Sioni umuhimu wa daraja la Aga Khan - Coco beach kwa sasa


Quinine

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Messages
16,505
Points
2,000
Quinine

Quinine

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2010
16,505 2,000
Kwa macho ya kawaida unaweza kufikiri lengo la daraja hili ni kupunguza foleni ya Salender Bridge na kuwaondolea wananchi wa Dar kero ya foleni. La hasha daraja hili linalojengwa kwa gharama kubwa halitapunguza foleni kwa sababu watakaotumia daraja hili ni idadi ndogo sana ya wakazi wa jiji la dar es salaam.

bridge-pic-jpg.972803

(under utilised bridge?).
Ukiangalia kwa jicho la tatu, lengo hasa ni kuwasaidia viongozi, mabalozi na wazungu wachache wanaoishi maeneo ya Osterbay na Masaki ambao hawazidi hata 200, labda wasikae kwenye foleni kwa muda mrefu wakichanganyika na walalahoi wa maeneo ya Mwenge, Kawe, Kunduchi, Tegeta, Boko na Bunju.

USHAURI: Kama lengo ni kupunguza foleni ya Salender Bridge ingefaa zaidi lijengwe daraja kubwa la nchi kavu kutokea maeneo ya Hananasifu au Magomeni hadi Muhimbili au Fire kuvuka bonde la Jangwani linalojaa maji kipindi cha mvua.

Daraja hili la Hananasifu - Muhimbili/Fire, lingehudumia watu wengi hasa wafanyabiashara wa Kariakoo na katikati ya jiji, ambulance, zimamoto na wafanyakazi wa kada za chini ambao ndio walio wengi, tofauti na daraja la Aga Khan - Coco beach ambalo litahudumia 'sana sana' wakazi wa Masaki na pengine kubaki 'idle' kwa kipindi kirefu.

Daraja kubwa la Jangwani si tu lingepunguza adha ya foleni ya Magomeni-Kariakoo/Posta lakini pia lingesaidia kupunguza magari yanayopita Salender Bridge.

Anyways kupanga ni kuchagua, tumechagua daraja la Coco beach kwa wadosi tukawaacha wa Mbagala wahangaike na foleni yao.

Ni ushauri na mawazo huru ya MwanaJF mzoefu Quinine.
 
C

chopspuro

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2018
Messages
277
Points
250
C

chopspuro

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2018
277 250
Serikali haitekelezi miradi kwa ajili ya muda huu pekee ina fanya even for furure ndio maana hata Japan wametengeneza Train inayo kimbia km 360 per hour lakini itaanza kutumika by 2030
 
P

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2006
Messages
9,316
Points
2,000
P

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2006
9,316 2,000
Daraja halina maana ile pesa wangepeleka kwenye matatizo zaidi
 
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
4,325
Points
2,000
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2011
4,325 2,000
Mpwa nakafahamu kale ka njia, ule ni uchochoro, hautapunguza foleni popote pale
Sio lazima kule kwenye uchochoro. Watu watapita hata St Peters au Dar Free Market kukwepa Salenda Bridge. Huu mradi utasaidia sana. Ngoja tuone
 
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
20,239
Points
2,000
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2011
20,239 2,000
Hata mwendokasi mlipinga,ndege mlipinga
Ajabu mnakua wa kwanza kutumia
 

Forum statistics

Threads 1,295,454
Members 498,335
Posts 31,212,570
Top