA WAAJIRIWA WAKE WAFANYE KAZI WALIYOANJIRIWA KUFANYA.

Pole Sana mkuu pia. Inaumiza Sana watu kutojali muda wa wengine. Hata Mimi napanga kuhama hapo na kwenda UDSM. Nimekubali kupoteza pesa zangu zote za ada nilizolipa.
 
Ila Masters wako active sana
Wanatafuta u profesa hao ila
UDSM pia kuna shida sana supervisors kuanzia level ya Masters

Sema hawajui kuwa chuo kikubwa kama UDSM hao una supervise wengine usalama wa taifa au baadaye waweza kuwa mabosi makatibu wakuu,mawaziri,maraisi nk wa kipewa nafasi ya ku recommend nani awe nani in future waweza comment supervisor wao au hata supervisor wao akiwa na Issue anaumwa ,kafiwa ,anaoza nk wanafunzi wake lazima wafurike na kuchangia
.
Sisemi wapewe digrii bure hapana vitu vyote vizangatiwe ila sio kuwa mkorofi supervisor kupindukia .Maisha ni mahusiano lakinii sio ya kupeana marks za bure lakini pia yasiwe ya kusumbuana kupindukia bila sababu za msingi
 
kwa usalama wa mwili na akili waachie ada ukaombe chuo kingine kama
lakini tujikumbushe haya kwa mwanafunzi anayesoma Phd chuo bora na chenye mifumo safi ya technology
mwanafunzi anafatiliwa kabisa hatua kwa hatua kuhusu thesis yake au dissertation yake
mwalimu nae anafatiliwa zaidi kuona kuwa wanafunzi wake wanakamilisha kwa wakati dissertation zao
uongozi wa chuo unafatilia kila hatua na kama mwanafunzi anaonekana kuchelewa unaulizwa sababu nini upo pale kukamilisha ndoto zake na sio kufeli ndio maana mwl akiona unafeli anakurekebisha hizi ndio hatua muhimu kabisa kwa vyuo bora duniani nafikiri kwa afrika hakuna
basi tuyaache hayo acha kusoma hapo omba vyuo hivi nmezipanga kwa mpangilio
  1. ESAMI Home • ESAMI
  2. The Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST)
  3. UDSM
  4. UDOM
  5. SAUT
ila kama una nafasi omba za ulaya

Asante mkuu kwa ushauri wako nadhani nitaenda UDSM.
 
Mimi sijui nipoje,,ila nawoana wanaoenda kusoma OPEN UNIVERSITY HAWANA AKILI,,,wameogopa kwenda Udsm au mzumbe kuogopa kufeli

Sio kweli kabisa. Nilienda OUT kwasababu kule unalipa ada kwa stage yako ya PhD thesis, ila UDSM na Mzumbe unalipa kila mwaka regardless upo stage gani. Hiyo tu. Ila waneniangusha Sana Open.
 
Supervisor akiona kazi yako haina jipya ni AI 75%, copy and paste 85%, haina mchango kwa chuo wala Taifa; hakika atakufanyia hayo yote. Kwa UDSM ungeshadisco; bora OUT wanakuvumilia

Punguza ujuaji. Naongolea kwamba proposal yangu haijawahi kusahishwa Wala kusomwa na supervisor. Kila nikienda hayupo na nikimpigia simu hapatikani kabisa na email hajibu miaka na miaka. Nikitaka kubadilisha supervisor yule secretary wao pale DPGS analeta dharau kibao.
 
Back
Top Bottom