Jadilini yote, Toeni pongezi zote lakin hii tamko la Zitto halitakuwa na maana endapo tu hataitisha press conference ili jamii ya nje ambayo idadi kubwa iweze kujua ukweli huu, Pia Zitto uache lugha tata katika maelezo yako kwan unazidi kuchanganya watu na kuwapa binamu zako wa damu CCM cha kupigia propaganda mfano unaposema sijui "malengo ya mtu mmoja yasifanywe kuwa ni ya taasisi"
Pia cha mwisho uache vita yako kwa Ben Saanane kwan unajishushia hadhi mwenyewe kwan Ben si mjinga kama unavyofikiri ww, kwani unapotumia masalia kumchafua usifikiri taarifa hazimfikii,
All in all Bravo Zitto kwa kuonesha uthubutu.
anaogopa kuuawa endapo atakiri chezea mbowe wewe
Nisome vizuri mkuu.Mkuu nadhani unafurahia sana utengano, Kamanda kesha sema na inaeleweka sasa wewe hukatazwi kutoa maoni lakini siyo ya kuendeleza utengano, after all mwenyewe ndio kasema hivyo na hatakiwi kulazimishwa kusema tunavyofikiri.
Vizuri sana Zitto kwa ufafanuzi mzuri.Gazeti la Mtanzania siku hizi limekuwa kama gagulo la kuandika uchochezi,chuki,fitina,majungu na uzandiki dhidi ya Chadema hasa likimuandama Dr Slaa.
Sijui kwanini Hussein Bashe anaruhusu gazeti hili kuandika upuuzi kama huu.
Again Thankyou Zitto you have made my day.
Mh.zitto haya magazeti yetu na vyombo mbalimbali vya serekali vinaendeshwa na skendo/mawazo ya watu humu jamii forums
1)TCRA ilivifungia vyombo kadhaa vya habari baada ya thread kuanzishwa humu
2)gazeti hilo la mtanzania na magazeti mengine yanaendeshwa na habari wanazoziona huku
3)hata kukamatwa kwa lwakatare walipata hiyo clip hukuhuku jamii forums
Kwaiyo nadhani wasikupe shida sana na pili washauri wabadilike kama nchi inaendeshwa na mawazo ya watu hapa jf inasikitisha
Kikubwa mheshimiwa zitto nakushauri hama chadema na utengeneze chama chenye malengo ya kumkomboa mtanzania
Chadema imeshaoza sana .........Take this from me
[MENTION]ben sanane[/MENTION]salamaaMara nyingi sana hapa jukwaani ben amekuwa akimsakama zitto kwa tuhuma za kuhujumu chama lakini zitto kwa busara zake hataki kabisa kulumbana na ben.. Hii ndio sifa ya kiongozi na tofauti kubwa iliyopo kati ya zitto na ben
Ndugu yangu Zitto napenda kukushukuru kwa kujibu gazeti hilo la Mtanzania. Maneno uliyoyaandika hapa haina unafiki hata mmoja. Haya maneno ni maneno ya busara na maneno ya Mungu. Sitokusahau siku ile uliposimama pale Revolution square pale mlimani na kuonyesha msimamo wako. Ninaamimi sana katika msimamo na hautatuangusha sisi vijana wenzako katika kupigania haki na ukweli katika nchi hii, hata kama ina uchungu. Ninakuombea kwa Mungu akubariki utujengee chama chetu cha chadema. Najua watu wengi wamo humo wanatumiwa na CCM ili CDM kife. Angalia walivyoiuwa CUF kwa kutumia mbinu zile zile wanazotumia sasa. Mungu akubariki mheshimiwa.