Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,029
Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima

IMEBAINIKA kuwa, wajumbe wa kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kupitia mikataba ya madini, wana sifa zenye kila dalili ya shaka kuwemo katika kamati hiyo.

Kwamba baadhi ya wajumbe hao, walihusika katika utiaji saini mkataba wa Buzwagi na mmoja wa wajumbe wa kamati ni rafiki mkubwa wa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni jambo linalotia shaka kuhusu kuteuliwa kwao katika kamati hiyo.

Hayo yalibainishwa jana katika kongamano la wanavyuo la kuadhimisha Siku ya Wanafunzi Duniani, lililohudhuriwa na wasomi wa kada mbalimbali, wakiwemo madaktari, wanasheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, wanaharakati na wanasiasa wa kambi ya upinzani.

Kongomano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa DDC mkabala na Mlimani City, karibu na kilipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.

Wachangiaji wengi katika mdahalo huo, walieleza kuwa kamati hiyo iliyoundwa na Rais Kikwete ni kiini macho cha kuwaghilibu Watanzania, ili wasiendelee kuhoji kuhusu utata unaodaiwa kuwepo kwenye mikataba ya madini, kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wote hawana sifa za kuunda kamati hiyo.

Wa kwanza kuelezea udhaifu wa kamati hiyo, alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibroad Slaa, ambaye alidai kwamba, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ni swahiba mkubwa wa Waziri Karamagi ambaye hawezi kumtia matatani rafiki yake (Karamagi).

Dk. Slaa alimtaja mjumbe huyo kuwa ni Peter Machunde, kutoka Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), ambaye mwaka jana alialikwa bungeni na Karamagi na akatambulishwa mbele ya Bunge kuwa ni rafiki yake.

Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Slaa aliyenukuu kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard) cha Agosti 7, mwaka 2006, alisema hata kualikwa kwa Machunde bungeni kuna kila dalili za shaka kuwa alikuja kufanya moja ya kazi za Karamagi.

"Mwaka huo, Karamagi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, alimtambulisha bungeni Machunde kama rafiki yake, leo hii anatambulishwa kwenye kamati ya akina Zitto.

"Hawa watu walikuja kufanya nini bungeni? Tunafuatilia walikuja kufanya nini… hatutaki kamati kiinimacho, kamati hii haitokani na Zitto peke yake, mwishoni mwa wiki ijayo tutatoa taarifa nyingine juu ya hiyo kamati na ndiyo maana tunasema hakuna wa kumfunga paka kengele kwa sababu wote wanafahamiana," alisema Dk. Slaa.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.

"Tuna historia ya ‘ku-miss use' hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?" alisema.

Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.

Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mang'enya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.

"Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto… Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii… ripoti haijatolewa," alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.

"Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.

Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.

Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.

Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.

"Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati… Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina ‘term of reference?" alihoji Lissu.

Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.

Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.

"Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina ‘judicial power', mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi," alisema Lissu.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, alisisitiza msimamo wake kuwa amekubali uteuzi huo na kwamba atahakikisha anaweka maslahi ya taifa mbele.

Alisema sekta ya madini inaonyesha kuwa sekta inayokuwa, lakini mchango wake kwa pato la taifa hauongezeki.

Baadhi ya watu wengine mashuhuri waliozungumza katika mdahalo huo na kuunga mkono kuwepo kwa shaka dhidi ya wajumbe wa kamati hiyo, ni Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye pia alisisitiza mshikamano wa wasomi na kutumia usomi wao ili kuleta maendeleo.

Wengine ni mwanahabari mkongwe, Makwaiya wa Kuhenga, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Elimu ya Juu, Susan Lyimo na Dk. Azaveli Lwaitama wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao wote walisisitiza nguvu ya pamoja katika kuleta mapambano ya kifikra.

Rais Kikwete alitangaza kamati hiyo hivi karibuni na itaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine kwenye kamati hiyo itakayofanya kazi kwa miezi mitatu ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) ambaye ni Mbunge wa Kyela, Ezekiel Maige kutoka Jimbo la Msalala (CCM), Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Pia wamo Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
 
hata mimi nilijawa na wasiwasi na hii kamati, ila washiriki wake sikuwaelewa kwa undani kama sasa hivi.
 
haha ccm mpoooooooo haya njooni muanze zibwaga pumba zenu kama kawa...mwadanganya watz na kamati zenu ndo yale yale at end kamati imetumia milioni mia moja..ripoti yafichwa uvunguni
ndo maana nawafagilia wapinzani as hawana kazi nyingine zaidi ya kuchokonoa udhaifu wa chama tawala kwa ajili ya maendeleo ya nchi!!m speakin kwa dunia nzima n not only tz!
 
haha ccm mpoooooooo haya njooni muanze zibwaga pumba zenu

Wakuu hebu muwe mnafikiri kabla ya kuandika hapa kwenye uwanja wa kiamtaifa, I mean what is this?

