Siri ya Lowassa yavuja

Siri ya Lowassa yavuja

Mtu anagombea urais anajinadi kwa kufuta posho za wafanyakazi. Hivi Magufuli hajui posho za safari semina mafunzo n.k ziko kisheria? Hili sio jambo la kujivunia hata kidogo. Au autuambie hizo posho za mawaziri ni tatizo kwenye serikali hii ya kwao tutamwelewa. Halafu raisi anajinadi kwa sera . Hivi kweli kupunguza au kuondoa kabisa posho za wafanyakazi ni sera au kipaumbele cha Rais ajeye 2015? Magufuli anatakiwa ajue tofauti ya utendaji wa serikali na miongozo yake na sera ya nchi. Huwezi kujinadi kwa vitu vidogo namna hii halafu ukaniambia wewe una uwezo wa kuwa Rais.

Sasa kama utafuta posho za mawaziri ina maana sisi wafanyakzi wa kawaida utatufanyaje? Yaani hata tukisaifri kikazi tujitegemee posho ?
 
Bashe nae kuunguruma soon madudu ya lowassa! hiyo ndio ccm
 
hata hajui anachokiongea , huwezi kuwa waziri mkuu kama si mbunge wa jimbo. sasa sumaye kagombea ubunge kwenye jimbo ? katiba inazuia mbunge wa kuteuliwa na raisi kushika wadhifa wa waziri mkuu ila wizara nyingine aweza kushika. kama msukuma hujui mambo kaa kimya unatudhalilisha std seven wenzako.
 
Shiiiiti! Kumbe nimesoma gazeti la Habari Leo😡😱 Hata hivyo Msukuma lazima alopoke hivyo kwani Chopa ashanyang'anywa tayari.
 
Siri siri gani,
si mseme hizo siri zenu au mnataka tuziseme;

Lowassa ndiye chaguo la watanzania, hata mkeo
na wanao nao watampigia kura, kama uongo tupinge.
 
Angalau simsupport Lowassa na kundi lake, lakini hawa jamaa walichokuwa wanaongea hakina msingi kabisa. Iweje leo

Lowassa amteue Sumaye kuwa waziri mkuu wakati waziri mkuu anatokana na ubunge, na ukiangalia Sumaye yeye

agombei ubunge. Hii inaonekana hawa viongozi hata kilichoandikiwa kwenye katiba hawakijui. Kingine kwa kurekebisha tu

Sumaye yupo NCCR Mageuzi na siyo Chadema.
 
Back
Top Bottom