Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Imeandikwa kwa uweledi najua ila Biblia ipi mkuu..... King james au NIV ambayo imekiri biblia imechakachuliwa na hivyo kufuta mistari zaidi ya 100???
Mi nadhan dhumuni la kuandika bible ni kuleta ujumɓe wa jinsi binadamu tulivyo na uhusiano na Mungu ..kwa wakati uliopita uliopo na ujao na nini yatupaswa tuwe ili kuweza kuishi maisha pasipo kufa(baada ya kufufuliwa ) na Yesu kutokana na maelekezo aliyotoa sasa kwa kuwa wameandika wanadamu basi wanakuja wanadamu na mawazo yao wanaongeza na kupunguza vitabu/maandish kutokana na mapoƙeo ila ujumɓe ni ule ule toka Mwanzo mpaka Ufunuo ni kuhubiri ujio wa Yesu Kristo..

Kutolea mfano king james bible sawa sawa mjaluo au mmakonde aitafsiri kwa kilugha chao naye ni binadamu huenda akakosa maana ya tafsiri ya maneno mengine au akaona maandishi mengine sio sawa au akaamua kuacha yote kama ilivyo ndio maana kwenye tafsiri za biblia wanaandika sehemu walipotoa maandiko (mfano imetokana na jerusalem ɓiɓle or king james bible) ...inaeleweka england asilimia kubwa ya wakazi wake ni anglicana (nikimaanisha dhehebu linatokana na mapokeo kutokana na kile walichotafsiri kutoka kwenye biblia ..rejea waadventista ,wapentekoste ,catholic n.k) kila dheheɓu hapo ukichukua bible zao wanazotumia utofauti utakuja kwa kile ulichozungumza( mf.king james from england-anglicana) ila dhumuni ni lile lile.
 
Habari za jioni wana JF mada ya leo pia ni sensitive kidogo maana inagusa imani za watu
hivyo tunapojadili hoja humu tuhakikishe tunazingatia hilo pia udini na kejeli na matusi sio uwanja wake humu, nataka tujadili kwa kujifunza sio kupambana.

habari ya masiku mpendwa zitto junior

ahsante kwa mada yako nzuri na samahani kwa kuchelewa

mpendwa zitto junior kabla ya kuleta mchango wangu wowote kuhusu hii mada ninaomba niwie radhi kabisa kwa yafuatayo KADIRI YA USHAURI WAKO MZURI HAPO JUU. (hii ni kwa sababu nimeona baadhi ya post zikidai zikiliingiza humu kanisa katoliki kwa ngonjera zilezile za upagani upagani upagani vitabu vya kipagani kwa misingi ileile ya chuki. hasa ukizingatia hoja za uzi wako ni nzito na hazihitaji majibu ya nini kilichofanywa na kanisa katoliki ila unahitaji majibu ya aya ulizoona zinacontradict katika version za kiprotestant na pia majibu ya kwa nini hiki kichukuliwe na hiki kiachwe. nadhani huko ndiko hoja zako zilikolala na ulikohitaji majibu na sio malumbano ya kidini na kutupia lawama kanisa katoliki au dhehebu fulani (mimi naomba nisiingie huko kama ulivoshauri kwenye uzi wako ninaheshimu hilo)

mpendwa mada yako kiufupi inahusu biblia. kwa upande wangu kuijadili tofauti na mtiririko wa kanisa katoliki au kuijadili kiprotestant au kuijadili ingeneral kwa maana ya kugusia michakato yote iliowahi kufanywa na madhehebu yote kiujumla kwangu ninakiri sitaliweza hilo mpendwa ni lazima nitavuruga mambo

isipokuwa kama utaniruhusu kuijadili kikanisa katoliki kwa maana ya kujibu hoja zako zote juu sababu za kujumuishwa au kutojumuishwa kwa kitabu fulani au contradictions ulizoziibua ndani ya bibilia HAYO YOTE ULIOYAIBUA YANAJIBIKA NA KUFAFANULIKA BILA SHIDA HATA KIDOGO

hivyo mpendwa zitto junior kama utapenda ninaomba hii mada yako niijadili kwa mlengo huo niliouomba (hapo juu) ninamaana yangu na sababu zangu za kuomba ivyo na baadhi ya sababu mpendwa zitto junior ni hizi zifuatazo:

ninatambua kuwa bila ubishi kwa upande wa biblia kanisa katoliki ndilo mama wa biblia na linajitegemea 100% katika hilo yaani kuanzia versions zake, wataalamu "scholars" nk. halihitaji msaada wala kukopakopa mambo au wataalamu ili kufanya jambo fulani la kibiblia. (toka karne ya kwanza mpaka leo kibiblia linajitegemea na zaidi madhehebu mengine mengi yamekopi na kupest vitu vingi vya kibiblia toka huko pasipo kuelewa nini kifanywacho na kizingatiwacho na kanisa. ndio maana leo kuna contradictions na maswali kibao wasioweza kuyajibu/kufanunua na mojawapo ni hayo ulioyaibua. lakini ndani ya kanisa katoliki hayo yote yanajibika na kuelezeka vizuri tu)