Yaani kwa mawazo yako ya-kipumba, akiesma Lisu na makwaiya wa kuhenga ndio ukweli? If that is the case kwa nini tuna mahakama? Na kwa nini tupeleke kesi za mfisadi kwenye sheria iwapo Lisu akisema basi ni ukweli?

I mean how low can we go kwenye hii forum na pumba? Yaani kweli mkuu unategemea kuna m-JF atakayeandika pumba zaidi ya hizi zako?
 
..fmes,

..watu wanapenda issues ziwe dramatized!ndio wanafurahi!if you know what i mean!

..pumba lazima ziwepo!usichoke!bila pumba hakuna mchele,bali mpunga!na mpunga hauliki!
 
Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima

IMEBAINIKA kuwa, wajumbe wa kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kupitia mikataba ya madini, wana sifa zenye kila dalili ya shaka kuwemo katika kamati hiyo.................

Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Slaa aliyenukuu kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard) cha Agosti 7, mwaka 2006, alisema hata kualikwa kwa Machunde bungeni kuna kila dalili za shaka kuwa alikuja kufanya moja ya kazi za Karamagi..............

“Mwaka huo, Karamagi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, alimtambulisha bungeni Machunde kama rafiki yake, leo hii anatambulishwa kwenye kamati ya akina Zitto.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema .......
“Tuna historia ya ‘ku-miss use’ hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?” alisema.“Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto… Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii… ripoti haijatolewa,” alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Hivi jamani hii kamati kumbe inaitwa "Kamati ya Zitto"? Naomba kuelimishwa kama ndivyo.
 
Nadhani ni kwa sababu ya aliyoyaibua Zitto Bungeni kuhusiana na mkataba wa Buzwagi. Sidhani kama kamati hii ingeundwa bila ya hayo.
 
Kwa mtu anayefikiria vizuri,hawa jamaa wameelezea mambo ya msingi sana na kuwafungua macho watu nikiwa mmojawapo.Kikubwa nadhani wanakamati wanatakiwa wawe clean na kwamba hawajahusika na mikataba iliyoleta utata.Hili la bwana mapesa na msimamo wake kuhusu iptl nadhani linajulikana wazi.Huyo mama anayebadili majina pia anajulikana umafia wake.Huyo rafiki wa karamagi ndiyo hivyo tena mpaka tarehe aliyoalikwa bungeni imeanikwa.Hakuna haja ya mahakama kuprove hapo.
Jambo lingine la msingi ni kwamba labda ingekuwa tume ya bunge ndiyo ingelikuwa na nguvu na utekelezaji wake ni tofauti na hizi tume anazounda raisi.Ni nyingi mna na ripoti zikitoka zinafungiwa kabatini.Lakini upande wa bunge ni tofauti kwani report na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa zinasomwa mbele ya wabunge na siyo mambo ya kufungia kabatini.Hivyo hata mimi sioni kama hii kamati ina impact.
 
haha ccm mpoooooooo haya njooni muanze zibwaga pumba zenu

Wakuu hebu muwe mnafikiri kabla ya kuandika hapa kwenye uwanja wa kiamtaifa, I mean what is this?

Yaani kwa mawazo yako ya-kipumba, akiesma Lisu na makwaiya wa kuhenga ndio ukweli? If that is the case kwa nini tuna mahakama? Na kwa nini tupeleke kesi za mfisadi kwenye sheria iwapo Lisu akisema basi ni ukweli?

I mean how low can we go kwenye hii forum na pumba? Yaani kweli mkuu unategemea kuna m-JF atakayeandika pumba zaidi ya hizi zako?

Hata kama ni pumba.....atleast wa Tz tumefunguliwa macho abt it na lisemwalo lipo na haiwezekani hao watu wakasema hayo mambo kama hayapo
 
haha ccm mpoooooooo haya njooni muanze zibwaga pumba zenu

Wakuu hebu muwe mnafikiri kabla ya kuandika hapa kwenye uwanja wa kiamtaifa, I mean what is this?

Yaani kwa mawazo yako ya-kipumba, akiesma Lisu na makwaiya wa kuhenga ndio ukweli? If that is the case kwa nini tuna mahakama? Na kwa nini tupeleke kesi za mfisadi kwenye sheria iwapo Lisu akisema basi ni ukweli?

