Siri ya kutokukosa hela tena (Kutokufulia) hii hapa. Soma hutajuta...

Mkuu mada yako imenigusa sana.
Watanzania wengi wamekosa hii elimu.
Utakuta kijana amepata kazi ya mshahara laki 7 then ghafla anaanza maisha ya showoff kabla hata hajajiwekea misingi mizuri.
Mwisho wa siku kazi mkataba ukiisha hata saving yoyote anarudi kuwa tegemezi hata kulipia kodi ya chumba hawezi tena anaanza kuuza vitanda alivyokuwa analalia ili apate hela ya kula.
Elimu ya uchumi binafsi ipp katika kiwango kibaya sana hii nchi
 
Watoto hufanya kile wanachokipenda ila mtu mzima kabarikiwa uwezo wa kuujua uhalisia, kubuni mipango na kuifata.

Kuna kitu muhimu ambacho hakikwepeki mimi na wewe tunapotumia pesa, si kingine bali ni "HESABU", yawezekana ni wengi tu tunazijua hesabu lakini hapa ni kuhusu kuzitumia.

Tunajiingiza katika matarizo, mawazo, umaskini, mikopo kwa sababu hatuna wito wa kufanya hesabu kabla ya kufanya miamala.

Si ajabu mtu akawa una uwezo wa kumsomesha mwanao shule za milioni 2 lakini misaada kwa ndugu ikaongezeka na hivyo kulazimika kumeta mtoto wako saint kayumba sababu ulipuuza hesabu.

Si ajabu kijana anaepokea laki 9 ya mshahara kwenda kukopa benki milioni 10 anunue gari ila akalipaki kwasababu mshahara umepungua kwajili ya makato mapya sababu alipuuza hesabu, Haiingii akilini utapata pumziko maridhawa la kuendesha gari bila stress kwa hii mbinu.

Mtu masikini wa mawazo yeye anaponunua kitu anachofikiria kinachompa tiketi ya kununua kitu ni "nina uwezo wa kununua hiki kitu (hata kwa mkopo) huku wakisahau kama wataweza kuvitunza bila stress.

Angalia hali yako jabla ya kufanya maamuzi ya fedha na sio baada ya kufanya muamala, hesabu ni hizi za kawaida tu za shule ya msingi, usiwe nyuma bali uwe mbele ya hizi hesabu.

Una miaka 30 lakini hali yako ni mbaya vile vile tangu uajiriwe ukiwa na miaka 25 na pengine ikawa mbaya zaidi, kila unaporejesha deni baada ya miaka mingi ya mateso ya marejesho unarudia tena kukopa ili ununue gari au ufanye anasa, nakwambia ya kwamba hadi uote mvi utamtafuta mchawi kumbe ni wewe.

Unaponunua vitu ambavyo huvihitaji ama havina umuhimu sana katika maisha yako basi jua kuna siku utashindwa kununua vitu muhimu utavyohitaji. hesabu nuepesi hii.

Anza kujengga tabia ya kuchukia kutumia pesa, jifunze kutengeneza pesa hata kama ni kutunza hazina, wewe kunja noti yako mara mbili irudishe mfukoni uone ndani ya mwaka umeweza kutunza ngapi, kwa maana hii achana na matumizi yasiyo na umuhimu/

Usiishi maisha ya mboga saba kwenye kipato cha tembele

Usiishi maisha ya kufurahisha wengine au kufanya ujulikane unazo, wewe una ex wako mshamalizana ya nini kujaza lita za ziada kwenye gari ili tu ujipitishe anaposhindaga akuone?
Unazungumziaje wale watu waliofuata km ulivyosema au shauri,lkn bado wana hali ngumu kiuchumi?.
 
dudu jeupe,
Aisee nimekupata kaka na kW huu ujumbe naamin in njia mojawapo yangu Mimi kuanza mapambano upya baada y mawazo y mda mref kW namna gan nawez kutengeneza hela,be blessed brother
 
Kwa hiyo unajiona maisha umeishayapatia kwa kuwa na nyumba na flat screen. Hizo ni liabilities hazikuingiziu chochote
wewe jamaa unajielewa sana.
Umefuata nyayo zangu hata mimi nilikuwa naishi hvyo.
Watu walikuwa wananicheka sina vitu vya ndani kumbe nilikuwa navunga tu kama ningeamua ningetumia mshahara mmoja tu.
Sasa hivi ninavyokwambia nimejenga my dream house na bonge la flat Screen limening'inia ukutani.
Endelea na hiyo spirit utafika mbali
 
Watoto hufanya kile wanachokipenda ila mtu mzima kabarikiwa uwezo wa kuujua uhalisia, kubuni mipango na kuifata.