hivyo kwa upande wangu ninakuomba nilete ufafanuzi wa vitabu vya biblia vilivyopo na vilivyoachwa kwa upande wa kanuni na taratibu "bible canon" zilizotumiwa na kanisa katoliki pekee. huko kwa waprotestant nisikuguse (kwani hata mjadala na mahojiano ya huu uzi upo juu ya version KJV na NIV(hii sijui kama inaidhini ya kanisa katoliki sina uhakika) ambazo ninaweza kuziita za kiprotestant kwa sababu hazina hizini ya kanisa.

hivyo huo mjadala wa KJV na NIV ninaomba nisiuguse kwani sina utaalamu na izo versions na zaidi binafsi hazinihusu na zaidi kutokuvuruga hali ya mambo kama ulivoshauri huko juu

mpendwa zitto junior sio kwamba mimi ni mbinafsi hapana ila lengo langu ni zuri sio kuanzisha malumbano ya kidini. kumbe ninapozungumzia umama na kujitegemea 100% kwa kanisa katoliki kibiblia ni kwa factors kama izi:

**ni kanisa katoliki chini mtaguso wa trento "council of trent" ndio lilivipa majina vitabu vya biblia "proper titles" kama uonavyo leo katika biblia zote za kikatoliki kokote duniani. (kwa wengine sijui, na kama tunafanana basi hakuna shaka walikubaliana na maamuzi ya mtaguso wa trento)

hivyo maswali kama hizi barua zinazoitwa za mtume paulo ziliandikwa na paulo kweli? au hii injili ya mathayo iliandikwa na mathayo kweli ? (hayo yote ndani ya kanisa katoliki yanajibika na kufafanuliwa vizuri kabisa kwani lenyewe ndio liliamua kitabu fulani kiitweje nk)

**ni kanisa katoliki chini ya askofu mkuu wa canterbury stephen langton, katika karne ya 13 aliganya biblia katika chapters. kama unavoiona leo. hivyo ni kanisa katoliki ndio liliamua kitabu fulani kiwe na sura ngapi au kiishie sura ipi.

na kwa niongeza tu ni kuwa "Santes Pagninus" divide old testament into verses in 1528, na mwisho "Robert Ettienne" aliyekuwa printer huko paris ufaransa divide the new testament into verses in 1551.

**kutafsiri biblia sio tu kufahamu lugha asili ya kitabu husika cha biblia. lakini pia kufahamu kwa kina maana halisi ya misamiati/maneno ya biblia yaliokuwa yakitumika wakati tukio husika linafanyika, yaani msamiati/neno fulani lilimaanisha nini wakati huo na sio leo au jana, "maana husika kwa wakati husika" (hiyo ni kwa sababu ya mabadiliko ya lugha kwani lugha nyingi zimepitia mabadiliko kadhaa ili kuziboresha. mf kuna kiingereza cha kale, cha kati na cha kisasa, kuna kiebrania cha kale ambacho kilitumika kuandikia agano la kale kwa wayahudi na cha kisasa. na ndio maana wayahudi walikataa kabisa kuiboresha biblia yao toka kiebrania cha kale kuja cha kisasa au kiaramayo lugha ya mtaani na ya mazungunzo wakati wa yesu. yaani ndani ya sunagogi/hekaluni somo linasomwa kwa kiebrania cha kale then wale waoitwa "waandishi" / "waalimu wa sheria" wanatafsiri kwenda kiaramyo ili somo husika lieleweke na wote. sababu kuu ni hiyo yaani kulinda maana halisi za misamiati/maneno kama yalivotumika wakati husika.

sasa kwa upande huo wa lugha kanisa katoliki linawataalamu wa kutosha wa lugha hizo tena katika ukale wake na sio usasa wake. na ndio maana kanisa katoliki linasisitiza translation ya biblia zifanyike moja kwa moja toka katika original language of sacred authors. na sio kukopi toka sijui vulgate nk rejea "Divino Afflante Spritu" ya pope pius XII 1943 au "Dei verbum" Dogmatic constitution on divine revelation, 18-11-1965 ya vatcan II 1962

ndio maana new american bible waliokuwa wakifanya translation toka douay-rheims version walisitisha na kuanza kuntranslate toka katika original language, old testament directly from original hebrew nk.

**ni kanisa katoliki pekee ambalo hutafuta ukweli wa maandiko matakatifu kwa kuzingatia mambo muhimu matano yafuatayo:

1: elimu juu ya mazingira ya uandishi wakati kitabu husika kinaandikwa, muandishi aliandika kitabu chake katika mazingira yapi yeye pamoja na waandikiwa. (hayo mazingira ya uandishi ndani ya biblia za kikatoliki yanapatikana mwanzoni mwa kila kitabu husika)

2: historia na utamaduni wa jamii za wakati kitabu husika cha Biblia kinaandikwa,

3: jiogarafia ya nchi za Biblia,fani na miundo ya vitabu vya Biblia

4: lugha asili ya kitabu husika cha Biblia (hiyo mpendwa wengi huwa tunachukulia poapoa lakini kwa upande wa kanisa katoliki limewekeza katika hilo kwani ni muhimu sana kufahamu na kuielewa lugha asili iliotumika kuandika kitabu husika ili kupata ujumbe halisi uliokusudiwa na mwandishi. ndipo utakuta kanisa katoliki linawataalamu lukuki wa lugha za biblia yaani kiebrania cha kale kilichotumika kuandika agano la kale, kigiriki kilichotumika kuandika agano jipya na LXX, kilatini nk

5: mikazo ya kiteolojia/lengo kuu la mwandishi.

hivyo kutokana na hayo matano hapo juu. kukinzana kwa baadhi ya aya za biblia kama ulivoeleza kwetu kanisa katoliki hakupo. hakipo kwa sababu katika kutafsiri maandiko matakatifu na ili kupata ujumbe aliokusudia kutoa/kufundisha mwandishi wa kitabu husika ni lazima kuzingatia mambo hayo matano hapo juu (mambo hayo yakizingatiwa na kuheshimiwa basi mawazo yote ya contradiction uliyoeleza katika uzi wako na post zako yanakuwa yamekufa na kila aya inakuwa cleared kabisa bila shida, nitakuonesha mfano mmoja kwa post iitayofuata iwapo utaniruhusu kuchangia kama nilivoomba)

mwisho
mpendwa kuhusu bible historia yake ni pana sana hivyo masuala ya
JEWISH CANON/ PALESTINE CANON , ALEXANDRINE CANON kwa agano la kale na KANUNI YA MURATORI kwa agano jipya. nkipata nafasi nitachangia

pia ancient manuscripts of the bible kama OLDEST HEBREW MANUSCRIPT ambayo ni copy ya kitabu cha isaya iliogunduliwa mwaka 1947 huko yeriko,

CODEX SINAITICUS (iligunduliwa 1858 katika kanisa la mtakatifu katarina huko sinai ambapo nusu ya agano la kale linapatikana humo ),

CODEX VATICANUS (hiyo ipo pale vatcan library karibu agano lote la kale lote linapatikana humo) ,

CODEX ALEXANDRINUS (agano ka kale lote linapatikana humo)

hizo manuscripts zote ni za karne ya nne na ya tano AD

kuhusu hayo hapo juu, kuhusu barua tunaxoziita za paulo , contradiction za baadhi ya aya za vitabu vya biblia nk ninaomba kuleta mchango wangu baadae kama Mungu akipenda.

TUOMBEANE UZIMA .......

mtu chake
SANCTUS ANACLETUS
Otorong'ong'o
KIBUYU 180
 
Biblia iliandikwa hivyo makusudi ili watu ambao wataichukulia kichwa kichwa lazima waje kuwa vichaa. na ndio maana unakuta kuna watu walifia majini na wengine na kufa na njaa yote hiyo ni kutaka kuvunja rekodi ya yesu.
 
Habari za jioni wana JF mada ya leo pia ni sensitive kidogo maana inagusa imani za watu ila kutokana na kuwepo hitaji la kuweka rekodi sawa nimeona nilete uzi huu ili tujifunze zaidi. Na sababu kubwa ya kuleta uzi huu ni kutokana na mada nazoleta humu nyingi zinatumia pia vitabu nje ya biblia kama source ya taarifa na kumekuwa na wengi wanaokuja na hoja kwamba chochote kilicho nje ya biblia sio kweli yaani quran,midrash,tanakh/torah,zohar,apocrypha,Pseudipigrapha zote ni batili sasa ni kutokana na hoja hiyo imenipelekea kuandaa uzi huu hivyo tuusome kwa makini na tuujadili kwa ustaarabu tu yote kwa yote kujifunza. Nitaugawa uzi huu kwa sehemu mbili ili iwe rahisi kuusoma na ningependa kabla ya kuchangia uusome wote na kuuelewa. Karibuni
View attachment 830330

UTANGULIZI
1. Biblia ni mjumuiko wa vitabu vya manabii walivyoandika kuhifadhi matukio katika historia ya imani yao kwa Mungu na ilikusanywa katika karne ya 3 baada ya Yesu baada ya kuonekana vitabu vya kiimani viko vingi vinakinzana hivyo wakaamua wawe na kitabu kimoja cha kutumika na wote na ilikuwa katika kigiriki na kiebrania. Baada ya karne zaidi ya 10 kupita biblia ya mapema kabisa kutafsiriwa kuingia kwenye kilatin iliyokuwa lugha ya Roma, ilikuwa ''vulgate'' iliyotoholewa kutoka kiebrania na kigiriki kwenda kilatin na padre Jerome karne ya 14 ila tafsiri ya kiingereza ilikuwa king james version karne ya 15 ambayo hata biblia za kiswahili na lugha zingine maelfu zimetoholewa hapo na ambacho wengi hatujui ni kwamba vitabu ambavyo leo tunaviita apocrypha vilikuwepo kwenye KJV ya kwanza ila mataifa mengi yalipotafsiri hayakuvijumuisha hivyo vitabu 14!!! Na leo hii ukivitumia humu JF kujenga hoja utaambiwa ni vya kishetani wakati biblia ya kwanza ya english iliviweka??

