Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima

IMEBAINIKA kuwa, wajumbe wa kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kupitia mikataba ya madini, wana sifa zenye kila dalili ya shaka kuwemo katika kamati hiyo.

Kwamba baadhi ya wajumbe hao, walihusika katika utiaji saini mkataba wa Buzwagi na mmoja wa wajumbe wa kamati ni rafiki mkubwa wa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni jambo linalotia shaka kuhusu kuteuliwa kwao katika kamati hiyo.

Hayo yalibainishwa jana katika kongamano la wanavyuo la kuadhimisha Siku ya Wanafunzi Duniani, lililohudhuriwa na wasomi wa kada mbalimbali, wakiwemo madaktari, wanasheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, wanaharakati na wanasiasa wa kambi ya upinzani.

Kongomano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa DDC mkabala na Mlimani City, karibu na kilipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.

Wachangiaji wengi katika mdahalo huo, walieleza kuwa kamati hiyo iliyoundwa na Rais Kikwete ni kiini macho cha kuwaghilibu Watanzania, ili wasiendelee kuhoji kuhusu utata unaodaiwa kuwepo kwenye mikataba ya madini, kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wote hawana sifa za kuunda kamati hiyo.

Wa kwanza kuelezea udhaifu wa kamati hiyo, alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibroad Slaa, ambaye alidai kwamba, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ni swahiba mkubwa wa Waziri Karamagi ambaye hawezi kumtia matatani rafiki yake (Karamagi).

Dk. Slaa alimtaja mjumbe huyo kuwa ni Peter Machunde, kutoka Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), ambaye mwaka jana alialikwa bungeni na Karamagi na akatambulishwa mbele ya Bunge kuwa ni rafiki yake.

Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Slaa aliyenukuu kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard) cha Agosti 7, mwaka 2006, alisema hata kualikwa kwa Machunde bungeni kuna kila dalili za shaka kuwa alikuja kufanya moja ya kazi za Karamagi.

"Mwaka huo, Karamagi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, alimtambulisha bungeni Machunde kama rafiki yake, leo hii anatambulishwa kwenye kamati ya akina Zitto.

"Hawa watu walikuja kufanya nini bungeni? Tunafuatilia walikuja kufanya nini&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; hatutaki kamati kiinimacho, kamati hii haitokani na Zitto peke yake, mwishoni mwa wiki ijayo tutatoa taarifa nyingine juu ya hiyo kamati na ndiyo maana tunasema hakuna wa kumfunga paka kengele kwa sababu wote wanafahamiana," alisema Dk. Slaa.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.

"Tuna historia ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ku-miss use' hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?" alisema.

Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.

Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mang'enya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.

"Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; ripoti haijatolewa," alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.

"Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.

Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.

Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.

Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.

"Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];term of reference?" alihoji Lissu.

Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.

Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.

"Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];judicial power', mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi," alisema Lissu.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, alisisitiza msimamo wake kuwa amekubali uteuzi huo na kwamba atahakikisha anaweka maslahi ya taifa mbele.

Alisema sekta ya madini inaonyesha kuwa sekta inayokuwa, lakini mchango wake kwa pato la taifa hauongezeki.

Baadhi ya watu wengine mashuhuri waliozungumza katika mdahalo huo na kuunga mkono kuwepo kwa shaka dhidi ya wajumbe wa kamati hiyo, ni Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye pia alisisitiza mshikamano wa wasomi na kutumia usomi wao ili kuleta maendeleo.

Wengine ni mwanahabari mkongwe, Makwaiya wa Kuhenga, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Elimu ya Juu, Susan Lyimo na Dk. Azaveli Lwaitama wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao wote walisisitiza nguvu ya pamoja katika kuleta mapambano ya kifikra.

Rais Kikwete alitangaza kamati hiyo hivi karibuni na itaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine kwenye kamati hiyo itakayofanya kazi kwa miezi mitatu ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) ambaye ni Mbunge wa Kyela, Ezekiel Maige kutoka Jimbo la Msalala (CCM), Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Pia wamo Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
Duh, wee jamaa wa kitambo sana humu! 2007??? Heko, umekuwa mpinzani kitambo! Hapo una msimamo ila uliboronga kumshabikia mamvi!
 
Back
Top Bottom