Siri ya waliotumbuliwa NIDA yaanikwa

Siri ya waliotumbuliwa NIDA yaanikwa

View attachment 319505

Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya vitambulisho(NIDA) waliokumbwa na "Operesheni tumbua majipu" walikutwa na mali nyingi "kupita maelezo" kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

Operesheni hiyo ambayo inatekelezwa tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, juzi ilimkumba Dickson Maimu, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa NIDA, Joseph Makani(Mkurugenzi wa Tehama Rahel Mapande (Ofisa Ugavi mkuu)< Sabrina Nyoni (Mkurugenzi wa sheria) na George Ntalima ambaye ni Ofisa Usafirishaji. Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga alisema hatua ya kutengua na kusimamisha watumishi hao imechukuliwa baada ya uchunguzi wa hali ya juu kwenye mamlaka hiyo.

"Walipoulizwa walisema wamepata mali hizo kutokana na mikopo na mali walizonazo" alisema. Waziri huyo alisema uchunguzi zaidi unajielekeza kujua ni jinsi gani sh 180 bilioni zilitumika kusajili watu milioni 6 tu na kati yao kuwapatia vitambulisho watu milioni 2.5 tu.

Mbali na kuwaweka kando watendaji hao, Rais aliagiza vyombo mbalimbali kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha katika mamlaka hiyo ikiwemo TAKUKURU, PPRA na Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

Chanzo: Dar es salaam wire
Tatizo la watumishi wengi katika Tassisi za umma bado hawajafahamu kuwa enzi za Awamu ya Nne zimekwisha. Walijisahau sana. Tumezoea kuona wafanyabiashara wakiwa na ukwasi mkubwa lakini kwa miaka kumi iliyopita hali ilikuwa ni tofauti kabisa. Ndio maana inakuwa vigumu sana kuwashawishi vijana wanaomaliza vyuo kuwa ajira binafsi inalipa wakati ukienda pale TRA, NIDA, SUMATRA, EWURA nk unakuwa tajiri wa kutupwa. Watu tujiulize kwanini Askari Polisi wanahonga ili kupata nafasi ya kuwa TRAFIKI pamoja na kupigwa na jua na mvua! KAMA INAVYOLIPA KUJIUNGA NA TIGO, NDIVYO INAVYOLIPA KUWA MFANYAKAZI KATIKA TAASISI YA UMMA.
 
Sio hivyo tu mkuu, ilitakiwa RITA, NIDA, na vitambulisho vya Taifa kuunganishwa kwa pamoja. Hizi ofisi zina Kazi zinazoshabihiana sana. Ngoja niandike proposal kuhusu hiyo kitu nami nile mpunga
Andika mkuu tuokoe kodi zetu kuchezewa na wajanja, hapo kwenye mpunga usisite kunialika.
 
Nadhani kutumbua haisaidii, nchi imekosa mfumo thabiti unaoweza kuwafanya watu watambue kuwa walipwe ujira kulingana na mtu anavyofanya kazi, au kama ni mfanyabiashara apate faida kulingana na mauzo halali yatokanayo na biashara zake, mifumo ianzie mashuleni hasa kuanzia shule za awali, watu wajue kuwa wizi ni kosa kubwa sana.
 
Haya ya kuhojiwa na kuachishwa kazi tu haitoshi na hata kama watafungwa miaka 20 kila mmoja haitasaidia kuondoa mijitu milafi kama hiyo ya NIDA.
Lazima itungwe sheria ya KUNYONGA mijitu kama hii inayo iibia nchi.
Hili swala la kufungwa halitoshi la watumishi wa umma hawaiyogopi hii sheria ya kufungwa.
Ifike wakati mtumishi akiibia serikali kiasi kinachozidi 10m anyongwe.
Ibaki mtumishi anaeibia serikali kiasi kisicho zidi 10m ndio afungwe.
Bila hivyo hawatakoma hawa wamesha jisahau sana lazima serikali iwakumbushe mijizi kama ipo kwa kuwauwa mijizi yote.
Naamini wakinyongwa mijizi kama 200 tu nchi itakaa sawa na watumishi wa umma watajua wajibu wao.
 
Tawiree !!! Mm au hawa majizi ya NIDA?
180 BILIONI VITAMBULISHO 2.5M ktk tuliondikishwa 6m
Ivi waliopata hivyo vitambulisho walipewa vitambulisho vya madini gani dhahabu au almasi?
Mijitu mifisadi kama hii ya NIDA haina haja hata ya kuiruhusu kuishi ni kuikatisha tu maisha iwe mfano tena wakanyongewe ktk viwanja vya vyuo vikuu ili wasomi na maafisa watarajiwa waone jinsi mijizi inavyo hukumiwa.
Nasema ikitokea sheria na ikitekelezwa kama hivyo hakuna mtumishi wa umma atakae thubutu kuiiba.
 
Mkurugenzi aliyewekwa kandi ni kama vile masamaki, ila yeye kanununua vijumba vingi uswahilini mikocheni, ni mmiliki wa bar, club na ukimbi wa MRC mikocheni
 
Hivi Membe yupo? Anajishughulisha na nini? Maana hasikiki tena!
Vipi na lile jibu sugu la ESCROW? Ilifikia mahali watu wakadharau hadharani kuwa 1 billion ilikuwa ni hela ya mboga!!!! Sasa sijui karudi tena kuchukua hela ya unga au laah!!!!!
 
Rahel Mapande (Ofisa Ugavi mkuu)< Sabrina Nyoni (Mkurugenzi wa sheria)


Mapande ni ndugu na yule aliyekuwa RAS Katavi? na huyu Nyoni ni ndugu na yule alikuwa KM wa wizara ya afya?
 
Back
Top Bottom