Miaka mingi ikapita ndipo yakaja matoleo mengine tofauti ila kwa karne hii biblia inayotambulika kutumika dunia nzima ni NIV yaani New International Version ya 1973, ambayo ilikuja kufanya utafiti na kutumia vyanzo mbalimbali vya nyuma zaidi na kutengeneza tafsiri yake na muhimu hapa tufahamu NIV iligundua makosa kwenye KJV na ikafuta mistari hiyo kwa kigezo kwamba mistari hiyo haikuwepo kwenye vyanzo vya mwanzo ikimaanisha viliongezwa baadae sana. Baadhi ya mistari ilioongezwa na ambayo NIV imeifuta ama kutoitambua Ni Marko 11:26, 15:28,9:44,9:46 Mathayo 23:14,18:11,17:21, Luka 17:36 Yohana 5:3-4, Matendo 8:37 n.k kwa uchache wake ila mingi zaidi iligundulika haikuepo kwenye vyanzo vya mwanzoni kabisa na kwamba vimeongezwa kinyemela.

Simply ikimaanisha biblia ya kiswahili tunayotumia hii ya chama cha biblia iliyotokana na KJV tumepotoshwa?? Je wakristo tumeambiwa haya kanisani?

Je nani mkweli kati ya KJV na NIV??
View attachment 830331
VITABU VILIVYOPUNGUZWA
Baada ya biblia ya nwanzoni kabisa ya kilatin kuwa na vitabu zaidi ya 76 na version zingine hadi 84 kuna vitabu vilitolewa na kina Jerome kwa sababu mbalimbali ikiwemo kughushiwa majina, kutovuviwa na Roho mtakatifu, kukinzana na vitabu vingine vya Biblia,kuandikwa na manabii wa uongo,utata wa maandiko n.k na vitabu hivyo ni kama 4 Maccabees, Assumption of Moses, Ethiopic Book of Enoch (1 Enoch), Slavonic Second Book of Enoch,Book of Jubilees,3 Baruch, Letter of Aristeas,Life of Adam and Eve, Ascension of Isaiah, Psalms of Solomon, Sibylline Oracles, 2 Baruch,Testaments of the Twelve Patriarchs na vinginevyo na hii ndio kitovu cha uzi huu embu basi tuchambue kwa pamoja.
View attachment 830333

TATIZO LA UANDISHI
Kuna hoja zilitolewa kwamba hivi vitabu vilivyoachwa kwenye biblia yaani Pseudipigrapha na Apocrypha mfano book of enoch, Book of Adam & Eve n.k kwamba vilitolewa kwenye biblia sababu kuna utata juu ya waandishi na kwamba kurasa zingine ziliongezwa baadae.... Ila leo hii wanatheolojia wote duniani wanakubali kuwa biblia bado ina pseudipigraphi nyingi mfano Isaya iliandikwa karne 8 kabla ya kristo yaani sura 1-39, ila kipande kuanzia sura 40-55 iliandikwa na mtu ambaye hajatambuliwa mpaka leo huko babeli na sura 56 mpaka 66 imegundulika na wanatheolojia dunia nzima kuwa ziliongezwa baadae yaani miaka mia kadhaa tokea isaya akiandike!!!

Hata jeremia kuanzia sura ya 26 iliongezwa miaka mamia baadae!! Hivyo swali la kujiuliza kwanini basi vitabu vingine vilitolewa kwa hoja hii ilihali biblia bado ina vitabu vyenye kasoro zilezile?? Mfano mingine ni waebrania, Wimbo ulio bora vyote vina utata wa uandishi na mikono zaidi ya miwili imehusika kwa gap la miaka zaidi ya 100!! Je sababu ya kupunguza vitabu vingine kwa kisingizio hiki ni halali au kuna mengine tunafichwa???

Hongera sana Zitto jr,
Unafanya homework kubwa sana yakudadisi maandiko, na kwa kufuatilia mada zako unapenda sana mambo yanayodhaniwa kuwa na Utata!
Kuhusu Mada hii naomba nijibu kama ifuatavyo;Kwanza ni Kweli kabisa kuna makosa ya Watafsiri na Wafanya nakala (Copysts) Na kama umewahi kufanya kazi au kusikia kazi ya kutafsiri sio ya polepole hata kidogo.
Baada ya watafiti na Wanatheolojia kuchunguza maandiko waligundua makosa mengi ya Tafsiri na ya Wazalisha Nakala na makosa hayo yalipimwa na kutambulika kuwa hayana "Madhara" They are Innocuous!.
Kwa kuwa makosa yaliyoonekana katika Biblia ni dhaifu sana na wala hayajapotosha Ujumbe Mkuu uliokusudiwa kwa Watu.Wengine hawakuridhika na hoja hiyo ndipo uwepo wa matoleo ya biblia mbalimbali (KJV,NIV na nk).
Hivyo hoja ya kuwa Biblia ina makosa - YES! Yapo makosa ya wanadamu wala sio Makosa ya Mungu.(spelling error,punctuations,repetitions na nk). LAKINI HAYAJAONDOA UJUMBE MKUU WA UKOMBOZI.
Hata mistari ya biblia haikuwepo hapo kabla ni mapendekezo ya Watu ili iweze kusomeka vema.

Hoja ya Apocrypha ni dhaifu sana! Vitabu vilivyokataliwa vingi vilikataliwa kwa hoja ambazo tukianza kuzijadili hapa tutachukua muda kidogo,lakini cha msingi kuhusu Vitabu vilivyofichwa ni kuwa havina mantiki wala haviendani na historia halisi ya Wahusika na Mazingira pamoja na Utamaduni.( Historicity of The Bible).

Lakini pia apocrypha ilikuja hasa baada ya kanisa la kwanza kutengana - Western na eastern schism.,na kwa ukali mkubwa baada ya Martin Luther na Harakati za Protestantism ambapo sasa! Waprotestant waliamua kuviacha kabisa vitabu hivyo kwa sababu vilisound too catholic.

Ukiacha Biblia vitabu vya imani nyingine havipaswi kabisa kujadiliwa humu kuna watu hawatabaki kama walivyo katika Imani zao! Wakijua Historia yake na uandishi wake.
Asante.
 
Mkuu SALA NA KAZI mchango wako umeshiba haswaa, nasubiri nondo zako kuhusu baadhi ya vitabu kuchukuliwa na vingine kubaki apocrypha.

Ubarikiwe
ninashukuru kwa kunielewa mpendwa na samahani kama kunakitakachokuwa kimeharibika .........

kiukweli mada zako ni nzuri na fikirishi sana na zinatusaidia kujifunza mambo mengi kwa kuturudisha library ili kutafuta maarifa zaidi na zaidi.

binafsi nimejifunza mengi sana kutoka kwako. "uwezo wako ni mkubwa sana" na zaidi wewe ni mvumilivu sana hasa pale mada zako zinapoharibiwa na mijadala ya kidini zaidi kuliko neno la Mungu.

NINAKUTAKIA MAISHA MAREFU NA MAFANIKIO KATIKA JITIHADA ZAKO.
 
ndugu katika kristo zitto junior ninaomba kutumia nafasi hii tushirikishane kimawazo juu ya moja ya maswali uliouliza katika uzi wako.

kumbe hiki hapa chini ndicho ambacho kwa kuanzia tu ningependa kukichangia then mengine nitaleta mawazo yangu kadiri ya nafasi na muda
Mathayo 28:9 inasema Yesu baada ya kufufuka aliruhusu Mary amshike ila Yohana 20:17 Inaonyesha baada ya kufufuka na kuonana na mary, Yesu akamzuia kumgusa sababu alikua bado hajarudi kwa Baba!!
kwa faida ya wengi ongeza na hii pia.

ni kwanini Yesu amemzuia Maria Magdalena asimguse katika sura ya 20:17 lakini baada ya aya chache za sura hiyo hiyo yaani 20:27 anamwambia Thomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu, ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu?

mpendwa zitto junior hayo ni moja ya maswali kati ya mengi ambayo watu wengi hutumia kudai kuwa biblia inajipinga yenyewe ila ukweli halisi haupo ivo yaani biblia haijipingi ila wengi wetu ndio hatujui na wala hatuthamini na kuzingatia kabisa mambo muhimu katika kutafuta ukweli wa kimaandiko. (kiufupi sisi ndio tunajipinga na wala sio biblia)

hayo mambo ambayo yapo matano nimekwisha yafafanua katika post yangu post namba #145. na hilo namba tano yaani lihusulo mambo ya lugha ndilo linakwenda kujibu swali lako.
4: lugha asili ya kitabu husika cha Biblia (hiyo mpendwa wengi huwa tunachukulia poapoa lakini kwa upande wa kanisa katoliki limewekeza katika hilo kwani ni muhimu sana kufahamu na kuielewa lugha asili iliotumika kuandika kitabu husika ili kupata ujumbe halisi uliokusudiwa na mwandishi. ndipo utakuta kanisa katoliki linawataalamu lukuki wa lugha za biblia yaani kiebrania cha kale kilichotumika kuandika agano la kale, kigiriki kilichotumika kuandika agano jipya na LXX, kilatini nk
jitahidi ulisome kwa umakini na kulielewa kwani ndilo linalokwenda kujibu swali lako hapo juu

mpendwa zitto junior
tunasoma katika Biblia Takatifu kuwa siku ile ya kwanza ya juma yaani aliyofufuka Yesu, Maria Magdalena na wenzake wengine walipokwenda kaburini waliukosa mwili wake, walipokuwa wakiondoka kurudi kuwapasha habari mitume walikutana na Yesu naye akawaambia “Salaam wao wakamkaribia wakamshika miguu wakamsujudia” (Mt 28:9).

sasa Je, kama Mwinjili Yohane anasema Maria Magdalena alizuiwa kumgusa lakini Mathayo Mwinjili anasema alimgusa, tusadiki lipi? tuamini lipi na tuache lipi ?, je bible inajipinga ? au sisi ndio tunajipinga ?

Kama suala lingekuwa ni kutomgusa yesu baada ya ufufuko wake. je, ilikuwa ni kutoguswa na Maria Magdalena tu ? au wote na mbona Tomaso alimgusa kabla hajapaa ?

Pengine ni vyema turudi kwenye lugha asili ya mwinjili yohane yaani kigiriki sasa tusome Biblia Takatifu kwa lugha ya Kigiriki lugha aliyotumia Yohane kuandika Injili yake, ili tuweze kupata tafsiri sahihi ya kile alichokisema Yesu.

Nasoma Injili Yn.20:17
“Legei auth o ihsous, “mh mou autou, aupw gar avnabebhka pros ton patera mou... poreuou de pros tous adelfous mou, kai eipe autois; a vabai vw pros tov patera mou kai patera umwn, kai eov mou kai eon umwn”

Kwa maandiko hayo ya kigiriki cha yohane mwinjili tunaona kuwa, Maneno, me mou apotou, yaani usinishike katika sentensi za lugha ya Kigiriki, huundwa kwa muunganiko wa “me na katazo lililo katika wakati uliopo”.

Hii ni kusema, neno “usinishike” linamaanisha amri ya kukataza kuendelea kutenda kile ambacho tayari kinafanywa au kinatendeka au kinaendelea kutendwa.

Amri hii inalenga kukatisha tendo lisiendelee. Ni sawa na kusema, acha kufanya ufanyalo au koma kulifanya unalolifanya.

Kwa maana hiyo, Amri ya Yesu (Yn 20:17) kwa Maria Magdalena ni ya mfumo huu. Anamwambia kwa kigiriki, me mou apotou, kuonesha kuwa Maria Magdaleja alikuwa tayari amemshika Yesu na alikuwa an`endelea kumshikilia. Yesu anachokataza ni tendo la Maria kubaki amemshikiria Yesu yaani anamwambia aache kuendelea kujing`ang`aniza kwake amwachie ili mambo mengine yafanyike.

Kwa mant)ki hiyo, Mwinjili Yohane hatofautiani na Mathayo kuhusu Maria Magdalena kumshika Yesu.

Yesu hamzuii Maria Magdalena kumgusa bali anamwambia imetosha asiendelee kumshika.

Ni kweli kwamba amefurahi kumwona lakini furaha hiyo ya maria magdalena ni lazima izingatie ukweli kuwa kitendo cha Yesu kuonekana tena baada ya kifo chake si cha kudumu ni kitu cha Muda mfupi, yaani kitu cha kupita tu.

Ndiyo maana anaendelea kumwambia sababu ya kumkataza, Yesu anasema, “aupv gar anabebhka pros ton patera mou. Yaani, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Ni kweli Yusu alitakiwa aondoke ulimwenguni kwenda kwa Baba yake ili apokee tuzo lake kwa kazi aliyokwishaifanya.

Ndiyo maana tukirejea nyuma kidogo aliwaambia mitume wake akisema, "Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona." na hIlo ni kwa Sababu anaenda kwa baba (Y. 16:16).

Sasa kitambo kidogo, ndicho hicho kwani kikiisha anapaswa kuondoka kwenda kwa baba.

Yesu anaendelea kumwambia, “poreuo de pros tous Adelphous mou,kai eipe autois,anabaivw pros tov patera mou kai patera umwn,kai theon mou kai theon umwn”.yaani enenda kwa ndugu zangu ukawaambie ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu .naye ni Mungu wenu.

Maneno hayo ya Yesu yanauonesha uhusiano wa karibu kati yake na Mungu na kati ya Mungu na mitume kumbe hata kama ataondoka, hakuna kit!kacho haribika.

Kutokana na maelezo hayo ni hakika kwamba Yohane alitaka kutufikishia ujumbe fulani ambao ama alishindwa kufikisha au alifikisha lakini haukuweza kueleweka kwetu sisi ambao Biblia tumeipokea katika tafsiri toka lugha ya Kigiriki.

Laiti tungekuwa tunajua jinsi sentensi za kigiriki zinavyoundwa na masharti yake, tusingepata shida kumelewa yohane.

kumbe kwa kifupi Yesu anapomwambia Maria Magdalena asimguse anamaanisha kwamba, Kumgusa Yesu kunakotakiwa tangu alipofufuka ni kwa njia ya imani. Maana yake ni kuwa, baada ya kupaa mtu anamgusa Yesu si kwa mkono bali kwa kuamini kuwa amefufuka na hafi tena.

Ndiyo maana baada ya siku 8 anapowatokea tena mitume wake, Yesu alimwambia Thomaso kuwa, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona wakasadiki.Hao ndio mimi na wewe ambao tunamsadiki kwa imani yetu ingawa hatukumwona kwa macho.

Pia habari hii ya ufufuko ni habari ya kimisionari zaidi. Hatutakiwi kupoteza muda tukishangilia ufufuko wa Yesu peke yetu bali tutoke twende tukawashirikishe wenzetu ambao bado hawaijui ndiyo maana anamwambia Maria magdalena usiniguse maana yake, usipoteze muda mwingi katika kuniabudu kwa furaha bali nenda kawaeleze mitume kile ulhchokiona karibu naenda kwa Baba na ningependa kuwaona wao badala ya kubakia na wewe tu.
(Yn. 20:17).

hivyo kwa maelezo hayo mathayo na yohane hawajipingi hata kidogo. na kama tulivoona tatizo sio waandishi ila tatizo ni watafsiriji wa biblia toka katika lugha mama za waandishi kuja lugha zetu hizi sijui kiiengereza, kiswahili nk

mpendwa zitto junior
ninaomba niishie hapo kwa leo pia kama kutakuwa na makosa ya lugha kama kukosea herufi hasa hicho kigiriki nk NINAOMBA UTANIWIA RADHI sababu mimi sio mtaalumu sana wa hiyo lugha ila ninaibiaibia tu. lakini naamini lengo langu na ujumbe wangu vitakuwa vimefika.

NIKUTAKIE JUMAPILI NJEMA NA SIKU NJEMA PIA.

mtu chake
SANCTUS ANACLETUS
KIBUYU 180
Otorong'ong'o
 
kama biblia imetungwa na mtu basi huyo mtu atakuwa sio mtu wa kawaida
ni kitabu kilichojaa hekima nguvu uponyaji
hakuna kitabu maarufu dunia zaid ya biblia
mimi huwa nasoma kila siku na kupata vitu vipya

tatizo imani ndio shida usipokuwa na iman utaona kama gazet tu
Imani na uhalisia au ukweli ni vitu tofauti,ndiyo maana inawezekana mtu kuamini et ng'ombe ni Mungu ila kwa mwengine anaona ni upuuzi.
 
Hongera sana Zitto jr,
Unafanya homework kubwa sana yakudadisi maandiko, na kwa kufuatilia mada zako unapenda sana mambo yanayodhaniwa kuwa na Utata!
Kuhusu Mada hii naomba nijibu kama ifuatavyo;Kwanza ni Kweli kabisa kuna makosa ya Watafsiri na Wafanya nakala (Copysts) Na kama umewahi kufanya kazi au kusikia kazi ya kutafsiri sio ya polepole hata kidogo.
Baada ya watafiti na Wanatheolojia kuchunguza maandiko waligundua makosa mengi ya Tafsiri na ya Wazalisha Nakala na makosa hayo yalipimwa na kutambulika kuwa hayana "Madhara" They are Innocuous!.
Kwa kuwa makosa yaliyoonekana katika Biblia ni dhaifu sana na wala hayajapotosha Ujumbe Mkuu uliokusudiwa kwa Watu.Wengine hawakuridhika na hoja hiyo ndipo uwepo wa matoleo ya biblia mbalimbali (KJV,NIV na nk).
Hivyo hoja ya kuwa Biblia ina makosa - YES! Yapo makosa ya wanadamu wala sio Makosa ya Mungu.(spelling error,punctuations,repetitions na nk). LAKINI HAYAJAONDOA UJUMBE MKUU WA UKOMBOZI.
Hata mistari ya biblia haikuwepo hapo kabla ni mapendekezo ya Watu ili iweze kusomeka vema.

Hoja ya Apocrypha ni dhaifu sana! Vitabu vilivyokataliwa vingi vilikataliwa kwa hoja ambazo tukianza kuzijadili hapa tutachukua muda kidogo,lakini cha msingi kuhusu Vitabu vilivyofichwa ni kuwa havina mantiki wala haviendani na historia halisi ya Wahusika na Mazingira pamoja na Utamaduni.( Historicity of The Bible).

Lakini pia apocrypha ilikuja hasa baada ya kanisa la kwanza kutengana - Western na eastern schism.,na kwa ukali mkubwa baada ya Martin Luther na Harakati za Protestantism ambapo sasa! Waprotestant waliamua kuviacha kabisa vitabu hivyo kwa sababu vilisound too catholic.

Ukiacha Biblia vitabu vya imani nyingine havipaswi kabisa kujadiliwa humu kuna watu hawatabaki kama walivyo katika Imani zao! Wakijua Historia yake na uandishi wake.
Asante.
Hongera sana Zitto jr,
Unafanya homework kubwa sana yakudadisi maandiko, na kwa kufuatilia mada zako unapenda sana mambo yanayodhaniwa kuwa na Utata!
Kuhusu Mada hii naomba nijibu kama ifuatavyo;Kwanza ni Kweli kabisa kuna makosa ya Watafsiri na Wafanya nakala (Copysts) Na kama umewahi kufanya kazi au kusikia kazi ya kutafsiri sio ya polepole hata kidogo.
Baada ya watafiti na Wanatheolojia kuchunguza maandiko waligundua makosa mengi ya Tafsiri na ya Wazalisha Nakala na makosa hayo yalipimwa na kutambulika kuwa hayana "Madhara" They are Innocuous!.
Kwa kuwa makosa yaliyoonekana katika Biblia ni dhaifu sana na wala hayajapotosha Ujumbe Mkuu uliokusudiwa kwa Watu.Wengine hawakuridhika na hoja hiyo ndipo uwepo wa matoleo ya biblia mbalimbali (KJV,NIV na nk).
Hivyo hoja ya kuwa Biblia ina makosa - YES! Yapo makosa ya wanadamu wala sio Makosa ya Mungu.(spelling error,punctuations,repetitions na nk). LAKINI HAYAJAONDOA UJUMBE MKUU WA UKOMBOZI.
Hata mistari ya biblia haikuwepo hapo kabla ni mapendekezo ya Watu ili iweze kusomeka vema.

Hoja ya Apocrypha ni dhaifu sana! Vitabu vilivyokataliwa vingi vilikataliwa kwa hoja ambazo tukianza kuzijadili hapa tutachukua muda kidogo,lakini cha msingi kuhusu Vitabu vilivyofichwa ni kuwa havina mantiki wala haviendani na historia halisi ya Wahusika na Mazingira pamoja na Utamaduni.( Historicity of The Bible).

Lakini pia apocrypha ilikuja hasa baada ya kanisa la kwanza kutengana - Western na eastern schism.,na kwa ukali mkubwa baada ya Martin Luther na Harakati za Protestantism ambapo sasa! Waprotestant waliamua kuviacha kabisa vitabu hivyo kwa sababu vilisound too catholic.

Ukiacha Biblia vitabu vya imani nyingine havipaswi kabisa kujadiliwa humu kuna watu hawatabaki kama walivyo katika Imani zao! Wakijua Historia yake na uandishi wake.
Asante.

Ninakushukuru sana wewe,pamoja na "Sala na Kazi" kwa namna mlivyoweza kujibu hoja nyingi zilizojibandika katika uzi huu. Mmetumia maelezo ya kisomi sana kuhitimisha mjadala.Kwa kuwa uzi umekwisha kufika mbali, mimi nitaleta uzi pekee kueleza ni nani alifanya nini kuhusu Biblia na ni akina ni bendera fuata upepo tu linapokuja suala la Biblia na ni akina nani wanazalisha mambo ya kizushi kwamba kuna Injli hii au ile ilikataliwa tu lakini na yenyewe ilifaa kuingizwa katika Biblia.

Kuna watu kwa sababu ya kufichwa historia,wanaamini kuwa wanaifahamu sana Biblia, kumbe wanakimbia na vipande vya Biblia tu huko waliko.Na kwa kuwa wameendelea kupiga mayowe muda mrefu na wanafanya hivyo wakifikiria wao ndio wenye ukweli,basi muda si mrefu tutaweka mambo hadharani.Na nina imani ukweli huo utakapowekwa hadharani hawatabaki salama huko waliko.
 
Ahsante mkuu kwa kuniita kwa sauti ya juu..

Hii post yako nimeihifadhi...

Mkuu mitale na midimu hebu pita huku upate maarifa...wachana na mambo ya chuki...elimu haina mwisho
Asante kwa maoni. Ingawa hayajaonyesha hicho unachokiita chuki katika usheherekeji wako wa mchango hapo juu . Na sijaelewa unataka nichukue nini kwenye maelezo na makubaliano ya kikanisa kulinganisha na nilichokieleza huko awali katika michango na maoni yangu.
Asante kwa maoni lkn.
 
Ukiacha Biblia vitabu vya imani nyingine havipaswi kabisa kujadiliwa humu kuna watu hawatabaki kama walivyo katika Imani zao! Wakijua Historia yake na uandishi wake.

Tunaomba uandae uzi kuhusu hili jambo mkuu, ili watu waelimike na kujitambua vizuri zaidi ( lengo likiwa ni kukuza maarifa ).
 
Back
Top Bottom