Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Siri kuu za CHADEMA hizi hapa...

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
CHADEMA sasa ni zaidi ya chama kikuu cha upinzani nchini. Bungeni ikiwa na Wabunge 48 ambao ni sawa na asilimia 13.445 ya Wabunge wote 357,inafanya mambo makubwa. Inabuni,inahoji,inajenga hoja na kuomba miongozo ya Spika mambo yanapokwenda mrama. Nje ya Bunge ndio usiseme. Mikutano ya kueleza ukweli na ya kujadili mstakabali wa taifa inafanyika kwa ubunifu,ufanisi na mafanikio makubwa. Sasa imejijengea heshima na uaminifu mkubwa kwa wananchi. Inasubiriwa kutwaa dola. Siri ya mambo haya ni tatu. Kwanza,imesimama yenyewe. Inapambana na yeyote anayeweza kupambana nayo kisiasa. Haiogopi. Pili,inatumia kila nafasi ijitokezayo ipasavyo. Si nje wala ndani ya Bunge. Pia,ina uongozi bora uliojaa ubunifu,busara na uwezo.Natamani na kutumai kujiunga nayo nikijiunga siasani...
 
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.
 
Acha uongo bwana liyumba hayupo BOT yupo mtaani anafanya shughuli zake kama raia mwingine tu.
 
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.

kijana 7000 per day masaa24 ndo masharti yake hakuna kulala naona umekuja kuinjoy ajira mpya za lumumba
 
Wewe unasumbuliwa na mawazo bangi?kwa nini usisifie serikali ya ccm inayowezesha nyinyi kufanya uhuni mtakavyo na kuwatizama,kwa taharifa yako padri ikulu ataisikia mpaka mauti yanamkuta.

we unamsema mungu wa CHADEMA? Utaona watakavyokushambulia.
 
Napatwa na wakati mgumu wanaposema Chadema kushika dola,sio kazi rahisi kama kuingia bungeni na kutoa matusi na kupokea posho yako, ni kazi ngumu kuongoza nchi kaka usijidanganye bado wanahitaji muda mwingi kujipanga.
 
kijana 7000 per day masaa24 ndo masharti yake hakuna kulala naona umekuja kuinjoy ajira mpya za lumumba

yaani mtu akiwa na mawazo tofauti na wewe ndo adui? Unalazimisha mawazo yako yawe mawazo ya wote?
 
Ila CCM hiki chama hakifai Kbs!! Asante Mungu kunipa uelewa ningejibu nini siku nikifa kwakua kuipenda CCM ni kumchukia mwenye dhiki huku unamchekea!!
 
Napatwa na wakati mgumu wanaposema Chadema kushika dola,sio kazi rahisi kama kuingia bungeni na kutoa matusi na kupokea posho yako, ni kazi ngumu kuongoza nchi kaka usijidanganye bado wanahitaji muda mwingi kujipanga.
Mkuu, jana waziri nchimbi kawabomoa sana. Sijui kama watakuwa na pa kutokea
 
Hakiwezi kushika dola kwa mwenendo huu kwakweli tusidanganyane tuliowengi ni mashabiki na sio wanachama wala sio wapiga kura!!!
 
Ila CCM hiki chama hakifai Kbs!! Asante Mungu kunipa uelewa ningejibu nini siku nikifa kwakua kuipenda CCM ni kumchukia mwenye dhiki huku unamchekea!!
Usimdhihaki MWenyezi Mungu kiasi hicho. Mungu hana ushabiki wa siasa. Labda kama slaa ndo mungu wenu
 
Back
Top Bottom