Kuna kitu muhimu ambacho hakikwepeki mimi na wewe tunapotumia pesa, si kingine bali ni "HESABU", yawezekana ni wengi tu tunazijua hesabu lakini hapa ni kuhusu kuzitumia.

Tunajiingiza katika matarizo, mawazo, umaskini, mikopo kwa sababu hatuna wito wa kufanya hesabu kabla ya kufanya miamala.

Si ajabu mtu akawa una uwezo wa kumsomesha mwanao shule za milioni 2 lakini misaada kwa ndugu ikaongezeka na hivyo kulazimika kumeta mtoto wako saint kayumba sababu ulipuuza hesabu.

Si ajabu kijana anaepokea laki 9 ya mshahara kwenda kukopa benki milioni 10 anunue gari ila akalipaki kwasababu mshahara umepungua kwajili ya makato mapya sababu alipuuza hesabu, Haiingii akilini utapata pumziko maridhawa la kuendesha gari bila stress kwa hii mbinu.

Mtu masikini wa mawazo yeye anaponunua kitu anachofikiria kinachompa tiketi ya kununua kitu ni "nina uwezo wa kununua hiki kitu (hata kwa mkopo) huku wakisahau kama wataweza kuvitunza bila stress.

Angalia hali yako jabla ya kufanya maamuzi ya fedha na sio baada ya kufanya muamala, hesabu ni hizi za kawaida tu za shule ya msingi, usiwe nyuma bali uwe mbele ya hizi hesabu.

Una miaka 30 lakini hali yako ni mbaya vile vile tangu uajiriwe ukiwa na miaka 25 na pengine ikawa mbaya zaidi, kila unaporejesha deni baada ya miaka mingi ya mateso ya marejesho unarudia tena kukopa ili ununue gari au ufanye anasa, nakwambia ya kwamba hadi uote mvi utamtafuta mchawi kumbe ni wewe.

Unaponunua vitu ambavyo huvihitaji ama havina umuhimu sana katika maisha yako basi jua kuna siku utashindwa kununua vitu muhimu utavyohitaji. hesabu nuepesi hii.

Anza kujengga tabia ya kuchukia kutumia pesa, jifunze kutengeneza pesa hata kama ni kutunza hazina, wewe kunja noti yako mara mbili irudishe mfukoni uone ndani ya mwaka umeweza kutunza ngapi, kwa maana hii achana na matumizi yasiyo na umuhimu/

Usiishi maisha ya mboga saba kwenye kipato cha tembele

Usiishi maisha ya kufurahisha wengine au kufanya ujulikane unazo, wewe una ex wako mshamalizana ya nini kujaza lita za ziada kwenye gari ili tu ujipitishe anaposhindaga akuone?
Ahahahaha mkubwa naona umeamua kutuchana ..
 
Tunaongeza liability badala ya assets
Me nimeajiriwa mwaka huu mwanzoni watu wananishangaa the way ninavyoishi Wengine wananicheka ninavyojibana
Sina TV wananiona mshamba japo kuwa hizo TV na takataka zake naweza nunua in in one month salary so nawacheki wanavyoshindana kununua mapambo ya ndani mwenzao huyo this month naanza kulipia kiwanja
Inshort vitu vya muhimu ninavyo Ila makorokoro ya kuuzia sura siyataki

Nahisi labda baada ya kunywa madini ya kiyosakiView attachment 1566775
Kweli tuko tofauti..

Nilianza ajira nikiwa na miaka 24 (2014) Ila sijawahi fikiria kujenga ndio mafanikio na Wala usiwazi kujenga.

