Siri ya kutoka kimaisha hii hapa

TuntemekeSanga

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
1,346
862
MAFANIKIO YAKO YAPO MIKONONI MWAKO, USIPITE BILA KUISOMA HII

1461332052509.jpg


Nikiwa kitandani kwangu alfajiri ya leo nikawa natafakari na kujiuliza "ni nini siri ya mafanikio, nifanye nini nifanikiwe?" majibu ya kufanikiwa nikayapata mulemule room kwangu.
Feni ikaniambia niwe cool nisikurupuke, dali ikaniambia "fikiri juu
zaidi", madirisha yakaniambia "tizama nje uone fursa zilizopo
ulimwenguni", saa ya ukutani ikaniambia "kila sekunde ina thamani sana katika maisha, muda ni mali."

Kioo kikaniambia "Jitizame na ujiamini kabla hujafanya jambo". Kalenda ikaniambia, "mwaka wako wa mafanikio ndio huu." Mlango ukaniambia "Sukuma kwa nguvu kwa ajili ya malengo yako." Choo kikaniambia "flash tabia zako zote mbaya zinazokufanya uendelee kuwa chini."
Na nilipokiona kitabu cha dini kikacheka na kuniambia "Nisome mimi kwa ajili ya kuenenda njia zilizonyoka, ili mwovu shetani asikupate."

Nikaamka nikiwa na nguvu mpya pamoja na matumaini mapya!
Mwenyezi Mungu, abariki kazi halali za mikono yetu, sisi ni vichwa na wala si mikia. Mafanikio ni kama barabara kwani haina mwisho bali viungio vya njia mpya.

Kama ujumbe huu umekutia moyo, comment neno lolote kama ishara ya kushukuru. Tunawatakia siku njema!
 
Mwanzo niliangalia jina nilifikiria Mrisho Mpoto aka Mjomba
Hahaha,Ubarikiwe sana mkuu
Kuna Ujumbe mzito sana ndani yake ujumbe wako huo mfupi wenye kubeba maisha ya sie vijana wenye kujitambua.
Kama ningekuwa mwalim,basi ningeipeleka hii post shule ili wanafunzi wachangie wameelewa nini ndani yake ili iwe kama assignment kwao ya kutambua wanakoelekea.
Maana ni ujumbe na burudani,aisee kwenye choo nimecheka mpaka basi
 
Back
Top Bottom