Siri 3 za Mafanikio ya Wachawi na Somo Kwetu

Siri 3 za Mafanikio ya Wachawi na Somo Kwetu

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,114
Reaction score
2,720
1. WAKO MAKINI NA MAMBO YAO.

Hawataki mchezo kwenye harakati zao za uchawi wakiambiwa lazima upatikane unyayo wa paka basi atamtafuta paka siku nzima na kwa gharama yoyote paka ampate.

Lakini wewe ukiambiwa toa chakula kwa mayatima ili ufanikiwe utaanza sababu mia kidogo unaona unapoteza hela alafu unataka Mungu akufungulie?.

2. WANAZINGATIA MUDA WA MAMBO YAO.

Wakiambiana kuroga tunaanza saa sita basi saa tano na robo kashafika eneo la tukio tena akiwa uchi wa mnyama😁. Ila wewe mwenye imani ya kweli ukiambiwa Dua au Ibada saa mbili unakuja saa nne tena kwa kujivuta na sababu nyingi za kipuuzi.

3. IMANI YAO NI KUBWA KUHUSU UCHAWI WAO.

Mchawi ana amini kuwa jambo lake litaenda vizuri hana wasiwasi kabisa na jambo lake. Lakini wewe mwenye imani ya kweli unamuomba Mungu huku una wasiwasi kweli Mungu atanijibu maombi yangu kweli.

Tena unaongeza maneno mabaya rohoni Mungu mwenyewe anazingua mwezi uliopita nimeomba sana hakuna lolote lililotimia😃. Yaani unataka ukimuomba Mungu akupe hapo hapo wewe nani katika dunia hii?.

Jenga imani na Mungu wako wakati wa Mungu kukupa ndio sahihi sio wakati unaotaka wewe kupewa. Mungu ndie anaejua kipi kitakufaa na kwa wakati gani.
 
Tumalizie kwa kusema, tusiache na tusisahau kusali na kuomba dua nyakati zote kuomba kinga ya mwenyezi mungu… 🙏🏾
 
Back
Top Bottom