Siri ya Lowassa yavuja

Siri ya Lowassa yavuja

Kweli ccm imechoka mnoo.. Lowasa na ukawa kiboko Yao. Nijuavyo Mimi sifa za uteuzi WA waziri mkuu sifa moja wapo lazima awe mbunge WA kuchaguliwa na wananchi. Sasa sumaye agombei ubunge kokote kwa hyo Hana sifa ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu kama ukawa itapewa ridhaa na wananchi. Sasa ccm sera zao zimegeuka kuwa pango na shimo la uongo,fitina,majungu,uzadiki na siasa maji taka. Wananchi atudanganyiki mwaka huu n mabadiliko na Lowasa mpaka magogoni.
 
Ili mtu awe waziri mkuu, ni sharti awe mbunge wa kuchaguliwa na wananchi. mbunge wa kuteuliwa na rais au chama viti maalum, hawezi kuteuliwa kuwa waziri mkuu. sumaye hagombei ubunge katika jimbo lolote, kwa hiyo, hatarajii kuwa mbunge wa kuchaguliwa mwaka huu; hivyo basi, sumaye hawezi kuteuliwa kuwa waziri mkuu. msukuma arudi shule akasome. aache blaablaa!
 
Mwaka huu ccm mtaomba majii...maana magoli yamewazidia.
 
hata hajui anachokiongea , huwezi kuwa waziri mkuu kama si mbunge wa jimbo. sasa sumaye kagombea ubunge kwenye jimbo ? katiba inazuia mbunge wa kuteuliwa na raisi kushika wadhifa wa waziri mkuu ila wizara nyingine aweza kushika. kama msukuma hujui mambo kaa kimya unatudhalilisha std seven wenzako.

Siyo kosa lake hizo ni hasira za kuzikosa ambulance za mzee alizopewa na kuzigeuza zake kumbe zilitakiwa ziwafikie wananchi.
 
Ccm mwaka huu bye bye....! Lowasa ndo hbr ya mjini
 
WE LIKES LOWASSA HATA MSEME NINI CHAGUO LETU NDIO HUYO!
HATUBADILIKI NGO,NGO,NGO!!
**LOWASSA 2015~2025**
ii
sasa si utoe hoja why you like lowassa! kila kitu kina upande wa pili..ndio maana mnaitwa wapumbavu/malofa.
 
huyu msukuma hajitambui kamwe. akifanikiwa kuwa mbunge atakuwa mbunge bomu kuliko hata lusinde.
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amesema ana siri kubwa ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia Chadema na kupewa nafasi ya kugombea urais akiwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Msukuma alisema yeye alikuwa miongoni mwa timu ya watu 11 iliyokuwa na mkakati wa kumsaidia Lowassa kushinda katika kura za maoni za kuomba kuteuliwa kugombea urais ndani ya CCM, ambapo alikatwa na kuhamia Chadema.

Alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu uliofanyika juzi kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nyankumbu.

Alidai kuwa baada ya Lowassa kukatwa wananchi wengi walianza kusema ana mpango wa kuhamia Chadema ili kumfuata, lakini alisisitiza kwamba hana mpango huo kwani ana siri nzito kuhusu mgombea huyo wa Ukawa.

Msukuma ambaye ni mgombea wa CCM Jimbo la Geita Vijijini, alidai kuwa hadi sasa mpango wa Lowassa kama atashinda kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kumteua Waziri Mkuu mstaafu aliyehamia Chadema, Frederick Sumaye kuwa waziri mkuu katika serikali yake.

Alisema mpango wake mwingine ni kumteua Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuwa Waziri wa Fedha, vyeo ambavyo alidai ni kugawiana kutokana na ukanda ili waunde Serikali.

“Mimi nilizunguka nchi nzima na Lowassa, nikiwa miongoni mwa timu ya watu 11 iliyokuwa ikimpigia debe ashinde, najua mipango yake mingi, namsubiri aje Geita aropoke hapo ndiyo atamjua Msukuma ni nani, nitatoa siri zake zote,” alisema Msukuma huku akishangiliwa na wananchi.

Aliwataka wananchi kumpuuza mgombea huyo wa Ukawa na badala yake wananchi waelekeze nguvu zao kumchagua mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli huku akisisitiza kuwa ni muda wa Kanda ya Ziwa kumtoa rais.
Matata

Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Mwanza kupitia Chadema, Henry Matata naye ametoboa siri baada ya kudai alijiunga na chama hicho akiwa pandikizi kutoka CCM na kwamba alichokipata kinatosha.

“Mimi nilikuwa pandikizi wa CCM ndani ya Chadema, baada ya kuona Mbowe natekeleza Ilani ya CCM katika kipindi changu cha Uongozi wakanifukuza,” alidai Matata.

Aliongeza kuwa akiwa Chadema amekaa humo na kujua matatizo na siri zote za chama hicho pamoja na matatizo yote ya Mbowe.

Hata hivyo, aliwataka wanachama wa CCM Wilaya ya Geita ambao bado wamegawanyika kutokana na makovu ya uchaguzi wa kura za maoni kuvunja makambi ili kujihakikishia ushindi katika jimbo hilo la Geita.

Mgombea

Mgombea ubunge wa Jimbo la Geita, Costantine Kanyasu alisema akichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Geita atahakikisha makapi ya mawe yanayosadikika kuwa na dhahabu katika Mgodi wa Geita maarufu kwa jina la Magwangala yanatolewa kwa wananchi.

