Siri za Nyota na Hatima

Siri za Nyota na Hatima

KUTEMBELEA NYOTA YA MTU MWINGINE!

Fuatana nami

Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️

Je, umewahi kusikia watu fulani fulani huko wakisema "fulani anatembelea nyota ya fulani?"

Na je, nini ulikuwa mtazamo wako kuhusiana na kauli hiyo au kauli kama hiyo?

Tumefundisha kwa miaka mingi kuhusiana na elimu ya Nyota na angalau watu wengi sana waliotupinga kwa nguvu zote miaka hiyo, hususani miaka ya 2019 kuja 2020 na 21, wengi wao ni wadau wakuu wa elimu hii siku hizi. Huo ni ushindi kwa waalimu wote wa ELIMU YA NYOTA kwa Afrika Mashariki na Kati; kwa hiyo hapa sitaanza kwa kuelezea maana ya nyota, acha niende moja kwa moja kwenye hoja.

Unaposikia watu wanasema kwamba mtu fulani anatumia nyota ya mtu mwingine au nyota za watu wengine, ni ukweli usiopingika kabisa.
Kuna uwezekano mkubwa endapo mtu akiamua kutumia nyota yako au ya mtu mwingine, kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa sababu kila mtu ana aina ya nyota inayosapoti mambo fulani tofauti na wenzake.
Aidha, kuna Nyota ambazo zenyewe kwa asili yake zinasapoti nyota zingine hususani Nyota ya Simba na Nyota ya Ng'ombe.

Mtu akianza kutumia nyota yako kwa maslahi yake, ni wazi kwamba wewe unakuwa unamfanyia kazi yeye kwa kujua au bila kujua, unakuwa unamnufaisha yeye.

Kuna njia nyingi za kutumia nyota ya mtu kufanikisha mambo yako, nitataja njia kadhaa:

1. Tendo la ndoa
Hili tendo ambalo wazungu huliita SEX ni tendo ambalo mtu mke na mtu mme wakikutana kimwili, wanabadilishana nishati zao; huyu anabeba za huyu na yule anabeba za mwenzake. Ndio maana ya neno S.E.X ambalo kirefu chake ni Sacred Energy Xchange!
Kila unapokutana kimwili (kingono) na mtu awaye yote, awe mkeo/ mumeo au la, mnachofanya kiroho mnabadilishana nguvu, unampa zako anakupa zake.
Sasa watu wengi wana nguvu au nishati (au roho) chafu ambazo zinaharibu mambo, sasa wakilala na wewe, wanakuachia zao chafu wanabeba za kwako safi, mkitoka hapo wewe unaharibikiwa wao wanasonga mbele (wametumia nyota yako kujisafishia au kuoshea nyota yako)

2. Huduma za jamii
Kama nyota yako ni safi na inang'aa alafu mtu 'akaiona' na akaitaka, anaweza kuanza kujitolea kukusaidia au kukuhudumia mahitaji yako yote bila kuhitaji chochote kutoka kwako.
Kikawaida utamuona ana roho nzuri (ni sawa), lakini kiuhalisia (kiroho) unakuwa unampa uhuru wa kuitumia nyota yako kufanikisha mambo yake.

3. Kugawa fedha na zawadi kama nguo, viatu, saa nk.
Kama mtu 'akiona' nyota yako inang'aa sana, lakini hujitambui, basi anaweza kuichukua 'kwa kuinunua'
Atafanya hivyo kwa kuchukua pesa na kuinuizia manuizo (spells) fulani fulani, kisha atakupatia kwa mkono wa kushoto na atajitahidi kuhakikisha na wewe unapokea kwa mkono huo. Tendo hilo linakuwa ni alama au Ishara ya mauziano, anakuwa amenunua nyota yako.
Asipotumia fedha anaweza kutumia nguo, saa, viatu, soksi au chochote kinachotoka kwenye mwili wake.

ZIPO MBINU AU NJIA NYINGI ZA KUPEANA NYOTA, ACHA NITAJE HIZO TATU TU.

Watu walio kwenye hatari kubwa ya 'kuibiwa' Nyota zao wengi ni wale wa Nyota za Simba na Ng'ombe, wachukue taadhari.
Kuna namna nyingi za kufanya ili kuilinda nyota yako isichezewe.

Nyota yako ikiwa chafu au imechezewa, fanya ufanyavyo, huwezi kutoboa!

Somo litaendelea......
Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

By Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho.


MENEMENE TEKERI NA PERESI Tumwesige senior DIVISHENI FOO Nikifa MkeWangu Asiolewe
 
UNAJIMU (ASTROGEOLOGY)

Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️
IMG-20250629-WA0012.jpg


Tabia za Nyota
Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa. Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.
Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi.
Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.
Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 60 tu. Hii si haba,kuna ukweli basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa

Tabia za Watu na Alama za Nyota
Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.
Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.

Alama hizi ni kama ifuatavyo :
Waliozaliwa Feb 19 – Machi 20 wana nyota ya Samaki (Pisces)

Waliozaliwa Machi 21 – Aprili 19 wana nyota ya Kondoo (Aries)

Waliozaliwa Aprili 20 – Mei 21 wana nyota ya Ng’ombe (Taurus)

Waliozaliwa Mei 22 – Juni 20 wana nyota ya Mapacha🙁Gemini )

Waliozaliwa Juni 21 – Julai 22 wana nyota ya Kaa(Cancer)

Waliozaliwa Julai 23 – Agosti 22 wana nyota ya Simba(Leo)

Waliozaliwa Agosti 23 – Sept 22 wana nyota ya Mashuke(Virgo)

Waliozaliwa Sept 23 – Okt 22 wana nyota ya Mizani (Libra)

Waliozaliwa Okt 24- Nov 21 wana nyota ya Ng’e (Scorpio)

Waliozaliwa Nov 22- Des 21 wana nyota ya Mshale (Sagittarius)

Waliozaliwa Des 22 – Jan 19 wana nyota ya Mbuzi(Capricorn)

Waliozaliwa Jan 20 – Feb 18 wana nyota ya Ndoo (Aquarius)

Makundi ya Alama za Nyota:
Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika sehemu kuu 4 zijulikanazo kama:

Moto : Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi

Maji : Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani

Hewa : Imara na yenye kukuza au kuendeleza
Udongo:Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha
Hizi ni sehemu nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.

Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:
Moto : Kondoo, Simba,Mshale

Maji : Ng’e, Samaki, Kaa

Hewa : Mapacha, Mizani, Ndoo

Udongo : Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi
Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni:
Yenye Umuhimu au Msingi “Cardinal”: Kondoo, Kaa,Mizani,Mbuzi
Yenye Kubadilika “Mutable”: Ng’ombe, Simba, Ng’e na Ndoo
Isiyobadilika “Fixed”: Mapacha, Mizani, Mshale na Samaki
Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama Kondoo
Alama ambayo ipo katika kundi la Udongo na Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.


Haiba na Tabia za Alama za Nyota
1 Nyota ya Kondoo


“Mimi Kwanza” Mimi nasema, mimi nimeamua
Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.
Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine
Mwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juu
Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa
Mwenzilishi wa mambo na mbunifu
Kiongozi
Muongeaji
Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.
Mwaminifu kwa marafiki na familia
Anajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi

2 Nyota ya Ng’ombe

“Nafanya ninachokipenda” Nimepata.
Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakili
Makini na muangalifu
Ana kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisi
Mstahimilivu
Mwenye kutegemewa
Ni mgumu kubadilika
Anapenda vitu vizuri na vya thamani
Unapenda urembo na vitu vya kupendeza
Mwenye hisia zilizofichika
Huenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa na mali au fedha.