I mean how low can we go kwenye hii forum na pumba? Yaani kweli mkuu unategemea kuna m-JF atakayeandika pumba zaidi ya hizi zako?

Wewe unajifanya smart sana lakini hamna lolote ungekuwa smart ungeona vitu vilivyo wazi kabisa. hata yule mtoto wa form one aliyembana koo babu yako kule kaskazini ni smart kuliko wewe.
 
Hebu wana JF kuweni siriaz!!!! Yaani hapo napo mshaibua issue????

Kamati haijaundwa heeeee, mbona hawataki kuunda kamati, imeundwa ooooh wamejichagua! PUMBAFFFF!!!!!!!!!!

Hebu mwacheni zito akafanze kazi, kama aliweza bungeni mpaka wakamdili atashindwaje huko??? Hivi hamjui sakata la Zito lilitokana na hoja ya kutaka kuanzishwa kamati ya kufuatilia Buzwagi contract? Sasa kapewa yote, mwataka nini!!! mmekuwa kama paka shume!

Hebu subirini acheni hoja za kitoto na kukurupuka!!!
 
In any committee what you expect is check and balance. What i believe Zitto is obligated to provide check and balance to this committee, his job will be to analyze all facts provided, and consult other mambers concern the facts .

What i don't understand is why Upinzani rise ant-trust for this committee which includes different people. Zitto is our red flag, if any non sense happen i believe Zitto will rise his red flag. That is check and balance. Nothing will be published if there is no agreements between members, unless otherwise CCM wamnunue Zitto which is possible due to Tanzanian works ethics.
 
Mtanganyika, unakumbuka Ndesamburo kwenye Kamati ya Mengi/Malima... aliponyanyua "bendera nyekundu"... walimuambiaje?
 
In any committee what you expect is check and balance. What i believe Zitto is obligated to provide check and balance to this committee, his job will be to analyze all facts provided, and consult other mambers concern the facts .

What i don't understand is why Upinzani rise ant-trust for this committee which includes different people. Zitto is our red flag, if any non sense happen i believe Zitto will rise his red flag. That is check and balance. Nothing will be published if there is no agreements between members, unless otherwise CCM wamnunue Zitto which is possible due to Tanzanian works ethics.

Mh.Mtanganyika sio kuwa Wapinzani hawapendi kuwepo kwa kamati.Ila wajumbe waliomo ndani sio waadilifu na katika mzunguko huo mjumbe anayeaminika ni Zitto pekeyake.Sasa wewe unafikiri atakuwa na nguvu ya kuwapinga hao wajumbe wote pale ambapo hawatakubaliana?Mwanakijiji kakupa mfano wa Dr. Slaa kwenye kamati ya Malima.
 
Hebu wana JF kuweni siriaz!!!! Yaani hapo napo mshaibua issue????

Kamati haijaundwa heeeee, mbona hawataki kuunda kamati, imeundwa ooooh wamejichagua! PUMBAFFFF!!!!!!!!!!

Hebu mwacheni zito akafanze kazi, kama aliweza bungeni mpaka wakamdili atashindwaje huko??? Hivi hamjui sakata la Zito lilitokana na hoja ya kutaka kuanzishwa kamati ya kufuatilia Buzwagi contract? Sasa kapewa yote, mwataka nini!!! mmekuwa kama paka shume!

Hebu subirini acheni hoja za kitoto na kukurupuka!!!

Bokassa being serious is to show how serious you can analyse issues. Ule muda wa kudanganyana umekwisha, hata ukiangalia maandishi hapo juu unaona sasa kweli wapinzani nao wanaweza kuchambua mambo, siyo zile zama za zidumu fikra za---, rejea yale ambayo hapo juu Bob Mkandara ameandika; in short we are having a real democracy in practice.
 
Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima

IMEBAINIKA kuwa, wajumbe wa kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kupitia mikataba ya madini, wana sifa zenye kila dalili ya shaka kuwemo katika kamati hiyo.
Kwamba baadhi ya wajumbe hao, walihusika katika utiaji saini mkataba wa Buzwagi na mmoja wa wajumbe wa kamati ni rafiki mkubwa wa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni jambo linalotia shaka kuhusu kuteuliwa kwao katika kamati hiyo.

Hayo yalibainishwa jana katika kongamano la wanavyuo la kuadhimisha Siku ya Wanafunzi Duniani, lililohudhuriwa na wasomi wa kada mbalimbali, wakiwemo madaktari, wanasheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, wanaharakati na wanasiasa wa kambi ya upinzani.

Kongomano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa DDC mkabala na Mlimani City, karibu na kilipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.