Kwanini tusifungue biashara tukamiliki mahisa, hivi kujenga ni mafanikio nayo?

#YNWA
 
Hakuna tajiri bahili ubahili ni hulka ya masikini asiye na kitu siri ya utajiri haipo kwenye ubahili bali ipo kwenye kutengeneza pesa nyingi na kuwa na vyanzo vingi vya mapato acheni kudanganya watu maskini wengi ndo hutumia pesa kwa ubahili na kujinyima sana hakuna tajiri bahili wengi ndo huongoza kwenye kufanya masherehe, kumili magari makali, nyumba nzuri, watoto kusoma shule nzuri, kusaidia etcetc in short wao ndo huongoza kwa expenditures. Kamwe usimshauri masikini ubahili. Ubahili hauleti utajiri, ubahili unaleta kuridhika na uvivu ubahili humfanya mtu asipende kufanya kazi.
Shauri watu kufanya kazi kwa bidii na kuongeza vyanzo vya mapato pesa iwe mingi expenditures ziwepo lakini pesa iwe iwe inaingia zaidi usishauri watu ubahili
Umeongea sahihi Ila ngoja Nikupe mfano tu;

Ubahili ni nguzo ya utajiri kwa uliyezaliwa umasikinini ..
Kuna jamaa mmoja ni yatima ye alikuwa kwa kudra za Mungu na sasa ana ajira.

Aliajiriwa 2015 serikalini.

Akaanza kuwa bahili.
Ubahili wake umemfanya awe na nunue mashamba makubwaa, maana hutunza pesa mwaka mzima halafu December (likizo) huenda kununua mashamba.

Alivyofika Eka 100 aliamua kupanda parachichi, kaanza 2020.

Pia kwa ubahili wake, ameweza kupanda eneo kubwaa mara MOJA.

Anaamini sanaa kwenye kilimo na anakomaa nacho.

Hana source nyengine ya pesa na yeye anakwambia INVESTMENT IS BETTER THEN BUSINESS.

POINT YANGU NI KWAMBA:-
Wakati una source MOJA, ukiwa unatengeneza ya pili UBAHILI MUHIMU na ni nguzo ya kujenga hiyo ya pili.

#
wewe jamaa unajielewa sana.
Umefuata nyayo zangu hata mimi nilikuwa naishi hvyo.
Watu walikuwa wananicheka sina vitu vya ndani kumbe nilikuwa navunga tu kama ningeamua ningetumia mshahara mmoja tu.
Sasa hivi ninavyokwambia nimejenga my dream house na bonge la flat Screen limening'inia ukutani.
Endelea na hiyo spirit utafika mbali.

Mnakuaje mabahili halafu mnajenga liabilities?

Maana nyumba ya kuishi ni liability, itahitaji maji, umeme, matengenezo na ....
Nafikiria tuwe mabahiri huku tukitengeneza cash generating assets.

Tujenge nyumba ZA KUPANGISHA
Tununue mashamba ya kupanda mfano miti, matunda ili tuuze hizo products.
Tununue hisa...

Unakuaje bahili halafu at the end unaishia kumiliki malii zisizozalisha?

#YNWA
 
Huu ulimwengu umejawa na mashauri kibao, ila kama Mungu alikupangia utaishi hivi, hata hakuna mwanadamu anaweza weka nguvu yake kubadilisha
Mungu akupangii uwe na madeni benki.
Mungu akupangii upate pesa ya mshahara leo kesho iwe imeisha.
Mungu akupangii uishi maisha ya madeni kwasababu mshahara hautoshi.

Ni akili zako binafsi.

Tafuta Financial intelligency.

#YNWA
 
Umeongea sahihi Ila ngoja Nikupe mfano tu;

Ubahili ni nguzo ya utajiri kwa uliyezaliwa umasikinini ..
Kuna jamaa mmoja ni yatima ye alikuwa kwa kudra za Mungu na sasa ana ajira.

Aliajiriwa 2015 serikalini.

Akaanza kuwa bahili.
Ubahili wake umemfanya awe na nunue mashamba makubwaa, maana hutunza pesa mwaka mzima halafu December (likizo) huenda kununua mashamba.

Alivyofika Eka 100 aliamua kupanda parachichi, kaanza 2020.

Pia kwa ubahili wake, ameweza kupanda eneo kubwaa mara MOJA.

Anaamini sanaa kwenye kilimo na anakomaa nacho.

Hana source nyengine ya pesa na yeye anakwambia INVESTMENT IS BETTER THEN BUSINESS.

POINT YANGU NI KWAMBA:-
Wakati una source MOJA, ukiwa unatengeneza ya pili UBAHILI MUHIMU na ni nguzo ya kujenga hiyo ya pili.

#

Mnakuaje mabahili halafu mnajenga liabilities?

Maana nyumba ya kuishi ni liability, itahitaji maji, umeme, matengenezo na ....
Nafikiria tuwe mabahiri huku tukitengeneza cash generating assets.

Tujenge nyumba ZA KUPANGISHA
Tununue mashamba ya kupanda mfano miti, matunda ili tuuze hizo products.
Tununue hisa...

Unakuaje bahili halafu at the end unaishia kumiliki malii zisizozalisha?

#YNWA
Mkuu huwezi kupata utulivu wa kufikiria maendeleo kama upo kwenye nyumba ya kupanga huku unafikiria muda wowote mwenye nyumba atakuja kukugongea mlango kudai kodi yake.
Ili kuondoa huo usumbufu ndio huwa tunaamua kukomaa kujenga nyumba ya kuishi then baada ya hapo ndio utaamua ujenge nyumba nyingine ya kupangisha au biashara nyingine.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo unajiona maisha umeishayapatia kwa kuwa na nyumba na flat screen. Hizo ni liabilities hazikuingiziu chochote
Bado maisha sijayapatia ila naamini nimejiwekea msingi mzuri.
Huwezi kupata utulivu wa kufocus maendeleo kama upo kwenye nyumba ya kupanga na unadaiwa kodi.

Kuishi kwenye nyumba yako kuna heshima yake.
Acha kuishi kwa theories kuwa real utakuja kubuma ujute.
Biashara huwa zina msimu sio kila siku zitakuletea pesa tu,kuna wakati huwa zinagoma na mwenye nyumba anataka kodi yake hapo ndipo utakapojua kuwa hujui.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Umeongea sahihi Ila ngoja Nikupe mfano tu;

Ubahili ni nguzo ya utajiri kwa uliyezaliwa umasikinini ..
Kuna jamaa mmoja ni yatima ye alikuwa kwa kudra za Mungu na sasa ana ajira.

Aliajiriwa 2015 serikalini.

Akaanza kuwa bahili.
Ubahili wake umemfanya awe na nunue mashamba makubwaa, maana hutunza pesa mwaka mzima halafu December (likizo) huenda kununua mashamba.

Alivyofika Eka 100 aliamua kupanda parachichi, kaanza 2020.

Pia kwa ubahili wake, ameweza kupanda eneo kubwaa mara MOJA.

Anaamini sanaa kwenye kilimo na anakomaa nacho.

Hana source nyengine ya pesa na yeye anakwambia INVESTMENT IS BETTER THEN BUSINESS.

POINT YANGU NI KWAMBA:-
Wakati una source MOJA, ukiwa unatengeneza ya pili UBAHILI MUHIMU na ni nguzo ya kujenga hiyo ya pili.

#YNWA
Mkuu uko sahihi.
Lakini hata waliozaliwa kwenye utajiri pia ni wabahili tena zaidi ya maskini.
Mfano angalia wakina Mo dewji wanavyowafanyisha watu kazi ngumu kwenye viwanda vyao kisha wanawalipa elfu 6 kwa siku.
Huu sio ubahili?

Kwa mfano sisi watu wa kawaida wenye mishahara jamaa yako au rafiki yako akikusikitikia shida kumpa elfu 50 au laki ni kitu cha kawaida.
Au kukaa bar na kumnunulia kinywaji mtu mliyejuana siku hiyo hiyo ni kawaida.
Ila kwa matajiri hawatoagi hela kama hizi japo akaunti zao zinasoma bilioni kadhaa.
Huo ndio ubahili wenyewe sasa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nimekosa Mkopo bank kwa Kutokuwa na nyumba ama kwa hakika bora ujenge Nyumba utafungua milango.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mkuu uko sahihi.
Lakini hata waliozaliwa kwenye utajiri pia ni wabahili tena zaidi ya maskini.
Mfano angalia wakina Mo dewji wanavyowafanyisha watu kazi ngumu kwenye viwanda vyao kisha wanawalipa elfu 6 kwa siku.
Huu sio ubahili?
Kwa mfano sisi watu wa kawaida wenye mishahara jamaa yako au rafiki yako akikusikitikia shida kumpa elfu 50 au laki ni kitu cha kawaida.
Au kukaa bar na kumnunulia kinywaji mtu mliyejuana siku hiyo hiyo ni kawaida.
Ila kwa matajiri hawatoagi hela kama hizi japo akaunti zao zinasoma bilioni kadhaa.
Huo ndio ubahili wenyewe sasa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Unamjua Gulam Dewji..
Baba wa Mohamed Dewji mwenye METL.

Yule mdingi ana nyumba amepanga Kati ya upanga au masaki.

Maana pia ana mdogo ake (fazal Dewji@baba mdogo wa Mohamed Dewji) sasa Kati yao mmoja yupo upanga mwengine masaki na wotee wamepanga.

Diamond platinumz pamoja na utajiri wotee alionao Ila kapanga kwa madale.

Kumiliki nyumba ya kuishi SI UTAJIRI.

Kabla ya kumiliki nyumba na/au gari hebu tengeneza MIFEREJI YA PESA KWANZA.

Kwa hiyo wewe unataka kujidanganya kwamba akina Mo kwa vile wamepanga upanga ndio hawana nyumba?au unadhani hawajawahi kujenga?acha kufuata mkumbo mkuu utaingia chaka.
Unamtolea mfano Gulam Dewji au Mo Dewji kwa mfano akifukuzwa kwenye nyumba ya kupanga,akiuza godowns zake za kutunzia magari hawezi kujenga nyumba?au akifukuzwa fenicha zake ataenda kuzihifadhi kwenye godowns zake,je wewe mwenzangu na mie utafanyaje?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nar

Narudia kwenye comment ya juu kabisa.

"Tengeneza secondary/other sources of incomes"

Mimi binafsi naishi mkoani Ila Nina nyumba ya kupangisha dar@kinondoni.

Kwa mwezi nakusanya si haba.

Nataka kutengeneza nyengine G.Mboto (Bro kaniambia kasikia nyumba inauzwa pale G.Mboto).
Nikuchukua hii nikaifanyia matengenezo nitatoboa (nyumba za ule mtaa hazina miaka zaidi ya 6)

Nimeajiriwa 2014 Ila nimepanga..!!

Kwasasa mkatengeneza MIFEREJI kwanza.

Hiyo MIFEREJI ndio ijenge nyumba za kuishi na inunue gari na sio mshahara wangu.

Lengo langu ikifike wakati niachane na mshahara ukae benki miaka

Yaani najaza standing order, mshahara ukitoka benki wapeleke saving account ukatengeneze return.

Achana na hizo liabilities, tengeneza kwanza asset za kukuingizia pesa, halafu hizo assets ndio zizalishe matumizi ya hizo liabilities

Nikupe mfano:- hiyo nyumba YAKO what if ingekuwa uswahilini mfano Mwananyamala na kule chumba 50k

Tuseme nyumba ina vyumba 6.
Inamaana wewe kila mwezi una laki 3.

Ungechukua hizo laki 3, ukajichanga na madili + mishahara, unatengeneza nyengine uswahilini kwengine.

Then baada ya miaka 5 - 10 hivi una nyumba 3 tuseme total vyumba 20.

Kwahiyo kila mwezi unaingiza Mil 1.

Halafu sasa ndio ujenge YAKO ya kuishi..!!!

#YNWA
 
Back
Top Bottom