Siri kuu yaghubika Vikao vya Kamati kuu ya Chadema, Wananchi wapagawa, wataka Majina yatangazwe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,295
222,379
Sasa ni Dhahiri kwamba Chadema ndio Nchi, Hii ni kwa sababu Habari za Chama hicho ndio pekee ambazo wananchi wanataka kuzisikia.

Bunge la Bajeti linaendelea lakini cha Ajabu Wananchi wote hawafuatilii kabisa! Sitaki kusema wamelipuuza, maana nitakuwa nafanya Uchochezi, Bali hali hii inatisha sana, Hii si kawaida Wallah tena!

Mnaacha kufuatilia Bajeti ya Nchi (hata kama huwa inatekelezwa chini ya 40%), Mnafuatilia Kamati kuu ya Chadema! Nyinyi Watanzania Mmekumbwa na nini?, Taarifa zinadokeza kwamba mlipoambiwa Internet imepata shida mkaamua kuunganisha betri za viredio vyenu ili msikose Taarifa za Chadema.

Sasa nawaambieni hivi, Msiondoke JF, muda wowote kuanzia sasa nitavujisha taarifa za Kamati Kuu.

FB_IMG_1648410131191.jpg
 
Msiondoke JF, muda wowote kuanzia sasa nitavujisha taarifa za Kamati Kuu.

Halafu utasikia vyama vilivyo chini ya chama dola kongwe vinalalamika kwanini CHADEMA ni maarufu kiasi taifa zima linasikilizia kila kinachoendelea kuhusu chama cha Demokrasia na Maendeleo ya kweli kwa waTanzania wote


TOKA MAKTABA :
17 February 2023

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki



Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?

Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.

Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.

Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.

Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.

Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.

John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.

Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima.
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Chadema ni kama Simba yule Moo ana 49% lakini anaogopwa na Wanachama wote isipokuwa Kigwangala tu

Ufipa yote mnamuogopa Mwamba isipokuwa TAL peke yake ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„

Ulale Unono ๐Ÿ˜€๐ŸŒŸ
TL Anamueshimu MBOWE kuliko hata familia yake. akikumbuka risasi 16 na mbowe alivyomuuguza. propganda hazifai
 
chadema imekosa mvuto kisiasa wallah

ni kama dubwasha flani lililo jifia kila likizinduka linakutana na izrael mtoa roho
 
Aliyekosa mvuto anawezaje kuua Bunge?
bunge limekufaje ndugu

kila kukicha miradi na bajeti kubwakubwa zinapitishwa huku inchi ikichanja mbuga chini ya mama yetu kipenzi!

fuatilia jungu kuu tbc pamoja na aridhio unapitwa na mengi sana ndugu
 
Kuna kipindi kilikuwepo, Chadema nilipenda kuwaita ni Wakombozi wa Nchi yetu, kipindi kifupi tena kimepita, baada ya tuhuma za Rushwa,

Sisi mashabiki wa Chadema, kawaida yetu ni wasema kweli tupu, Chadema sisi hatuna huruka ya uchawa,

Aliyepokea Rushwa aadabishwe, hata kama akiwa ni mwenyekiti wa chama
 
bunge limekufaje ndugu

kila kukicha miradi na bajeti kubwakubwa zinapitishwa huku inchi ikichanja mbuga chini ya mama yetu kipenzi!

fuatilia jungu kuu tbc pamoja na aridhio unapitwa na mengi sana ndugu
Siku nikiangalia TBC ndio siku nitang'oka macho! hivi mnawezaje kuangalia hiyo channel?
 
Back
Top Bottom