Wachangiaji wengi katika mdahalo huo, walieleza kuwa kamati hiyo iliyoundwa na Rais Kikwete ni kiini macho cha kuwaghilibu Watanzania, ili wasiendelee kuhoji kuhusu utata unaodaiwa kuwepo kwenye mikataba ya madini, kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wote hawana sifa za kuunda kamati hiyo.

Wa kwanza kuelezea udhaifu wa kamati hiyo, alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibroad Slaa, ambaye alidai kwamba, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ni swahiba mkubwa wa Waziri Karamagi ambaye hawezi kumtia matatani rafiki yake (Karamagi).

Dk. Slaa alimtaja mjumbe huyo kuwa ni Peter Machunde, kutoka Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), ambaye mwaka jana alialikwa bungeni na Karamagi na akatambulishwa mbele ya Bunge kuwa ni rafiki yake.

Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Slaa aliyenukuu kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard) cha Agosti 7, mwaka 2006, alisema hata kualikwa kwa Machunde bungeni kuna kila dalili za shaka kuwa alikuja kufanya moja ya kazi za Karamagi.

“Mwaka huo, Karamagi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, alimtambulisha bungeni Machunde kama rafiki yake, leo hii anatambulishwa kwenye kamati ya akina Zitto.

“Hawa watu walikuja kufanya nini bungeni? Tunafuatilia walikuja kufanya nini… hatutaki kamati kiinimacho, kamati hii haitokani na Zitto peke yake, mwishoni mwa wiki ijayo tutatoa taarifa nyingine juu ya hiyo kamati na ndiyo maana tunasema hakuna wa kumfunga paka kengele kwa sababu wote wanafahamiana,” alisema Dk. Slaa.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.

“Tuna historia ya ‘ku-miss use’ hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?” alisema.

Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.

Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mang’enya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.

“Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto… Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii… ripoti haijatolewa,” alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.

“Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.

Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.

Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.

Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.

“Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati… Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina ‘term of reference?” alihoji Lissu.

Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.

Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.

“Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina ‘judicial power’, mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi,” alisema Lissu.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, alisisitiza msimamo wake kuwa amekubali uteuzi huo na kwamba atahakikisha anaweka maslahi ya taifa mbele.

Alisema sekta ya madini inaonyesha kuwa sekta inayokuwa, lakini mchango wake kwa pato la taifa hauongezeki.

Baadhi ya watu wengine mashuhuri waliozungumza katika mdahalo huo na kuunga mkono kuwepo kwa shaka dhidi ya wajumbe wa kamati hiyo, ni Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye pia alisisitiza mshikamano wa wasomi na kutumia usomi wao ili kuleta maendeleo.

Wengine ni mwanahabari mkongwe, Makwaiya wa Kuhenga, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Elimu ya Juu, Susan Lyimo na Dk. Azaveli Lwaitama wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao wote walisisitiza nguvu ya pamoja katika kuleta mapambano ya kifikra.

Rais Kikwete alitangaza kamati hiyo hivi karibuni na itaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine kwenye kamati hiyo itakayofanya kazi kwa miezi mitatu ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) ambaye ni Mbunge wa Kyela, Ezekiel Maige kutoka Jimbo la Msalala (CCM), Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Pia wamo Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Yaani hapa Kikwete ndio inabidi aangalie sana washauri wake (kama akitaka niamini kuwa alishauriwa kuunda hii Kamati).

Huwezi kuunda kamati ya kuchunguza na kuboresha mikataba ya madini ukamweka mama Kejo, Machunde and the company. Kikwete anazidi kuthibitisha kuwa yeye naye ni player katika this Buzwagi skendo!

yangu macho na masikio!
 
"Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina ‘judicial power', mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi," alisema Lissu.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kamati ya bunge na tume ya rais!!!!

Kamati ya Bunge mara nyingi ni ya Uchunguzi, pale ambapo wanaona serikali haijafanya vizuri au ina walakini mahali na ukweli haueleweki in most cases inafanya kazi kwa hali ya "Reactive".

Tume ya Serikali/Rais inaundwa mara nyingi kiutendaji, kuishauri serikali, nini ifanye shughuli fulani au jambo fulani liende vizuri, mara nyingi yale yanayotokana na tume hizi hayatangazwi kwa sababu maoni ya tume mara nyingine sio msimamo wa serikali,,, mfano tume ya kurekebisha mishahara huwezi kuweka mambo hewani kabla serikali haijachambua maana inawezakuleta dhana mbaya,,, kumbukeni maoni mengine ya kamati ni ya kinatharia zaidi, kwa mfano lipa wafanyakazi kima cha chini cha 500,000/- yet practically serikali ikiangalia inaona haiwezekani.

