Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

MAANDIKO YENYE UTATA
Kuna mistari mingine ambayo ni halali kibiblia ila imebadilishwa maeneo husika ipo mistari zaidi ya 50 kwenye agano jipya mfano Yohanna 7:53-8:11 kuhusu Yesu kuwepo hekaluni ila ghafla kipande kati ya 7:52 na 8:11 vimechomeka story ya mwanamke kahaba alietaka kupigwa mawe na ghafla mstari wa 12 unaendelea Yesu akiwa hekaluni hii inakubaliwa na wanatheolojia wote kuwa kilichomekwa na hakikuwepo kwenye maandiko orijino kama una biblia hapo kasome hiki kipande alafu utaelewa nachosema. Kanisa likaamua kuita vitabu vyenye maandiko na uandishi wa utata kuwa ni disputed books ilihali zina sifa zile zile za kuitwa pseudepigraphi na kutakiwa kufutwa kwenye biblia. Mfano Marko 16 inaishia mstari wa 8 ila 9-20 haikuwepo bali iliongezwa miaka mingi mbele na mtu asiyetambulika ila bado kipo kwenye biblia lakini kitabu cha Enoch au Yuda iskariot vimetolewa kwa hoja hiyo hiyo?? Kuna ajenda gani hapa wakuu?? Kipi tunafichwa?? Anyway disputed books kulingana na mwanatheolojia E. P. Sanders ni waefeso,wakolosai,2 wathesalonike, 1 & 2, Tito na vingine vingi.... Je kama vina kasoro kwanini vimeachwa??

VILIANDIKWA NA MUNGU?
Kuna hoja inasema vitabu vya Biblia viliandikwa kwa uweza wa Roho mtakatifu hivyo vile vilivyoachwa havikuandikwa na Roho mtakatifu sasa tujiulize GT kama kuna mistari ya Biblia imeongezwa na wanadamu mfano isaya,wimbo ulio bora,Tito,Yeremia,marko je bado hoja hii ina mashiko ilihali wanatheolojia wanakiri biblia ilichezewa kwa mifano niliyotoa hapo juu na kama si kweli viliandikwa kwa uweza wa Roho bali fahamu za wanadamu je kwanini basi ilitumika kuzuia vitabu kama Injili ya Yuda ama Thomaso?? Je hakuna agenda ya siri kwanini vilizuiwa alafu sisi tukaaminishwa tu kuwa havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu??
View attachment 830349
PSEUDEPIGRAPHI ZINAKINZANA NA BIBLE
kuna hoja ilitolewa kwamba vitabu vya biblia vinakinzana na Pseudipigrapha ndio maana vikatolewa kwenye bible ila cha kujiuliza GT mbona kuna taarifa zinakinzana ndani ya biblia lakini havijatolewa??

MIFANO
Mathayo 4:1-11 inasema mara tu baada ya ubatizo Yesu alienda kufunga siku 40 ila Yohana 2:1 anasema siku tatu baada ya kubatizwa Yesu alikua kwenye harusi ya Cana!!

Au mathayo 27:44 wale wezi wawili walimtukana Yesu ila luka 23:39 inasema mmoja alitukana mwingine alimtetea.

Mathayo 28:9 inasema Yesu baada ya kufufuka aliruhusu Mary amshike ila Yohana 20:17 Inaonyesha baada ya kufufuka na kuonana na mary, Yesu akamzuia kumgusa sababu alikua bado hajarudi kwa Baba!!

Hyo ni mifano tu ila kuna mistari zaidi ya mamia inayopishana taarifa ila vimeachwa kwenye bible lakini pseudipigraphi zikipishana hta neno moja ndio wanajengea hoja kwamba ndio sababu havipo kwenye bible je sababu hii ilisababisha vitolewe ama kuna mengi tunafichwa??