3 Nyota ya Mapacha
Ninafikiri, Nadhani “Ninapanga” Ndugu zangu
Ni mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa
Anafikiri kwa haraka na mcheshi
Ni mwasilianaji mzuri
Ni mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko.
Mwenye kuamua kwa akili na mbunifu
Hana utulivu
Ana mipango na malengo makubwa
Mwenye kubadilika kirahisi

4 Nyota ya Kaa
Ninahisi, Nasita, Nakwama
“Nina wasiwasi kuhusu Jambo”Naogopa
Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpautulivu ,usalama na amani
Anapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukoo
Hisia zake ni za wazi na ni rahisi kujulikana
Ana huruma
Ni mwangalifu
Mkimya na

5 Nyota ya Simba

Nitafanya, Nitaanza
“Najifanya” Nitasingizia
Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu.
Anapenda kuonekana na watu
Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe
Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.
Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwa
Ni viongozi wazuri na wenye nguvu
Mwenye matumaini mazuri
Mwenye kuheshimika
Mshindani
Mpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanya
Mwenye mvuto

6 Nyota ya Mashuke

Ninasoma, Nasikitika, nakula, naumwa,Naonewa
“Nina khofu” nitakunywa, nasingiziwa, napoteza, nakunywa dawa, kelele nyingi.
Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengine
Ni mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kazini
Ni mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja.
Wapangili wazuri wa muda na watekelezaji
Ni mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu.
Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao.
Wanajali afya

7 Nyota ya Mizani
Ninashirikiana, Nakusanya, Naimba,Napenda, Nakumbatia
“Nafanya mambo nisiyoyapenda” Nachumbia naunganisha.
Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro.
Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili.
Husimamia haki na usawa
Anapenda sanaa na urembo
Wabunifu wa sanaa
Ni mpenzi wa muziki
Ni muwazi katika kuonyesha upendo
Ana ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamii
Anatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisia
Mpenda amani
Wenye mvuto wa kupendwa

8 Nyota ya Ng’e

Nataka kufanya, Natamani, Nadhibiti. “Ninashuku”Ninahusudu.
Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuri
Mjasiriamali namwenye uwezo wa kukabiliana na vizingiti vikubwa
Anapenda malumbano makali
Wanatumia nguvu
Jasiri
Wastahimilivu
Washindani
Wanauwezo ,
Wachunguzi wa mambo
Wasiri
Ni mpenzi mzuri na mwenye tabia za umiliki
Wanajitegemea
Ni wenye maamuzi

9 Nyota ya Mshale
Ninaelewa, Nafahamu yote, hakuna Nisilojua

Mwanafalsafa na mkusanyaji wa habari
Mwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamoto
Ni mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele.
Ni mwenye kupenda uhuru
Ni mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wake
Rafiki
Mwenye ari
Hawana utulivu
Waaminifu na wakweli
Wanapenda safari

10 Nyota ya Mbuzi
Ninatumia, Nimezoea, naongoza “Sijiamini” Nimebanwa
Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwa
Ni mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri wa mambo-Mtendaji
Ni mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yake
Si mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe.
Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maisha
Mgumu kubadilika
Mbishi na asiyekubari kushindwa kirahisi
Mfanyabiashara
Mwajibikaji

11 Nyota ya Ndoo

Ninajua, Nathibitisha “Usinitegemee”Nitakwepa
Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria.
Wakipekee
Anaejitegemea na hupenda kuwa peke yake
Mwenye huruma
Muona mbali
Mwenye ufahamu wa hali ya juu nma mbunifu
Anafanya marafiki wa aina mbalimbali
Ana utu na mwenye kudai haki
Anapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa haraka
Anapenda sanaa na maisha ya anasa.

12 Nyota ya Samaki

Ninaamini, Ninaota “Ninakwepa”
Ni mkweli na mwenye hisia nzito
Hana ubinafsi
Ni mpenzi mwaminifu na rafiki
Mpenda amani
Ana huruma
Anajitoa
Wana ndoto
Wabunifu
Wana aibu

ITAENDELEA


Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

By Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom