Siridhiki na utendaji wa Baraza la mitihani la Taifa, NECTA

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,549
2,000
Nimeangalia matokeo ya kidato cha 4. Kwa ujumla wake wanafunzi wameshindwa hesabu. Je, Baarza limeleza sababu yake? Hapana! Wako bize kutueleza shule fulani imeongoza.

Baraza hili linalojiita NECTA ni shemu ya wizara ya Elimu. Miaka nenda rudi limeheshimika kwa kusimamia ubora wa mitihani na matokeo yake. Kwa maana nyingine, wanakagua kuona kama wizara mama, imetimiza wajibu wake wa kuwaelimisha watoto wetu. Tunachotaka ni elimu na siyo division 1,2,3,4. Hizo divisions ziwepo lakini kweli tunapozunguma na mtu wa division tuone hiyo division.

Hali haiko hivyo. Hao wote unaowaona division 1, baada ya miaka miwili ya form 5 na 6 unawakuta division 3, 4 na wengine sifuri! Inakuwaje? Hii ni kwa sababu NECTA wameweka sana suala la division kama kipimo cha ufahamu. Hata shule bora sasa ni ile yenye division 1 nyingi jambo ambalo naliona ni upuuzi tu!

Mtendaji mkuu wa NECTA tunaamini kisha sikia maoni kama haya, kwamba aache mtindo wa kututangazia shule ya kwanza, ya pili, nk. Kwa sababu haina maana yoyote zaidi ya kutangaza bishara za watu. Biashara hizi zinakuzwa na NECTA kwa kuzifanya divisions ndo elimu.

Imefikia hatua waalimi wanaiba mitihani ili tu wapate division 1 nyingi. Ubunifu umekuwa ni kujibu maswali madarasani ili wanafunzi wapate division 1. Huu ni upuuzi tuachieni hata division 4 ambaye anaonesha ukomavu na uwezo wa sekondari kuliko division 1 asiyeweza hata kuzungumza mbele za watu.
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,406
2,000
Education sector is relative my friend

Wait and see the comments around here; as we keep on waiting, I have to take you in several concepts concerning what is so called Education;

There is a thing called, Education as the product

Then, there is school stressing on Education as an output

Lastly, there is a last thinkers clarifying education as an outcome

Hii mambo ukiielewa utajaona elimu ina matarajio yake ambayo kila mtu huona vile anavyoona. However Education should obey the rule of thumb where as education taken as the home of critics.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,771
2,000
Ppendekeza unataka wapimwenje kuona kuwa kweli learning has taken place.
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,089
2,000
Nimeangalia matokeo ya kidato cha 4. Kwa ujumla wake wanafunzi wameshindwa hesabu. Je, Barza limeeza sababu yake? Hapana!
Jibu ni ndio.
Sababu za wanafunzi kushindwa hesabu na masomo mengine hubainishwa vizuri kwa kila swali na takwimu kabisa.
Mwisho Baraza huchapisha vijitabu vyenye tathmini ya kila somo na kuzisambaza kwa wadau.
 

sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
6,344
2,000
Wewe ulitaka iweje ili uridhike? Kuloloma peke yake bila kutoa way forward hakukusaidii wewe binafsi.
 

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,981
2,000
Mtoa hoja sawa, una nia nzuri!

Labda tu nikuulize unajua vizuri kazi ya NECTA kwa mujibu wa sheria!

Je, unajua kazi ya taasisi ZOTE za wizara husika? Kuna mgawanyo wa majukumu ya nani asimamie mitaala, yupi asimamie utoaji wa elimu na nani afanye monitoring and evaluation ya ubora wa elimu!

Ningeuliza baada ya NECTA kutoa matokeo yanaonyesha ufaulu au kuanguka kwa maeneo flani hatua ipi inachukuliwa na instrument zingine Za wizara?

Bado una genuine concern!
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,549
2,000
Wewe ulitaka iweje ili uridhike? Kuloloma peke yake bila kutoa way forward hakukusaidii wewe binafsi.
Usiwe vivu, Soma Act iliyoanzisha NECTA na majukumu yake ya msingi. Haya mengine na kuchapisha vijarida vya past papers ni kulawiti elimu yetu.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,532
2,000
Usiwe vivu, Soma Act iliyoanzisha NECTA na majukumu yake ya msingi. Haya mengine na kuchapisha vijarida vya past papers ni kulawiti elimu yetu.