HITIMISHO
Kwa kuhitimisha labda niseme tu kumekuwa na maswali mengi juu ya chanzo hasa cha vitabu vingine kutolewa kwenye biblia na vingine kuachwa wakato vina kasoro zile zile..... Na hata mkuu Pendael24 alishawahi kuhoji kwamba kama tunafikiri biblia imechezewa je Mungu haoni hadi aruhusu hilo?? Na akahoji mbona Biblia inatenda ina maana kazi ya forgery inaweza kuwa na nguvu za Mungu na akanihoji je wachungaji wote hawa wakubwa hawalijui hili kiasi Mungu awaache watumie bibloa iliyochakachuliwa?? Kiukweli nilikosa majibu ila nategemea leo humu majibu yote yatapatikana

NB: Mimi nimechokoza mada tu ili kupata maarifa ya GT ila sio msimamo wangu kuwa bible ni batili au Qur'an ndio sahihi hivyo tunapojadili hoja humu tuhakikishe tunazingatia hilo pia udini na kejeli na matusi sio uwanja wake humu, nataka tujadili kwa kujifunza sio kupambana.

Karibuni kwa mjadala

Zittojr hii Id yako hapa jF inaheshimika sana tu. Naomba ni ambie hii mistari ya Yohana 7:52-8:11 na 12 tatizo lililo onekana hapo ni lipi?
 
Zittojr hii Id yako hapa jF inaheshimika sana tu. Naomba ni ambie hii mistari ya Yohana 7:52-8:11 na 12 tatizo lililo onekana hapo ni lipi?
Mkuu Yohana 7:28 hadi 7:52 inaonyesha Yesu akiwa kwenye dialogue na mafarisayo hekaluni ila ghafla yohana 7:53 hadi 8:11 inaonyesha alishaondoka kabisa hekaluni na kurudi kesho yake asubuhi na ndipo kisa cha mwanamke kahaba kinatokea alafu 8:11 inaonyesha wote wametawanyika alafu kabaki Yesu peke yake na mwanamke yule ila ghafla tena mstari wa 13 Yesu bado ana conversation na mafarisayo hekaluni!

Wakati amebakia mwenyewe?? Yaani matukio ya ile ya 7:28- 7:52 yanaendelezwa 7:13 ikimaanisha hicho kipande hapo kati kilikuwa misplaced yaani kilipandikizwa na sio mimi nayesema hivyo ila biblia zote zinatambua hilo ndio maana zinaweka mabano kwenye kipande hicho ili kukitenganisha na mtiririko wa matukio ya Yohana 7:28-52.

Mfano huu hapa
20180809_154656.jpg
 
Hiki ni kitabu kisichokua na shaka ndani yake na ni muongozo kwa wamchao mwenyezimungu (Qur an),toka enzi hadi ss kiko vilevile na wanaojaribu kukibadilisha wanapata tabu saana
 
Mkuu Yohana 7:28 hadi 7:52 inaonyesha Yesu akiwa kwenye dialogue na mafarisayo hekaluni ila ghafla yohana 7:53 hadi 8:11 inaonyesha alishaondoka kabisa hekaluni na kurudi kesho yake asubuhi na ndipo kisa cha mwanamke kahaba kinatokea alafu 8:11 inaonyesha wote wametawanyika alafu kabaki Yesu peke yake na mwanamke yule ila ghafla tena mstari wa 13 Yesu bado ana conversation na mafarisayo hekaluni!!! Wakati amebakia mwenyewe?? Yaani matukio ya ile ya 7:28- 7:52 yanaendelezwa 7:13 ikimaanisha hicho kipande hapo kati kilikuwa misplaced yaani kilipandikizwa na sio mimi nayesema hivyo ila biblia zote zinatambua hilo ndio maana zinaweka mabano kwenye kipande hicho ili kukitenganisha na mtiririko wa matukio ya Yohana 7:28-52.

Mfano huu hapa
View attachment 831102

Hebu tuambie Yohana 7:53 katika Biblia uliyo nayo hapo/piga picha inasemaje? Kwamba tujue wewe na hao ulio wanukuu kuhusu mistari 50 yenye utata katika Biblia ni wakweli au waongo au wazushi?
 
Hebu tuambie Yohana 7:53 katika Biblia uliyo nayo hapo/piga picha inasemaje? Kwamba tujue wewe na hao ulio wanukuu kuhusu mistari 50 yenye utata katika Biblia ni wakweli au waongo au wazushi?
Hiyo niliopiga picha ya kiswahili huo mstari ulifutwa ila King james version unao huo mstari wa 53
Screenshot_2018-08-09-16-52-22.png

Unasema WOTE WALIENDA MAKWAO

Hapo kumbuka NIV wamefuta karibua sura nzima ya marko 18!! Sasa hapo nani mkweli nani muongo?? Kwanini hautolewi msimamo mmoja wa biblia gani ni feki na ipi ni ya kweli???
 
Hiyo niliopiga picha ya kiswahili huo mstari ulifutwa ila King james version unao huo mstari wa 53 View attachment 831138

Unasema WOTE WALIENDA MAKWAO

Hapo kumbuka NIV wamefuta karibua sura nzima ya marko 18!! Sasa hapo nani mkweli nani muongo?? Kwanini hautolewi msimamo mmoja wa biblia gani ni feki na ipi ni ya kweli???

Nikusaidie John 8:

1Then everyone went home, but Jesus went to the Mount of Olives.

2. Early the next morning he went back to the Temple. All the people gathered round him, and he sat down and began to teach them.

Labda ni typing errors tu. Lakini hukuni jibu swali langu na lirudia hii mistari iko na shida gani?
 
Inasema Yesu alibaki peke yake ila inaonyesha bado anahutubia watu at the same time soma vizuri mstari wa 10-13, ndio maana bible imeweka mabano kwamba hyo story iliongezwa ila ilitakiwa mstari wa 8:13 uwe baada ya 7:52 soma upya uone mtiririko ulivyo

Na hii hoja inakubalika kote mkuu soma footnote za biblia yako utakuta wamecite kwamba upo misplaced
 
Iweke hapa tuione.
 
Biblia Hii Inayotumika Sasa Ina Contradictions Kibao Ambazo Zinaweza Kukupunguzia Imani Yako.

Kwa Ujumla Huwa Nasema Naamini Kuwa ' Yupo Muumba Wa Ulimwengu Na Vyote Vilivyomo ', Awe Ni Mungu Huyu Wa Kwenye Biblia:Sawa, Awe Ni Mwingine:Sawa. Haya Mambo Ya ' Dini ' Ni Pasua Kichwa Tu.

Kusema Biblia Ni Kitabu Kitakatifu Si Sahihi Hata Kidogo, Ni Sawa Ile Katiba Pendekezwa Kutoka Bunge Maalumu!
Kaka una amini kuna watu nyoyo zao zimetulia tuli,kaka Mola hatafutwi kwa mtindo wa voda fasta,Mola anasomwa tena kusomwa haswa. Leo watu wanatumka muda mwingi katika mambo ya kipuuzi,starehe na kuongea umbea umbea tu. Halafu unakuta ana muamini Mola halafu hamjui. Kwanini umuamini Mola usie mjua ? Huo ni uvivu na ujinga usiotakiwa mzee.

Hutakiwi kukata tamaa,madamu una akili timamu,mtafute Mola mpaka umjue.
 
kama biblia imetungwa na mtu basi huyo mtu atakuwa sio mtu wa kawaida
ni kitabu kilichojaa hekima nguvu uponyaji
hakuna kitabu maarufu dunia zaid ya biblia
mimi huwa nasoma kila siku na kupata vitu vipya

tatizo imani ndio shida usipokuwa na iman utaona kama gazet tu
Umaarufu sio tatizo,tatizo ni usalama na ukamilifu. Je Bibilia imekingwa na makosa yaani imekamilika ? Haijapunguzwa wala kuongezwa ?
 
Bwana @zittojunior nafahamu namna unavyoheshimika hapa jf kwa mada tata na vikirishi ila nikusaidie kitu kimoja cheza na mipaka yako katika mambo yanayomuhusu Mungu yaani hapa sizungumzii dini wa dhehebu.

Sijaona utata katika vilivyoandikwa katila bibli kwakua ni vitu vya kiimani na si kisayansi kwamba vinahitaji scientific proof.... Huweizi pata.
Ninauhakika hujisoma biblia ukaielewa nnauhakika hii hoja umeiokota.... Ni kwamba mi si muandishi mzuri ila nishakutana na hoja hizi wakati nafuatilia imani zilizo kinyume na Mungu.....

Ukisoma biblia Agano la kale na jipya limetofautiana kimapokeo tuu lakini kusudio la Mungu lilikua moja tu na bado liko vile vilehata sasa.

Tambu baraza lilipata mamlaka ya kipi kiingie kipi kitoke kutoka kwa Mungu (uvuvio) na huo ndio mpaka wangu wa kuhojik
Hata imani kuna potofu na sahihi,yaani lazima zichekechwe.
 
Zurri Nimesoma Sana Kuhusu Huyo Unayemuita Mola, Waliojaribu Kumuelezea Wameleta Contradictions Kibao, Sifa Anazopewa Na Wenye Dini Zinajikanganya Ndani Ya Vitabu Vya Dini!

Nimesema Kuwa, Kuna Muumba Wa Ulimwengu Na Vyote Vilivyomo ( Sijasema Mola Tafadhali ), Ila Sijui Ni Yupi Kama Ambavyo Simjui Fundi Aliyejenga Nyumba Hii Niliyopo Sasa.Je, Kutomjua Huyo Fundi Unanitaka Niseme Hakuna Aliyejenga Nyumba Hii?
 
Iweke hapa tuione.
Soma hapo chini kabisa wanasema nakala za MWANZO kabisa na BORA kabisa hazina hiyo mistari niliyotaja hapo juu na wanasema tena kwamba hiki kipande kipo eneo jingine kabisa sio hapo simply ikimaanisha hoja yangu kuwa kipo misplaced ni halali.

Sasa cha kujiuliza neno la Mungu lina uwezo wa kuwa misplaced?? Je nani mkweli kati ya KJV na NIV?? Kama watu wanaweza kupachika misplaced content kwenye biblia sasa kwanini vimeachwa kwenye biblia alafu Pseudipigrapha zimetolewa kwa hoja hii hii kwamba baadhi ya sura zilipachikwa hivyo kuondoa uhalisia?

Karibu tuelimishane
20180809_183838.jpg

Cc blackstarline
 
View attachment 831232
Cc blackstarline

Mbona unapata hofu kuiandika hapa.

Nani anayema hayo uliyo ya sema yeye ni nani nabii, mtume, mtu tu wa kawaida? Maana umeleta hapa 7:53, mimi nikakuletea 8:1 yenye maneno ya 7:53 na mengine. Labda tatizo lako ni mpangilo wa namba za hiyo mistari. Kwenye namba ndipo neno lilipo? Au ukiona hiyo namba bila ya maneno umekuwa umeshaelewa hilo neno?
 
mathayo 16:28
yesu alisema uongo
Katika mstari huo Yesu hakusema uongo,aliyosema yalitimia.
Ili uelewe vizuri soma Mark 9:1 "Until they have seen the kingdom of God come with power"
Luke 9:27 "Till they see the kingdom of God"

Hayo yalitimia kuanzia siku ya pentekoste, kanisa lilianza kuenea kwa kasi, hii ikionyesha utawala wa Mungu ukishika hatamu duniani. Mmoja wa wanafunzi wa Yesu aliye itwa Yohana alishuhudia kanisa likienea kutoka Uhahudi mpaka Asia, Ugiriki, mpaka Roma
 
Mbona unapata hofu kuiandika hapa.

Nani anayema hayo uliyo ya sema yeye ni nani nabii, mtume, mtu tu wa kawaida? Maana umeleta hapa 7:53, mimi nikakuletea 8:1 yenye maneno ya 7:53 na mengine. Labda tatizo lako ni mpangilo wa namba za hiyo mistari. Kwenye namba ndipo neno lilipo? Au ukiona hiyo namba bila ya maneno umekuwa umeshaelewa hilo neno?
Mkuu nimeshindwa kuandika nini si nmeshakuonyesha biblia inaposema kuwa mstari uko misplaced ama unataka nikuwekee nini hasa

Yes ni mtu wa kawaida ila Amesoma theolojia na tafsiri yake imekuwa verified kutumika ulimwengu mzima kama ambavyo Vulgate ilitafsiriwa na mtu wa kawaida ila leo hii ndio imezaa biblia ya kiswahili sasa unaanzaje kuhoji waandishi wa NIV ila hauhoji uhalali wa waandishi wa KJV??

Jikite kwenye hoja ni hivi 8:10 tunaona Yesu kabaki mwenyewe ila ghafla anawahutubia watu kufikia 8:12 ndio wanatheolojia wakaona hio text iliongezwa maana kwenye dead sea scroll haipo kabisa hicho kipande yaani kipo misplaced ila naona wwe unapingana na biblia hiyo hiyo unayosema ni neno la Mungu!!

Tutafika kweli
 
Mkuu nimeshindwa kuandika nini si nmeshakuonyesha biblia inaposema kuwa mstari uko misplaced ama unataka nikuwekee nini hasa

Yes ni mtu wa kawaida ila Amesoma theolojia na tafsiri yake imekuwa verified kutumika ulimwengu mzima kama ambavyo Vulgate ilitafsiriwa na mtu wa kawaida ila leo hii ndio imezaa biblia ya kiswahili sasa unaanzaje kuhoji waandishi wa NIV ila hauhoji uhalali wa waandishi wa KJV??

Jikite kwenye hoja ni hivi 8:11 tunaona Yesu kabaki mwenyewe ila ghafla anawahutubia watu kufikia 8:13 ndio wanatheolojia wakaona hio text iliongezwa maana kwenye dead sea scroll haipo kabisa hicho kipande yaani kipo misplaced ila naona wwe unapingana na biblia hiyo hiyo unayosema ni neno la Mungu!!

Tutafika kweli

Hivi ni kuulize mawe watu walikuwa wanapigiwa hekaluni enzi hizo? Hekaluni wangeweza kusema Bwana Yesu akiandika aridhini/ground kwa kidole.

Lakinu kungekuwa na nia ovu/dhamira mbaya yeyote hao walio andika hapo kwenye footnotes wange ta andika waliyo ya andika?
 
There are a number of differences between KJV and NIV:
  1. The language - The KJV was translated into the English of the day (1600's) and the NIV into modern English.
  2. The KJV is a more direct, word-for-word translation; the NIV more "dynamic equivalent" (idea-for-idea).
  3. The KJV used the best Hebrew and Greek manuscripts available at the time and chose a single version. The NIV used the best manuscripts available at the time, including the newly-discovered Dead Sea Scrolls and used footnotes to indicate major differences between manuscripts. This means that some verses found in the main KJV text, are only found in the footnotes of the NIV.
As for the actual content and message, the two translations are essentially the same. If you want a good middle-of-the-road translation, the NIV is a good choice, especially for non-Christians or people unfamiliar with Christian ideas. If you want a authoritative and well-known translation for memorization, or like the archaic language, the KJV is a good choice.
 
Back
Top Bottom