Sipangi tena nyumba waliyopanga wanawake tu

Sipangi tena nyumba waliyopanga wanawake tu

Na ww ni mwanaumee sema nyie wapangaji wote ni wa kike mwanaume gn unakimbaia hvyo pmbana
 
Kuna jamaa kama wewe alivamiwa na jambazi akakurupuka na kuanza kupiga mayowe,majirani walipotoka kumpa msaada akawa anajisifu nimemvunja mbavu mie wakamuuliza umempiga na nini?Akajibu jibwana lina nguvu sijaona nimempiga na mto mbavuni bado lakimbia tu.
 
Na ww ni mwanaumee sema nyie wapangaji wote ni wa kike mwanaume gn unakimbaia hvyo pmbana

mhhh,maelezo yako yananipa shaka, napata hofu lazima wewe ndiye uliyekuwa unanikimbiza. ebu niambie lengo lako lilikuwa nini ? itabidi uisaidie polisi
 
inaonekana unawazibia watu .ndo maana umeletewa kibaka.kibaka gani anayefukuza mtu kwake.hama haraka
 
mhhh,maelezo yako yananipa shaka, napata hofu lazima wewe ndiye uliyekuwa unanikimbiza. ebu niambie lengo lako lilikuwa nini ? itabidi uisaidie polisi
Nilikuwa nakutisha tuuu coz niliona unajisifu mno kwa wapangaji kuwa una nguvu
 
Nadhani hao wadada nao watakuwa wanapanga kuhama baada ya kuona mwanaume waliyemtegemea kama kamlinzi kao kapigishwa mduara bila hiana,ni bora ungekimbia ukaenda mbali kuliko kuendelea kuzunguka nyumba.

Hahaaaaaaaaa yaani nimecheka kama chizi. Daa Jf noma
 
"akaishia tu kusema bahati yako" nami nikamjibu nawe bahati yako"

Kama namuona anavyomjibu na we bahati yako, sijui alikua anamchungulia kwa dirishani Hahaaaaaaaaa

Hahaha ni shiiidah mi nachoshangaa mkuu alipata wapi ujasiri wa kumwambia "bahati yako" wakati ye ndo kashikiwa panga huku anakimbizwa na kupiga mayowe
 
Kilichonikuta leo sina hamu ya kupanga nyumba ambayo wapangaji wake ni wanawake tu. Nyumba niliyopanga mwanaume nipo peke yangu kati ya wapangaji saba , wengine ni wanawake ambao hawajaolewa ila wana familia zao.

Tulikuwa tumekaa uwani tuna piga story mnamo kama saa 2 usiku. ilipofika saa tatu kama kasoro robo niliwaacha wenzangu na kuamua kwenda haja ndogo kabla ya kwenda kulala huku wenzangu nikiwaacha wakiendelea kupiga story uwani.

Wakati narudi sasa uwani nikitokea chooni mbele yangu nilimwona mtu kashika upanga mkononi, nikasimama wakati natafakari huyu ni nani na lengo lake nini ghafla akaanza kunikimbiza ikabidi nirudi nyuma nianze kukimbia huku nikipiga kelele za kuomba msaada toka kwa wapangaji wenzangu.

Tukawa tunakimbizana na yule kibaka huku tukizunguka nyumba nilipofika mlangoni kusukuma mlango haufunguki, kumbe wenzangu wamefunga mlango na kukimbilia ndani, ikabidi nipitilize huku nikipiga kelele wanifungulie mlango na huku yule kibaka akiendelea kunifukuza.

Nilipofika mara ya pili tena mlango haujafunguliwa nikapitiliza tena na kibaka naye yupo nyuma, bahati nzuri nilipofika awamu nyingine nikakuta mlango umefunguliwa nikasukuma na kuingia na kufunga mlango haraka alipofika yule kibaka akakuta mlango umefungwa na akaishia tu kusema bahati yako huku na mimi nikimjibu na wewe bahati yako.

Kijana mdogo wa kiume wa darasa la tano ndiye aliye nifungulia mlango baada ya kusikia kelele za kuomba msaada. Wale wadada wengine wamejifungia milango vyumbani kwao.

Nilichukia sana na kama si yule mtoto kunifungulia mlango sijui ingekuwaje na yule kibaka. Kweli nimeamini wanawake wengine si watu wa kuwategemea katika kutoa msaada. Nimepanga kuhama nyumba hiyo naenda kutafuta nyumba ambayo ina wapangaji wanaume au mchanganyiko wa nusu kwa nusu.

Huo ni uongo kibaka uwe kwako akukimbize round 3? Alikuwa anataka roho yako au pesa? Basi atakuwa mume mwenzio mnachukuliana hao wadada wapangaji uliozoea kuona mapaja yao!!
 
Kibaka anajua ile nyumba ya wanawake tupu, kwa hiyo alidhani na wewe mwanamke, na ole wako maana angekubaka mpaka ungekoma. Hahaaaa
 
Back
Top Bottom