Sipangi tena nyumba waliyopanga wanawake tu

Sipangi tena nyumba waliyopanga wanawake tu

ligera

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
2,646
Reaction score
1,173
Kilichonikuta leo sina hamu ya kupanga nyumba ambayo wapangaji wake ni wanawake tu. Nyumba niliyopanga mwanaume nipo peke yangu kati ya wapangaji saba , wengine ni wanawake ambao hawajaolewa ila wana familia zao.

Tulikuwa tumekaa uwani tuna piga story mnamo kama saa 2 usiku. ilipofika saa tatu kama kasoro robo niliwaacha wenzangu na kuamua kwenda haja ndogo kabla ya kwenda kulala huku wenzangu nikiwaacha wakiendelea kupiga story uwani.

Wakati narudi sasa uwani nikitokea chooni mbele yangu nilimwona mtu kashika upanga mkononi, nikasimama wakati natafakari huyu ni nani na lengo lake nini ghafla akaanza kunikimbiza ikabidi nirudi nyuma nianze kukimbia huku nikipiga kelele za kuomba msaada toka kwa wapangaji wenzangu.

Tukawa tunakimbizana na yule kibaka huku tukizunguka nyumba nilipofika mlangoni kusukuma mlango haufunguki, kumbe wenzangu wamefunga mlango na kukimbilia ndani, ikabidi nipitilize huku nikipiga kelele wanifungulie mlango na huku yule kibaka akiendelea kunifukuza.

Nilipofika mara ya pili tena mlango haujafunguliwa nikapitiliza tena na kibaka naye yupo nyuma, bahati nzuri nilipofika awamu nyingine nikakuta mlango umefunguliwa nikasukuma na kuingia na kufunga mlango haraka alipofika yule kibaka akakuta mlango umefungwa na akaishia tu kusema bahati yako huku na mimi nikimjibu na wewe bahati yako.

Kijana mdogo wa kiume wa darasa la tano ndiye aliye nifungulia mlango baada ya kusikia kelele za kuomba msaada. Wale wadada wengine wamejifungia milango vyumbani kwao.

Nilichukia sana na kama si yule mtoto kunifungulia mlango sijui ingekuwaje na yule kibaka. Kweli nimeamini wanawake wengine si watu wa kuwategemea katika kutoa msaada. Nimepanga kuhama nyumba hiyo naenda kutafuta nyumba ambayo ina wapangaji wanaume au mchanganyiko wa nusu kwa nusu.
 
Sasa wewe dume zima kweli unakimbizwa hivyo tena viunga vyako na mbele ya wadada?? Wao walikutegemea ila ndo cv ushaharibu!! Inapokuja suala la FIGHT or FLIGHT, mwanaume unapigana!! Ila pole, pia licha ya kasoro hiyo ya kuwa na madada, ila nina uhakika kuna kafaida fulani unakapata, ha haaa haaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
mkuu mwenzako ana upanga mkononi na wewe hata fimbo huna unafanyaje ? , hata jkt wanafundishwa mbinu ya mwisho kabisa vitani baada ya kutumia mbinu zote imeshindikana ni kutimua mbio.
 
Hapo ndo sitakagi usengerema wa alikufa kishujaa
 
Yaani nyumba nzima mwanaume peke yako! Mnakaa uani kupiga story mpaka usiku! Naomba weka sawa kumbukumbu zako, hiyo nyumba haikuwa hata na mwanaume mmoja!
 
mkuu mwenzako ana upanga mkononi na wewe hata fimbo huna unafanyaje ? , hata jkt wanafundishwa mbinu ya mwisho kabisa vitani baada ya kutumia mbinu zote imeshindikana ni kutimua mbio.

mkuu, umenifanya nicheke asubuhi subuhi hii.
Aisee
 
'unapiga nao stor uani,kibaka anakukimbiza unatarajia wakuokoe' at last kijana wa mwanamke mwenzio kakuokoa,soon mahar
 
mimi nilifikiri umewapanga kumbe unacheza nao karata za kuoana
 
Ha ha haaaa,kibaka na panga ww na toi,duh kweli kumekucha mkuu
 
Back
Top Bottom