..utasumbuliwa sana na wana-CCM.

..wao wanataka usifie elimu bure.

..hawajali kama watoto wanajifunza.
 
Oct 22, 2020
74
150
Education sector is relative my friend

Wait and see the comments around here; as we keep on waiting, I have to take you in several concepts concerning what is so called Education...
Tuache nadhalia. Tuliosoma wote tunafahamu tulikotoka, tulikopitia, na pale tulipo. NECTA ya leo siyo ile iliyotuweka juu miaka ile. mmoja wetu kisha sema, ya leo tunaiona ikichapisha past papers kuwauzia wanafunzi, wasome maswali.
 

mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,960
2,000
Kila mwaka wanatoa tathimini ya kila somo na wapi watahiniwa wengi walichemka kwenda mikoani hadi mashuleni sasa sijui ulitaka wamwandikie kila mwananchi kwann somo fulani wanafeli hata hvyo wajibu wao wa msingi ni kuandaa mitihani,kusahihisha na kutoa feedback kwa maana matokeo.Acha kuwasingizia baraza matatizo ya kufeli wanafunzi.
 
Jul 29, 2014
54
125
Tuache nadhalia. Tuliosoma wote tunafahamu tulikotoka, tulikopitia, na pale tulipo. NECTA ya leo siyo ile iliyotuweka juu miaka ile. mmoja wetu kisha sema, ya leo tunaiona ikichapisha past papers kuwauzia wanafunzi, wasome maswali.
My young sister ana div one ya 12pts niliwahi kumuuliza second president of Tanzania hakunijibu ila ajabu ana A ya civics,,,,,,halafu uwezo wake naujua kwa div hyo hapaana tunadanganyana
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
10,838
2,000
Huna pakusemea hata wawe wazembe kiasi gani

Huna mbunge wa kumwabia akasemee bungeni maana wote hawawezi hata mmoja kuongea against the govt bungeni

Tutaishia kudiscuss humu kama stori tuu

Walipokua wanaiba kura na kuua watu mlikua mnacheka upinzani uomeondoka,here we are again playing the fool outta ourselves!
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,271
2,000
Kwanza kabisa nadhani NECTA na wizara wangeacha huu mtindo wa ku rank shule kwa ufaulu. Shule iliyofaulisha watoto wengi mara nyingi inakuwa regarded kama shule bora. Lakini ukweli ni kwamba ubora wa shule ni zaidi ya kufaulu wanafunzi. Ufaulu wa wanafunzi ni kigezo moja wapo tu.

Sasa kwa kuwa shule zimeingizwa kwenye ushindani wa kufaulisha mitihani, walimu na wamiliki wa shule wamekuwa busy kuwamezesha au kuwakaririsha wanafunzi maswali ili wafaulu. Hii inawafanya wanafunzi wasijifunze uwezo wa kufikiri yaani analytical skills ndo maana wanafanya vibaya kwenye masomo kama hesabu ambayo yanahitaji analytical skills.

Tunatengeneza kizazi cha watu waliomezeshwa vitu fulani fulani lakini hata hawajui chimbuko na matumizi yake (application).

Kama kweli tunataka kujenga kizazi cha watu walio elimika tuachena na mambi ya ku rank wanafunzi na shule.
 

IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
9,766
2,000
pendekeza unataka wapimwenje kuona kuwa kweli learning has taken place.......
Mtihani wa mwisho uwekewe only 30 % yaani mwanafunzi akipata yote 100 % then it means ana 30 %. The remaining 70 % iwe ni mixture of assignments, presentations, group works, kazi za mikono, usomaji wa vitabu etc.... Kiufupi kutegemea sana mitihani ya mwisho kunaongeza tatizo la kukariri na wizi wa mitihani.
 

IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
9,766
2,000
My young sister ana div one ya 12pts niliwahi kumuuliza second president of Tanzania hakunijibu ila ajabu ana A ya civics,,,,,,halafu uwezo wake naujua kwa div hyo hapaana tunadanganyana
Amekariri tuu hapo au walipewa majibu, hii elimu ni shidaaa...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom