Mistari; Siri ya mchezo fid q ft juma nature

appoh

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
4,902
1,645
Fid Q ft Juma
Nature (verse1):Fid Q
Nilipotoka mbali na
ninaheshimu nilipo
sikuwa na umuhimu kihivyo
stimu zikanipa elimu ya Biko
Kimaandiko kimistari..
hadi fans wanascream nikirap
sikuamini kama nina zali
mpaka nilipoidream hiphop
Wanapagawa…. Na baadhi ya
mambo nayoyajua pia nina uwezo wa kufanya
mpaka madawa yanaugua
Wanapagawa na nyimbo
ngumu hawa #teamMabiiitoz Achana na power window..
sijui rimz za dimpo
haileti bingo, mshiko? Star ishi
simple
sanaa iko hivyo sometimes..
hukataa kukaaa ulipo wanaodharau.. hujiletea
matatizo..hawajui kama
wadau hupendelea kukuona
hivyo
bonge la staa.. donge la njaa..
hauna kitu jikombe ugongwe…mtaaa
ukuone hauna ishu
ukishindwa kujiandaa…
jiandae kushindwa
mjinga utaachwa unashangaa
kumuona Martin Kadinda Usmati anaotinga, majumba
mandinga ya bwana Almasi
je hizi track za harakati ni
ujinga
HAPANA…. nguvu ya mamba ni
maji na umaarufu au kutamba..
kushika namba ni bahati..
sio kipaji kama Kubanda eti
unachana kigumu
kisa track ikivuma sana
kwenye chati haidumu Amani kwa chachage na
MAKUWADI wa SOKO HURIA.
baba asante kwa UTAFITI na
ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA
NYUMBANI… nasikiliza DUNIA
YA SASA ya MARIJAN najiuliza tutarithi nini ikiwa
IMANI ishakwisha tangu
zamani
labda kubisha na wakinitisha
najihami
inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani
‘’ Pole MAPROSOO’’ uhujumu –
uchumi umefanya umetubu
WAZEE ni wahuni hadi soo
waay back before SUGU
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu
na MBWA MWITU wenye siri.. ili
bepari umuabudu
kimahakama, kiserikali, kidini
umsujudu
huo ni utumwa pia Unafanya vijana wanaumia.
Tunaishia kufia mabatani kama
nzi ndani ya glass ya bia CHORUS: ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mchezo naijua mimi tu.. na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua mimi
tu.. na hakuna mwingine (Verse 2):Fid Q
Tofauti ya BIASHARA na SIASA
ikila hasara inaweza buma
wakati SIASA kila mara ukiwa
unang’ara ujue kuna
kinara anayeunda msafara wa wanaojituma na
kuchuma kwa kukufanya uwe
imara hapo hasara hakuna
KIDUMU CHAMA CHA MASELA…
Ukoloni mambo leo umetupa
uhuru wa bendera tuone kufuru za wenye hela
TANZANIA ni ‘ demu wa
mtungo ‘ wanamuiita CHA
WOOTE’’
HANGOVER .. ‘’anaikimbia kwa
kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote Mkubwa anazuga atasolve…
matatizo ya nchi yake
‘’na gari bovu..’’ halisukumwi
kwa kukaa ndani yake
MAENDELEO ni ile
ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza je Kukaa karibu na moto ni
kuuota au kujiunguza
hakuna UHURU wa kweli
(Africa) msidanganywe na
illusion
na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions
CIVILIZATION imeadvance sasa
wanatuua economically
hakuna utumwa mbaya kama
ule wa kujiona uko free
Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu
kila ganda litakutoa machozi
na utabaki macho juu
Ukishafika kwenye kiini
niambie nini utagundua
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA
zao zikatoboka
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO
zao hazikugeuka NYOKA
sasa wanaujaribu Umungu mtu kuamua leo nani atatoka CHORUS: ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mtungi aijuaye kata
komaa… kaza.. kisha utapata
Siri ya mchezo naijua mimi tu.. na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua mimi
tu.. na hakuna mwingine
 
Fid q sio wa kizazi hiki na kizazi hiki hakitamuelewa kwa kuwa falsafa yake kubwa kuliko kizazi hiki ni kizazi cha baadae ndio kitamuelewa kwenye wimbo kamaliza kila kitu hakuna alichobakiza kuanzia wasanii wanaoigiza wako poa mpaka jamii inayodhani ipo huru.Fid q imba ndugu yangu lakini sio kwa ajili ya kizazi hiki.
 
Unapoongelea mwana HIPHOP ambaye ni mwandishi mwenye uwezo wa hali ya juu hapa Bongo hakika hakuna zaidi ya Fareed Kubanda. Jamaa anajua saana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom