Siri ya kuishi miaka mingi ya Kheri Duniani

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,894
SIRI YA KUISHI MIAKA MINGI YA KHERI DUNIANI!

Anaandika, Robert Heriel
Baba.

Tena Sisi tuliowatoto wa Baba asiyeonekana, tukawa Baba wanaoonekana ili tuweze kufanya yaliyo mapenzi ya Baba yetu aliyemkuu Yule asiyeoonekana na kamwe ambaye hatokuja aonekane. Basi nisikilizeni Wanangu.
Kwa maana maneno yangu ni Haki, tena Yana Hekima, nayo yafanye sheria katika maisha yako. Hivyo ndivyo namna utakavyoweza kufanikiwa katika njia yako, utakapojawa na wingi wa miaka yenye Kheri.

Niite Taikon kutoka nyota ya Tibeli, Baba yako.

Nimekufundisha katika njia ya hekima, katika mapito yaliyomema nimekuongoza.
Haya andika;

1. Tumia Akili
Maisha ni kuishi, ukitaka kuishi maisha màrefu basi jifunze kuishi Kwa furaha na Amani, na haki na upendo.
Na ili uweze kuishi Kwa hayo yote basi jifunze kutumia Akili kisha usimuamini mtu yeyote. Na Ili uweze kutumia Akili basi jifunze Kwa yanayokuzunguka Kwa kuona au kusikia. Hasahasa mazingira na viumbe vya asili. Kwa maana ukijifunza Kwa yanayokuzunguka ukayajua utaweza kuyatawala, kuyatumia na kutatua changamoto zinazokukabili.
Jifunze kutumia Akili ili uweze kuishi Kwa Amani, furaha na Upendo.
Akili itakusaidia kuishi, hivyo lazima uisadie nayo kuishi.

Na ili usimuamini mtu au yeyote basi itakupasa ufikie hatua kitu hicho haukijui vizuri. Huwezi kuamini au kukiamini mtu/kitu usichokijua au kuelewa. Naam ndio maana wahenga walitangulia kusema Trust No one. Yaani usiamini chochote usichokijua Kwa 100%

2. Usidhulumu/ Tenda Haki.
Usiidhulumu Nafsi yako au Nafsi ya mtu mwingine.
Usichukue stahiki ya mtu mwingine.
Upe mwili wako haki zake, kamwe usiudhulumu.
Usichukue Mke au mume WA mtu. Utakufa au kuuawa.
Usiibe Mali za watu. Kaa mbali za vitu vya watu.

Namna Bora ya kuishi maisha ya furaha ni kutenda haki na kujipa haki katika maisha yako. Furaha msingi wake umejengwa hapo.

3. Kuwa na Kiasi.
Maisha ni Balance.
Kama vile uonavyo usiku na mchana, juu na chini, kulia na kushoto basi hakikisha unajua kuweka mambo Kwa uwiano Sawa. Kuwa na kiasi Kwa Jambo lolote ulifanyalo.
Usiwe na haki kupita kiasi usije ukafa mapema kabla ya wakati wako, na usijekuwa mwovu kupita kiasi usijeukafa mapema.
Usiwe na furaha kupita kiasi usije ukakufuru na wala usijekawa na huzuni kupita kiasi ukaona maisha hayana maana.

Kula Kwa kiasi, vaa Kwa kiasi, Sali Kwa kiasi, fanya lolote Kwa kiasi.
Huo ndio ubinadamu.

4. Fanya Kazi.
Haiwezekani mtu asiye na kazi akaishi miaka mingi, haiwezekaniki. Mwili WA binadamu usipofanya kazi ubongo unaassume mwili umekufa. Hivyo magonjwa huanza kurandaranda kuumaliza mwili.
Usikubali kukaa vivihivi. Fanya kazi. KAZI ndio maisha. KAZI ndio Utu wako.
Maisha bila ya kazi hayafai kitu. Utadharaulika na hautahesabika kuwa ni kitu.
Mwanangu kazi ndio itakayoamua utaishi maisha ya namna gani uwapo Duniani.

Fanya kazi kadiri uwezavyo hata ufikishe miaka 100 fanya kazi.
Aina za kazi
1. Kazi za Akili
2. KAZI za mwili na nguvu
3. KAZI za kiroho na kiimani
4. KAZI za hisia na mihemko
5. KAZI mchanganyiko wa Aina hapo juu.

Ukiwa mzee fanya kazi za Akili zisizohitahitaji kutumia nguvu, kama kushauri na kuelimisha kizazi kichanga kinachokua.

5. Pumzika.
Kila kitu Duniani kinahitaji mapumziko.
Usifanye vitu pasipo akili wala pasipo Akili.
Hakikisha unaupa mwili na Akili, hisia na roho yako pumziko.
Kupumzika husaidia mwili na Akili kujiongeza nguvu zaidi na zaidi.
Seli mpya za mwili huhitaji mwili unaopumzika vizuri ili ufanye kazi Kwa usahihi.

Umri wa kupumzika Kwa masaa
Umri miaka 0- 2 masaa 14- 18
Umri miaka 3- 10 masaa 10- 13
Umri miaka 11-22 masaa 8 - 12
Umri miaka 23 - 35 masaa 6 - 7
Umri miaka 36 - 60 masaa 5 - 6
Umri miaka. 61 - 80. Masaa 5
Umri miaka 81 - 100. Masaa 2 - 4

Kikawaida mwili WA binadamu kadiri mtu anavyokua ndivyo usingizi unavyozidi Kupungua. Hii kama mtu hataweza kujitawala anaweza kujikuta anapata athari za usahaulifu kwenye UTU uzima.
Mara nyingi mtu asiyelala vizuri anapata tatizo la Loss of Memory.

Muda wa kupumzika unaendana na matumizi ya umri wa Mtu katika Kazi na uzalishaji katika jamii.

6. Mlo na unywaji
Kula vizuri na kunywa maji ya kunywa vizuri.
Bahati nzuri vyakula vya asili ni BEI rahisi.

7. Ibada
Maisha Kwa ujumla ni ibada. Kila ufanyalo ni ibada. Ikiwa ni Jambo Baya basi unafanya ibada ya kishetani, na ikiwa unafanya Jambo jema basi unafanya ibada Kwa Mungu.
Ndio maana kila mara nasemaga, kila mtu ni mtumishi wa Mungu Kwa maana kila KAZI ufanyayo iliyohalali ambayo haidhuru watu, haikudhuru wewe na wala haidhuru mazingira hiyo kazi ni KAZI ya Mungu na ni KAZI halali.
Aina za Ibada
i. Ibada ya Mafunzo.
Hii ni watoto wakipelekwa kanisani au msikitini kusoma elimu ya kiroho. Hiyo ni ibada.
Kwenda msikitini kupewa mawaidha au kanisani kusikiliza mahubiri, hiyo ni ibada ya kujifunza.
Mtu habarikiwi Kwa kwenda kanisani au msikitini kufanya ibada ya kujifunza Bali anabarikiwa akifanya Yale aliyofundishwa huko Kanisani au msikitini au mahali popote kwenye ibada.

ii. Ibada ya Shukrani
Kutoa Sadaka Kwa wahitaji, mayatima, wajane, ombaomba na wote wasiojiweza hiyo ni ibada ya Shukrani.
Kulisha viumbe vya Mungu kama Ndege kupitia mashamba yako Kwa kuacha masazo ya kile ulichokivuna hiyo ni Sadaka.
Kutoa zaka Kwa watumishi wa Mungu kama Wachungaji, masheikhe, mapadri, Makuhani, n.k hiyo ni ibada ya Shukrani.

Kuimba kanisani au Kusafisha nyumba za Ibada kama misikiti au makanisa Kwa kujitolea hiyo ni Sadaka na ibada ya Shukrani.

Kukarimu wageni na kuwalisha wasiojiweza ambao hawana uwezo wa kukurudishia Kwa lolote. Sio ualike watu wenye Majina makubwa au wenye pesa Kama Sisi kina Taikon wenye mapesa yetu alafu useme umetoa Sadaka, huko ni kujidanganya.
Alika watoto machokora, ombaomba huko ndiko kukarimu wageni, HAO ndio wageni haswa.

Kutoa sehemu ya ulichobarikiwa bure mfano karama, kipaji, au Huduma bila kutegemea malipo Kwa Nia ya manufaa hiyo ni ibada ya Shukrani.

iii. Ibada ya Toba.
Tumezaliwa na wazazi ambao hawakuwa Wakamilifu. Huenda walifanya maasi na kubeba laana. Lazima ufanye ibada ya toba ili kuondoa na Kusafisha njia yako ambayo huenda iliharibiwa na Watangulizi wako. Hiyo inaitwa Spiritual Diplomacy. Kurejesha mahusiano mazuri na miungu unayoiamini.

Pia Sisi sio wakamilifu, hivyo muda na saa yoyote tunakosea, hivyo toba ni sehemu ya ibada katika kurejesha mahusiano Bora na miungu. Spiritual Diplomacy.
Huwezi ishi maisha ya Kheri ikiwa mahusiano yako ya kiroho yana migogoro na mafarakano.

Ibada ya toba itaendana sambamba na wewe kusamehe wanaokukosea lakini pia kuna makosa lazima uwajibike Kwa maana hiyo ndio Haki.
Na sio kila kosa unapaswa umsamehe binadamu mwenzako anapokukosea, yapo makosa lazima umuwajibishe aliyekukosea.

Haya nipumzike sasa,

Ni Yule Mtibeli kutoka Nyota ya Tibeli. Baba yako.

Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ninaishukuru serikali maana ninekuwa mchangiaji wa 5 kuchangia huu uzi
 
Wasi sahau kuishi porini kama nyani kwa mjin humu hizo fomla kazi bure moshi wa magari viwanda.madem.kula beer nk
 
Umeeleweka kwa kiasi chake changamoto za maisha ni nying snaa na nyingi zipo kukutoa kwenye uwepo
 
Katika mda wa kupumzika ni jambo la kheri sana ili usipoteze kumbukumbu
 
Back
Top Bottom