Siri ya Mahakama ya Kadhi yafichuka

Siri ya Mahakama ya Kadhi yafichuka

proisra

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2012
Posts
215
Reaction score
159
Utangulizi:

Kwa muda mrefu sasa, "wenzetu katika imani" wamekuwa wakiishinikiza Serikali iweke katika Katiba ya Tanzania kipengele chenye kuitambua rasmi Kadhi Courts (Mahakama ya Kadhi). Hata hivyo LENGO la uwepo wa Mahakama hizi za Kadhi kwenye Katiba siyo kutambulika kisheria kama wanavyodai, bali ni ili Umma wa Watanzania (wenye dini na wasio nazo) ubebe gharama ya kuziendesha (Operation costs).

Baada ya utangulizi huu, tunaomba kurudi kwenye mada kuu ‘Siri ya Mahakama Ya Kadhi Yafichuka' ili ijulikane kuwa Mungu pekee ndiye mwenye siri, na si wanadamu.

Siri ya Mahakama ya Kadhi:

1. Kwamba, baada ya kelele za muda mrefu za Waislamu kudai kuwa Serikali inawaonea, na haiwapi fursa za elimu kwa usawa, Serikali ya Awamu ya tatu (Benjamin Mkapa), aliwapatia bure majengo ya kilichokuwa Chuo cha Tanesco – Morogoro, ambapo Waislamu walikifanya kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu Tanzania.

2. Kwamba kwa sasa wahitimu wengi wa Chuo Kikuu hiki wapo mitaani bila ajira (hasa waliosomea ‘Elimu Ahera'), na mlango pekee wa kuwapatia ajira serikalini ni kwa kuanzisha MAHAKAMA ZA KADHI, na ambapo kila Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa maelfu ya hawa ‘wenzetu katika imani' wataajiriwa.

3. Kwamba utafika wakati ambapo ‘wenzetu katika imani' wataamua, ama kupeleka mashauri yao ya ndoa/mirathi kwenye Mahakama za Serikali (ambazo wataziita ni "Mahakama za Makafri") au kwenye Mahakama za Kadhi.

4. Kwamba popote pale penye Mahakama ya Mwanzo (kwenye Kata, Tarafa au Mahakama za Wilaya na Mikoa Tanzania), LAZIMA Kadhi awepo pia. Hii inamaanisha kuwa, hata kama Kijiji/Kata au Tarafa haina muislamu hata mmoja (na jambo hali hii lipo maeneo mengi Tanzania Bara), lakini almradi ipo Mahakama ya Serikali mahali hapo lazima Kadhi ataajiriwa kukaa mahali hapo kwa gharama ya serikali, kwa nchi ya ‘TANZANIA ISIYO NA DINI'.

5. Kwamba Gharama za Kadhi kwenye haya maeneo (mishahara na marupurupu mengineyo) ni za Serikali ya Tanzania. Maana yake, Serikali itakusanya Kodi za Waislamu, Wakristo na Wasio na dini ili kulipa mishahara ya Makadhi wa Dini moja tu (Islam) – kwa sababu inatambuliwa na Katiba ya Tanzania.

HITIMISHO:

1. Kwa sasa Hayupo Mtanzania mwenye imani na wanaoitwa ‘MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI', kwa kuzingatia historia yao, na jinsi wanavyopotosha umma kwa minajili ya kuwafurahisha wakubwa zao waliowateua. Kawaida ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kuuwasha moto, lakini ukeshakolea hukaa pembeni kwa kisingizio kuwa ‘Ushauri wangu haukueleweka vizuri'.

Ndiyo maana Tunamtahadharisha Ndugu George Masajo (Mwanasheria wa Serikali wa sasa) asiwashe moto wa kuliteketeza taifa la Tanzania na ambao siyo rahisi kuja kuzimika hata baada ya kizazi cha nne kijacho pale machafuko ya UDINI kila kona yakishaanza Tanzania.

2. Rais Mh. Dr. Jakaya Kikwete, kilinde kiapo chako kwa Katiba kwa sababu yatosha sasa kuona unaendelea kuisigina Katiba iliyoweka Tanzania isiyo na dini kuwa taifa la mfano kwa umoja, uhuru, amani na utulivu hapa Afrika. Yatosha kuona mauaji ya maaskofu, mapdri, wachungaji na mashekhe kumwagiwa tindikali.

3. Tunawashauri Wabunge, waachane kabisa na mtego wa CCM wa kujipatia kura kwa gharama ya damu za Watanzania. Ni mtego kwa Wabunge wanaotaka kudumisha madaraka yao kwa kura za Waislamu mwaka huu 2015, hao ndio watajipendekeza kuunga mkono mswada huu wa hatari.

Tanzania ni zaidi ya madaraka / au cheo cha Rais/Mbunge au Mwanasheria Mkuu. Tanzania si jalala la kufanyia majaribiio ya mfumo ambao utatugawa mapande mawili. Wapo watu wanashabikia jambo hili kwa kuwa watafaidika kwa hizi ajira za mfumo wa Mahakama ya Kadhi.

Wapo wanaotolea mifano ya Uganda au Kenya lakini wanasahau hizi ni nchi zinakuja kujifunza kwetu namna ya kujenga umoja wa kitaifa. Waziri Mkuu (Mh. Mizengo Pinda) hata kwa ziara yake Uarabuni, hajaweza kubainisha kama ipo nchi aliyotembelea mwaka jana 2014 yenye mfano wa amani, mshikamano, usawa wa kijinsia kama Tanzania pamoja na kuwepo kwa Mahakama za Kadhi lukuki huko Uarabuni.

Tujikumbushe: Ombi la Kwanza la kupatiwa Chuo Kikuu cha Kiislamu lilifanikiwa (Awamu ya 3), Ombi la Pili la Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba (Awamu ya 4), na hatujui Ombi la Tatu la "Sharia za Kiislamu kwenye Katiba" litamuangukia rais wa Awamu ipi.

Uzoefu ni kuwa Ombi moja la Waislamu huzaa ombi linalofuata kwa mtiririko wake.

Mwisho, Tunaungana na nia njema ya Jukwaa la Wakristo na Wadau wengine, wanaopendekeza Mahakama za Kadhi endapo zikianzishwa kikatiba zijiendeshe 100% kwa gharama ya Waislamu wenyewe. Mungu Ibariki Tanzania iendelee kuwa nchi isiyoegemea Dini au Sera za Udini.
 
proisra

Umeandika meeengi kama huna ubongo vile. Sema mahakama ya kadhi ianzishwe ila ijigharamie yenyewe ingetosha. Ila ni kwanini ijigharamie yenyewe na inatoa huduma kwa wananchi? Ushani tibua na akili yako ndogo.
 
Last edited by a moderator:
SIRI YA MAHAKAMA YA KADHI YAFICHUKA

1. Kwamba, baada ya kelele za muda mrefu za Waislamu kudai kuwa Serikali inawaonea, na haiwapi fursa za elimu kwa usawa, Serikali ya Awamu ya tatu (Benjamin Mkapa), aliwapatia bure majengo ya kilichokuwa Chuo cha Tanesco – Morogoro, ambapo Waislamu walikifanya kuwa Chuo
Kikuu cha Kiislamu Tanzania.


Hapo penye wekundu, una uhakika na unachokisema? Msiwe mnapenda kuwaza na kusema msivovijua? hebu nenda Mtaa wa Bibi Titi pale karibu na shule ya Mnazi Mmoja , angalia kuna mitambo ya Tanesco imejengwa pale! uliza kile kiwanja kilikuwa cha nani? ukipata jibu njoo uhororoje hapa!
 
Umeandika meeengi kama huna ubongo vile. Sema mahakama ya kadhi ianzishwe ila ijigharamie yenyewe ingetosha. Ila ni kwanini ijigharamie yenyewe na inatoa huduma kwa wananchi? Ushani tibua na akili yako ndogo.

Inatoa huduma gani..??
 
Pia wataaguza Alhamis na Ijumaa iwe siku ya mapumziko.
Zanzibar walianza kudai kimoja kimoja, na sasa nchi ishasilimishwa.
 
Hapo penye wekundu, una uhakika na unachokisema? Msiwe mnapenda kuwaza na kusema msivovijua? hebu nenda Mtaa wa Bibi Titi pale karibu na shule ya Mnazi Mmoja , angalia kuna mitambo ya Tanesco imejengwa pale! uliza kile kiwanja kilikuwa cha nani? ukipata jibu njoo uhororoje hapa!

Waislam walipewa BUREEE na Mkapa na hata SHETANI ANAJUA HILO.
 
mbona mkataba wa MOU unawapa fursa wakristo kupewa pesa kuchangia maendeleo yao kama AFYA ,ELIMU KUKOPESHANA kushamiri kwa makanisa hata kama sehemu hakuna wakiristo.pesa za MOU mnazopewa kodi mnalipa peke yenu?
 
wakuu embu nisaidieni formulation ya mahakama zetu sisi tusiokuwa dini rasmi(kwa kipare tunawaita VA NGOMA). Maana baada ya uchaguzi nina imani tutaunda tume nyingine kama ya kina warioba kwa ajili ya kutafuta maoni.
 
Inamaana, sisi tunywe konyagi, beer, na vinywaji vingine na pia kule kwenye kitimoto itolewe kodi ndiyo ije wakapewe waendeshee mahakama yao??

kwa kodi ya kitimoto, na beer, na kama wata rasimisha wale wenzetu kulipia kodi biashara ya kuuza miili yao??
 
Kwani hao si Watanzania???kwani hawalipi Kodi?? Kwani kila kitu tunacholipia Kodi lazima tufaidi sote?? Kwani ni lazima sote tufuate sheria za mahakama hiyo?? Je kuna Nchi ambazo zina mahakama za aina hiyo??je kuna matatizo yemejitokeza??je kuna utafiti umefanyika Juu ya suala hili????
 
bado ni ujinga serikali ndiyo inatakiwa kutoa maelezo siyo nyie.
 
Back
Top Bottom