Alisema kilio kikubwa cha wananchi wa Geita hasa vijana wachimbaji wadogo ni Magwangala na kuahidi kama atapata ridhaa hiyo atapambana kufa au kupona ili kuhakikisha mawe hayo yanatolewa kama inavyofanyika katika migodi ya Kahama na Nyamongo.

Kanyasu alisema kero kubwa kwa wananchi wa Geita ni tatizo la maji ambalo limekuwepo kwa kipindi kirefu na kudai kwamba kabla ya kuomba ridhaa alikuwa anafuatilia tatizo hilo ambalo limeanza kutatuliwa na Serikali.

“Mimi mkinipa nafasi hii nitahakikisha stendi inakuwa ya kisasa..ni muda mrefu stendi yetu mmekuwa mkiilalamikia…mvua zikinyesha yanakuwa majaluba ya mpunga..nawaahidi nitahakikisha tunakuwa na stendi inayoendana na hadhi ya mkoa wetu,” alisema.

Aliongeza kuwa atahakikisha Kituo cha Afya Nyankumbu kinapatiwa gari la wagonjwa ili kuondoa kero ya kutegemea gari la Hospitali ya Wilaya ya Geita hali inayochagia vifo kwa wagonjwa.

Aliwaomba wananchi wamchague yeye pamoja na mgombea urais, Dk. Magufuli ambaye anaamini kwa uchapakazi wake Geita itabadilika na kuwa mkoa unaofanana na rasilimali iliyopo.

Dk Slaa

Katika hatua nyingine, aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Same, Magu na Misenyi, Mhandisi Elias Maarugu (70) amemlipua aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuwa si msafi wala mwadilifu akisema asiwadanganye Watanzania.

Alidai kuwa Dk. Slaa hana tofauti na dikiteta na kwamba alikuwa mzigo kwa chama hivyo wananchi wapuuze kauli zake ambazo amezitoa hivi karibuni kuhusu Lowassa.

“Slaa si mwadilifu. Ameendesha chama kwa mabavu kwa sababu alikuwa hatoi nafasi kwa wanachama kujitetea ambayo ni haki ya mtu kufanya hivyo,” alidai Maarugu wakati akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Bukoba na kuongeza;

“Alinisingizia kuwa nimehongwa fedha na kunitaka nitoe majibu ndani ya wiki mbili nilifanya hivyo lakini alinijibu kwamba suala langu linashughulikiwa na sekretarieti ya chama kumbe ulikuwa uongo mtupu. Ni muongo na hana uadilifu wowote,” alidai.

Chanzo: Jambo leo


Msukuma anadai kwamba EL akichaguliwa, ataunda serikali iliojaa watu wa ukanda wa kaskazini. Labda nimuelewe kwamba anapinga swala la Ukanda. Ni vyema.

Lakini aliendelea kusema kwamba "sasa ni wakati wa kanda ya ziwa kutoa rais" wa JMT.

Naona anajikanyaga mwenyewe!
 
Hata msemeje hapa lowasa tu. Halafu huyo msukuma kma ni sir anaxo bas zitakuwa ni siri nzuri za lowas kuwa raisi lkn kma ni siri chafu hata yy hapaswi kumpigia debe mtu yoote kwan atakuwa ameshiriki uchafu
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amesema ana siri kubwa ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia Chadema na kupewa nafasi ya kugombea urais akiwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).



Msukuma ambaye ni mgombea wa CCM Jimbo la Geita Vijijini, alidai kuwa hadi sasa mpango wa Lowassa kama atashinda kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kumteua Waziri Mkuu mstaafu aliyehamia Chadema, Frederick Sumaye kuwa waziri mkuu katika serikali yake.

Alisema mpango wake mwingine ni kumteua Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuwa Waziri wa Fedha, vyeo ambavyo alidai ni kugawiana kutokana na ukanda ili waunde Serikali.



Aliwataka wananchi kumpuuza mgombea huyo wa Ukawa na badala yake wananchi waelekeze nguvu zao kumchagua mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli huku akisisitiza kuwa ni muda wa Kanda ya Ziwa kumtoa rais.
Matata



Chanzo: Jambo leo

Sasa kwa hizi paragraphs mbili za katikati mbona anajichanganya? Anamsema Lowasa kwa Ukanda bado yeye anapigia chapua ukanda. Pathetic
 
Sumaye alikuwa hajajiunga ukawa wakati huo, kwa hiyo ni uongo kusema Lowassa alikuwa na mpango wa kumteua Sumaye kuwa waziri mkuu. Hata hivyo mbona awamu ya 3 waziri mkuu na waziri wa fedha walitokea ukanda huo?
 
Kanyasu huyu aliyeuza miti nakuigeuza wilaya ya ngara kuwa jangwa..!??kanyasu huyu mtembea na wake za watu..huyu kanyasu mpaka sasa mo mkuu wa wilaya ya ngara,ila ni kati ya majizi na waaribudu nmewai kuona..!!polen wana geita..!!
 
Msukuma ana shida.... yaani hana la kumsema el.... anatafuta kukubalika ndani ya ccm asionekane msaliti....eti Sumaye awe waziri mkuu... kwa katiba ipi....
 
Back
Top Bottom