Mara nyingi tume ya rais inakuwa kwenye hali ya "Proactive" Kuangalia mambo ya baadaye kuangalia mambo mazito na maoni ya kamati yanajadiliwa baadaye na Serikali na serikali ina haki ya kuchukua mawili, matatu au manne kutekeleza na mengine kuacha, hii sio tatizo hata kidogo...

Wale waliowahi kuwa mameneja wanaweza kutoa mchango wao hapa, hivi kila unaloletewa na sub-ordinate wako ni lazima ulitekeleze kama lilivyo? je ni mangapi yanayoletwa kwako ni ambition ambazo huwezi achieve?

Mpaka sasa naona watu wanachanganya haya mambo mawili ndio maana mijadala inaendelea bila sababu...

Kuwepo watu wa wizara ndani ya tume ya Rais, ni pamoja na kutoa realistic, achievables things,,, mfano Zitto anaweza akasema tugawane 50% 50% faida ya madini, mshauri wa wizara atasema lakini kumbuka sisi sio shareholders, we are depending on Taxes, na taxes tulizoweka ndizo ambazo ziko duniani kote,,, then they we will say why don't we be one of shareholders of the mining company, mtu wa wizara atasema lakini kumbuka mtaji ni mkubwa na hatuwezi ku-raise, ndio maana tushindwa hata kuongeza mitaji kwenye makampuni mengine mengi (mfano ATCL), then atasema basi tutumie ardhi yetu kama mtaji,,, then watarudi kwani thamani yake ni kiasi gani etc. etc. eventually they reach a consesus na maslahi ya taifa yatkuwa yamezingatiwa na objective, goals, recommendations zinakuwa zina-u-reality

Tume kuwa na Upinzani, CCM, serikali, etc... is good thing, wote wakiwa upande mmmoja won't proceduce realistic results, ofcourse the outcome results may not be expected result and thus how business goes anyway.

As I said before kumbukeni tume hii sio ya kumchunguza Karamagi, na kuwepo rafiki yake is not a problem at all!!! tume hii ni kuangalia tutawezaje kufaidika na madini baadaye...

So acheni kufanya mchezo wa kurudi rudi nyuma!!!

Kwa Maana nyingine hii composition ya tume ya rais kama ingekuwa kwa nia ya ku-serve as Kamati ya Bunge, kweli kungekuwa kuna tatizo kubwa sana....otherwise it is very fine as it is now, with the purpose of its composition
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kamati ya bunge na tume ya rais!!!!

Kamati ya Bunge mara nyingi ni ya Uchunguzi, pale ambapo wanaona serikali haijafanya vizuri au ina walakini mahali na ukweli haueleweki in most cases inafanya kazi kwa hali ya "Reactive".

....

Kwa Maana nyingine hii composition ya tume ya rais kama ingekuwa kwa nia ya ku-serve as Kamati ya Bunge, kweli kungekuwa kuna tatizo kubwa sana....otherwise it is very fine as it is now, with the purpose of its composition

Mhhh,

Baada ya hili kutoka kwa kilitime, nadhani sasa kilichosemwa mwanzoni kuwa huu ni usanii wa JK kimeanza kuonekana. Yaani hii tume inaundwa kufanya ambacho tume na kamati kama tano hivi zimekuwa zinaendelea kukifanya for the last five yrs only!
 
haha ccm mpoooooooo haya njooni muanze zibwaga pumba zenu

Wakuu hebu muwe mnafikiri kabla ya kuandika hapa kwenye uwanja wa kiamtaifa, I mean what is this?

Yaani kwa mawazo yako ya-kipumba, akiesma Lisu na makwaiya wa kuhenga ndio ukweli? If that is the case kwa nini tuna mahakama? Na kwa nini tupeleke kesi za mfisadi kwenye sheria iwapo Lisu akisema basi ni ukweli?

I mean how low can we go kwenye hii forum na pumba? Yaani kweli mkuu unategemea kuna m-JF atakayeandika pumba zaidi ya hizi zako?

Mzee hapa sijaelewa kama kweli umesoma vizuri sana.

Point zilizopo kwenye hiyo mada ni muhimu sana kuona kama kweli Muungwana yuko siliasi kweli na anachokifanya.

Mzee usikasirike sana angalia mambo haya mzee ni muhimu sana.

Halafu Mzee sina uhakika kama kweli umeandika wewe au wamekuingilia kwenye account yako.

Kuna CCM, kuna LISU na makwaiya hapa naomba unieleweshe kidogo sijapata connection.
 
Back
Top Bottom