SIRI YA MCHEZO.... Wakunuli kuntuli

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
1,633
559
Tofauti ya BIASHARA na SIASA
ikila hasara inaweza buma
wakati SIASA kila mara ukiwa
unang’ara ujue kuna
kinara anayeunda msafara wa
wanaojituma na
kuchuma kwa kukufanya uwe
imara hapo hasara hakuna
KIDUMU CHAMA CHA MASELA…
Ukoloni mambo leo umetupa
uhuru wa bendera
tuone kufuru za wenye hela
TANZANIA ni ‘ demu wa mtungo ‘
wanamuiita CHA WOOTE’’
HANGOVER .. ‘’anaikimbia kwa
kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote
Mkubwa anazuga atasolve…
matatizo ya nchi yake
‘’na gari bovu..’’ halisukumwi kwa
kukaa ndani yake
MAENDELEO ni ile
ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza
je Kukaa karibu na moto ni kuuota
au kujiunguza
hakuna UHURU wa kweli (Africa)
msidanganywe na illusion
na daily tunafeli sababu ya
POLITICAL institutions
CIVILIZATION imeadvance sasa
wanatuua economically
hakuna utumwa mbaya kama ule
wa kujiona uko free
Kuusaka ukweli ni sawa na
kumenya kitunguu
kila ganda litakutoa machozi na
utabaki macho juu
Ukishafika kwenye kiini niambie
nini utagundua
zaidi ya mafaili yaliyounganika
utaghairi kuyafunua
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao
zikatoboka
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao
hazikugeuka NYOKA
sasa wanaujaribu Umungu mtu
kuamua leo nani atatoka
 
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo… stimu zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../
sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/


Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/


Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa
#teamMabiiitoz /
Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/
Haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/


Wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/
bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
Jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/

Ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/
Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?/
HAPANA.... nguvu ya mamba ni maji/
na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu/
kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu /
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../
baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../
najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/
labda kubisha na wakinitisha najihami../ inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
'' Pole MAPROSOO'' ( uhujumu --uchumi ) umefanya umetubu.. /
WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/
na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../
huo ni utumwa pia/Unafanya vijana wanaumia../
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..


CHORUS: ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2
Siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2


VERSE 2:
Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma/
wakati SIASA kila mara ukiwa unang'ara ujue kuna.. kinara/
anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/
KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/
Tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ' demu wa mtungo ' wanamuiita CHA WOOTE/'
' HANGOVER .. ''anaikimbia kwa kupiga ' " mtungi " saa zote /Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/
''na gari bovu..'' halisukumwi kwa kukaa ndani yake/
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../
je Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? /
hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/
na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions/
CIVILIZATION imeadvance sasa wanatuua economically../
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/
Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu/
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..? zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Akiutoa ajiandae kukaa selo kwa siku kadhaa! Amuulize mwenzake wa Kenya na wimbo wake Nchi ya kitu kidogo.......
 
Ni kweli yawezekana kabisa watu walilambishwa bingo wazuge tumepewa uhuru kumbe hakuna la ziada zaidi ya kuachiwa mavitambaa yanayoitwa bendera ...make inatia wazimu, una uhuru kweli alafu kiulaini unakubali kuwekewa masharti eti ndo upewe vyandarua?? stupid!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom